Yaani katika maisha ya shule haya unatakiwa uwe mvumilivu sana kwa sababu wengi wetu hatukuweza kukaa wa wazazi hasa wakati wa kusoma elimu za juu na vyuo! nakumbuka nikiwa high school nilikaa kwa kakangu/binamu, duh! kama sikuwa mvumilivu basi maisha yasingeenda huyo shemegi yangu alikua noma, akimtia-tia maneno broo ili niondoke pale kaka alishaanza kubadilika lakini shangazi (mamake) alikua makini akamwambia awe na subira tu kwani siku zenyewe chache. Kisa hapa "eti house girl ananipenda mimi zaidi kuliko wao mabosi" yaani nilivumilia wala sikulalamika hata kwa baba yangu (R.I.P) kwa sababu asingeniruhusu kukaa tena pale kwa jinsi alivyokua akinipenda, mama ndio usiseme..Hutokea wivu lakin binadamu unatakiwa uishi nae kwa akil sana......ukipanga ratiba yako vizur na ujishughulishe na shughul za nyumbani wataishia poroji tu hapo ndo pakuwabaini.
Nakubaliana na wewe, huyu binti kama alivumilia tangu primary mpaka first year chuo, unashindwa nini kuvumilia kwa miaka miwili au mitatu iliyobaki? Kwa nini asitafute room hostel kama nyumani hakukaliki? \inawezekana kabisa nyumbani kwao pamekuwa pagumu lakini pia inawezekana anatafuta moral support ya kwenda kuishi sehemu anayoiona ina uhuru zaidi wa kufanya mambo yake yasiyo ya kishule. Ni bora avumilie na kukaza kwenye masomo au kama mambo ni magumu zaidi amwombe mjomba wake amtafutie hostel.
Haya mambo ya kupanga chumba kwa mtoto wa kike tena wa first year, kuna madhara makubwa na hasa mjomba atakapokasirishwa na kitendo cha kuhama nyumbani na kuamua kusitisha huduma, anaweza kuishia kujiuza.
Ushauri mzuri, ila huenda uncle naye ameanza kale ka tabia ila ameshindwa kusema wazi wazi hapa, si bora akapange akimbie ufataki?
%%%ANGALIZO%%%
Ni kweli mtoto wa kike kupanga, kuna mambo mengi, achukue uamzi wa busara, hana wazazi? kama wapo aende kwao, kama hamna, akafunge novena kabla ya kuamua.
Habari ya jioni wana jf. Naomba ushauri. Naishi kwa uncle ambaye ni kama baba yangu kanisomesha toka primary mpaka chuo first year namshukuru kwa hilo sana. Nimeishi nae kutoka 2006 mpaka sasa miezi ya likizo. Uncle hana tatizo lakini kuanzia shangazi, ndugu yake shangazi na wasichana wake wa kazi wamenifanya nichoke kabisa kuishi pale. Nimemwambia uncle kuwa maisha ya pale kwake yamenishinda nataka nikaishi sehemu nyingine tofauti na pale. Kanijibu mtoto wa kike haachi wazazi wake na kupanga pia dharau.
Siko mbali sana na wadau wengine naona ni vema ukaendelea kukaa hapo kwa mjomba wako. Kama umekaa hapo kwa muda huu wote jiulize kwanini wamebadilika , pengine wewe mwenyewe umechange. Kosa ulilofanya ni hapo ulipomwambia uncle wako kua hapo home pamekushinda hii si lugha nzuri. Ungetaka mjomba wako akubaliane na wewe kwamba mkewe ana tatizo wakati umekaa nao muda huo wote? Kumbuka uvumilivu siku zote unalipa na si vizuri hata kidogo kuwalaumu unaoishi nao hata kama wanakunyanyasa, wewe ni kijana/binti mkubwa sasa . Kumbuka hao si wazazi wako hivyo yakupasa uwavumilie na ujaribu wakati wote kuongea kwa busara na mjomba wako. Hata akiona umenyanyaswa na akakuuliza unaonaje maisha ya nyumbani we sema mazuri tu tena namshuru sana shangazi amekua msaada sana kwangu. Tumia muda wako mwingi chuoni au kwa marafiki zako na bila kusahau kushirikiana na hao wadada wa kazi uwapo home. Kumbuka mtaka cha uvunguni sharti ainame
Jasmini huna boifriend?