mkuu na mimi nina tatizo kama lako nimeshafanya kila kitu na paypal walishanikata $1.9 lakini code ndo sipati sielewi nifanyeje
Wakuu kwa aliyefanikiwa kufanya verification ya CRDB VISA card kwenye PayPal na akafanikiwa anisaidie, mimi inanipa msg "billing address doesnt match with paypal street address. NB: hii card nishaiauthorize crdb ifanye transaction online!
Well Said kabisa... Ila ni vizuri wasubiri kama five days ndo wakaombe full statement... Am not sure kwa CRDB kama wanaweza kutoa Statement ya current month kabla mwezi haujaisha.Kama ulisha activate card yako itumike online na Paypal wakakukata hela kidogo. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua bank statement. Kwa mfano kama paypal wamekata pesa leo wewe tulia halafu nenda kesho au kesho kutwa benk uombe statement ya kuanzia tarehe ya nyuma ambayo paypal wamekukata. kwenye statement yako tafuta transaction za VISA/MasterCard utona zile CODE tarehe na amount.
HIZI CODE HAZIPATIKANI KWENYE VILE VI STATEMENT VYA KWENYE ATM.
Mkuu Nyasiro mimi nimeactivate itumike online lakini nikiende kufanya verification ya card kwenye Paypal inanipa hiyo message ya Billing address haimatch na street address ya paypal. NIFANYEJE HAPO?
Pole sana lakini mimi sijawahi kukutana na tatizo kama lako. Labda uangalie tarifa zako ulizojaza kwenye paypal ni sahihi.