Msaada: Nna tatizo gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Nna tatizo gani?

Discussion in 'JF Doctor' started by toghocho, Oct 15, 2012.

 1. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa na tatizo la kuteswa sana linapokuja swala kwamba naumwa mafua...hii imekuwa muda mrefu tangu niko sekondari.
  taitzo liliongezeka baada ya kuwa kila nnapougua malaria lazima iambatane na mafua, na kufanya kuwa even worse.
  tatizo ni kwamba kila nnapougua mafua nakuwa so weak, yaani siwezi fanya kitu cha maana (hii nliambiwa ni normal)

  baadaye nikawa mpenzi wa juisi za azam hizi za lita moja, tena za baridi...nkawa napiga angalau kwa wiki mara mbili lazima nipate azam mango.
  nikaanza kupatwa na tatizo la koo, yaani nahisi kama kuna stick imekwama...nkaonana na dakatri...hakunipima, akadai ni minyoo, akanipa dawa za minyoo, tatizo likakoma, baada ya muda likarejea tena, safari hii nkawa nahisi kama kuna kitu kinanikaba, nkanunua dawa za minyoo nkameza likaisha, likaanza baada ya muda mfupi, nkarejea hospitali...dokta mwingine..akanikoromea na kusema sio minyoo, akanipa antibiotics, akisema njia ya hewa imechafuka..
  nkameza tatizo likaisha, likarejea baada ya kama miezi mi2, nkaona uzushi kwenda hosp. nkanunua antibiotics nkameza...nkawa normal..ikawa hivyo mpaka mwezi wa 6 mwaka huu nlipomeza mara ya mwisho na tatizo likaendelea kidogo, kisha likakoma..
  sasa huwa nalisikia kila ninapokunywa vitu vya baridi sana, au pombe mara zingine.
  kitu kingine ni kwamba, sasa siugui mafua tena, yaani tangu mwezi wa sita, nikipata vumbi napiga chafya basi..sijawahi kuugua mafua tangu hapo, tofauti na zamani ilikuwa haichukui miezi mitatu, then juzi nimeugua malaria, lakini haikuambatana na mafua, dalilli za mafua nilizisikia but cha ajabu sikupata ugonjwa wenyewe,
  naombeni msaada, nina tatizo gani, na je kama sina hela ya kwenda hospitali kwa sasa nn madhara yake? maana mie ni mzima isipokuwa nasikia kitu kwa mbvali kooni.
   
 2. Isaac Chikoma

  Isaac Chikoma JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uvimbe kooni unaweza kuwa tonsils,kutokana na kutumia vitu vya baridi,ukipatwa na ugonjwa kama malaria unaweaken immune system,inakusababishia kusumbuliwa na magonjwa kama mafua,epuka vitu kutumia vitu vya baridi, kuhusu vumbi, unaweza kuwa na allergy,unaweza kwenda kupima allergy,ukapatiwa dawa kama cetrizine,kama ni tonsils,muone daktari wa uhakika atakuandikia dawa nzuri za koo,jaribu maethodex longez,za kumumunya.
   
Loading...