Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Dalili gani?

Utajuaje dalili ambazo hujaziona?

Wewe ni mtaalamu wa forensic science?
Mfano mgonjwa anatamka na hisi sehemu ya mwili inauma tangu jana lazima utaelewa kuwa hizo ni dalili za ku umwa
 
Mkuu,

Dawa ya uchawi ni Yesu Kristo pekee.

Ngoja nami 'nishee' nawe stori kama yako iliyonipata mwaka 2013. Ilikuwa hivi;
1. Baba yangu alinunua shamba kijiji cha mbali kidogo na kijijini kwetu. Aliyemshawishi kununua shamba hilo ni rafiki yake. Jina lake anaitwa mzee Chai (siyo jina lake halisi).
2. Katika mauziano ya shamba, baba hakumshirikisha mzee Chai ila alimtaarifu baadaye juu ya manunuzi hayo. Haya yalitokea kama miaka 15 hivi iliyopita.
3. Baadaye mzee Chai akaomba kulilima shamba hili sababu lilikuwa karibu na nyumbani kwake. Baba alimruhusu kwa masharti kwamba atakuwa anarejesha kiasi fulani cha magunia ya mahindi kama malipo kwa kutumia shamba. Walikubaliana na maisha yakasonga.
4. Mwaka 2010, baba alifariki dunia. Mwaka mmoja baadaye mzee Chai akasitisha kupeleka nyumbani marejesho ya mavuno yake kama walivyokuwa wamekubaliana na marehemu baba. Nilipomuuliza sababu akanijibu haoni sababu ya kuendelea kuleta marejesho kwa kuwa amekuwa anavuna kiasi kidogo sana.
5. Kama familia, tukamtaka arudishe shamba letu ili tumpatie (kumkodisha) mtu mwingine. Aliposikia hivi akaja juu na akanitishia 'kunitengeneza'. Pia akadai kuwa shamba hilo ni lake sababu walikubaliana hivyo na marehemu baba. Kifupi ni kuwa alitaka kutudhulumu kwa sababu alijiamini na 'silaha' zake. Nilichomjibu ni kuwa kwanza, shamba ni letu kwa sababu tuna uthibitisho wa umiliki wake (tunazo hati za mauziano). Pili, hataweza 'kunitengeneza' sababu aliye ndani yangu ni mkuu zaidi ya vyote pamoja na 'silaha' zake.
6. Nilichoamua kufanya baadaye ni kumtafuta mzee mmoja hukohuko kijijini na nikamueleza 'stori' yote na pia nikamuomba aende kwa mwenyekiti wa kijiji lilipo shamba ili wamwite mzee Chai na kuongea naye.
7. Mzee Chai alipoitwa aling'ang'ania kuwa shamba ni lake na mke wake akathibitisha hilo mbele ya viongozi wa kijiji. Kikao hicho kikaamua kuwa kwa kuwa kila mmoja anadai shamba ni lake, basi kila mmoja alete ushahidi wa madai yake.
8. Nilituma 'copy' ya mauziano siku chache baadaye. Ilikuwa kama saa saba hivi ya siku hiyo. Usiku wa siku hiyohiyo kama saa nne hivi usiku nilipata ajali mbaya sana pale Tazara mataa kama unaenda uwanja wa ndege, Dsm. Nilikuwa naendesha gari, Toyota Carina, kutoka uelekeo wa uwanja wa ndege kuelekea Temeke. Niligonga ukuta wa barabara karibu na mataa ya Tazara, gari ilipaa ikatua katikati ya barabara ( ikaziba barabara ya kutoka uwanja wa ndege). Nilipotua tu nikaona lori linakuja kwa kasi toka uwanja wa ndege na lilikuwa linakuja kugonga ubavuni mwa Carina. Mungu mkubwa lori likanikosa na kupita pembeni upande wa Azam. Injini ya gari ilipasuka pamoja na 'gear box'. Matairi yote yakapasuka. Mimi nilitoka nikiwa mzima sijachubuka kata kidogo.
9. Kesho yake mchana wakati nashughulika kutoa gari polisi, mzee Chai alinipigia simu. Sikuweza kupokea simu yake sababu nilikuwa 'bize'. Jioni yake nikampigia na katika maongezi yetu nikamwambia shamba ni mali yetu hatoweza kamwe kulidhulumu.
10. Mwisho alikuja omba radhi kwa uongozi wa kijiji na familia kwa kudanganya na kujaribu kudhulumu shamba letu. Kwa sasa, bado analilima shamba lakini kwa makubaliano mapya na familia yetu. Tuliamua kumpa yeye mwenyewe, mzee Chai.

Ndugu, hakuna jambo linaloshindikana kwa Yesu.


Tafakari.

 
MWENYEZI MUNGU ndio muweza wa tatizo lako,mkimbilie kwa amani kila kitu kitakuwa sawa na utapata haki yako bila gharama..
 
 
mpe matibabu kwanza anko wako mengine yatafuata na kwenda vizuri..
 
ukimuona njiani mwagie petrol na umchome moto, uko shinyanga nini
 
 
 
Kabla ya mgonjwa kumuona dokta lazima akutambulishe dalili kuwa anaumwa nn..then utamshauri kuwah hospital

Hujajibu maswali uliyouliza, uliyojibu hujaulizwa.

Ukishindwa hili tu, utajua dalili zote za magonjwa yote?
 
Wewe ni daktari? Unajua magonjwa mangapi?

Mimi sio dokta ila na utimamu wa kelewa kuwa mtu yupo normal au anaumwa...
Hospitali kuna vifaa tiba vya kutambua ugonjwa kwa undani zaidi...
 
Hujajibu maswali uliyouliza, uliyojibu hujaulizwa.

Ukishindwa hili tu, utajua dalili zote za magonjwa yote?
Nikuulize mkuu wewe kwa mfano nduguyo anakohoa mara kwa mara na yupo nyumbani
Je kwa utimamu wako utaelewa nn hapo??
 
Mimi sio dokta ila na utimamu wa kelewa kuwa mtu yupo normal au anaumwa...
Hospitali kuna vifaa tiba vya kutambua ugonjwa kwa undani zaidi...

A false sense of competence is characteristic of ignorance.

While the real doctors would be second guessing every hue of every hair in search of exellence.
 
A false sense of competence is characteristic of ignorance.

While the real doctors would be second guessing every hue of every hair in search of exellence.
Sio kweli mkuu before somebody to be patient there must be pre features to show up how deep disease is

Na ndio maana unampeleka hospitali baada ya kuhisi dalili
 
Sio kweli mkuu before somebody to be patient there must be pre features to show up how deep disease is

Na ndio maana unampeleka hospitali baada ya kuhisi dalili

Wewe unafahamu dalili zote za magonjwa yote?

Na una uwezo wa kumuina mtu mpaka ndani ya mwili wake hata pale dalili zisipoonekana kwa nje?
 
Mi sijaona sababu ya maana ya kuja kuomba msaada humu hali ya kuwa ushajiridhisha kwa kuamini kuwa kinachomsumbua Anko wako ni uchawi,na wewe ni muumini wa ukristo hivyo ungeenda kutafuta msaada wa hayo matatizo uliyonayo sehemu husika katika dini yako,kuliko kuleta tatizo lako humu kwenye watu wenye imani tofauti na mitazamo tofauti..matokeo yake ndiyo kama unavyoona wengine wanakushauri umuuwe huyo mama,wengine wanakwambia uende kwa mganga,wengine ndiyo wanakwambia hakuna uchawi kabisa.
 
Hivi kama kweli uchawi ni uzushi tu mi najiuliza maswali:

1.Je, ni wapi palipoanzia uzushi huu hadi ukasambaa dunia nzima?
2.Je,ni njia gani ilitumika kusambaza uzushi huo hadi ikafanikiwa dunia nzima?
3.Kama zama hizo watu waliamini uchawi kwa sababu ya ujinga je,vp sasa hivi bado watu wanaendelea kuamini huo uchawi?
 

Pande zipi unapatikana ? nikuelekeze kanisani umlete huyo anko wako tuzivunje kazi za ibilisi huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…