Msaada: Nini maana ya treasury bill (hati fungani)?

NImelisikia sana hili neno kwenye Tegeta-Escrow. Je, kwa kiingereza linaitwaje?
 
Hatifungani in english is known as BOND'bond is the face value certificate of loan to the government issued through discounted bills.sometimes the goverment may having a shortage of funds so it issue bonds to the public to raised fund to finance a concernd issue
 
sina hakika kama ni jukwaa sahihi,lakini kwa kuwa ni hoja mchanganyiko panaweza kufit hoja yangu,
hivi karibuni tu kuna msemo ambao umeanza kupata umaarufu hata bungeni unatumika,'hati fungani'hili neno limeniacha kidogo,japo linahusika na masuala ya kibenki,mwenye aidia nalo naomba msaada.
 
Bid bond/Bank Guarantee/Advance payment bond etc. ndio nadhani hio ndio hati fungani. Zinatumika zaidi kwenye contracts/Tenders etc.
 
Hati fungani au Bond(kwa kiingereza) ni utaratibu unaotumiwa na makampuni au serikali kukopa pesa kutoka kwa wananchi. Wale wanaonunua hizi hati wanakuwa wakopeshaji wa hiyo kampuni, kwa maana kwamba badala ya kampuni kukopa pesa benki, wanaweka utaratibu wa kuwawezesha wananchi kutoa pesa kwa makubaliano ya kuwarudishia hiyo pesa yao pamoja na riba kwa muda maalum.

Hati fungani inaweza ikatolewa na serikali kuu(Government bond), serikali za mitaa( Municipal bond), kampuni(corporate bond) au serikali ya nchi za nje(Euro bond).

Hati fungani utofautiana na hisa(share) kwa maana kwamba wenye hisa ndo wenye kampuni(debtors) kwa hiyo wao wanalipwa faida pale ambapo kampuni imepata faida na pesa yao hukatwa pale ambapo kampuni imepata hasara wakati wenye hati fungani ni wakopeshaji(creditors) kwa hiyo wao kulipwa faida haijalishi kampuni imepata hasara au la.
 
asante sana mkuu.. barikiwa sana
 
Mkuu ungeandika kiswahili tu....
 
Upo vizuri mkuu maelezo yako.
Ila kwenye muda huwa inategemea na Serikali jinsi ilivyopanga muda wa kurudisha hizo pesa na ukubwa wa riba kulingana na muda wa kuiva kwa hati fungani.
 
Nimeona niifufue hii mada ili tujifunze zaidi, ili mtanzania wa kawaida anunue treasury bills au bonds anatakiwa kuwa na sh. Ngapi? Pia napenda kufahamu huwa zinatangazwa kuuzwa kupitia chombo gani cha habari?
 
Nini maana yake? Hapa naona umuhimu wa shule...
 
Kwa mwenye uelewa wa masuala ya kiuchumi na kiuhasibu, hivi hati fungani ni nini? Na inaivaje ivaje?
 
Pale hati fungani zilizoiva inapogeuka kuwa mapayo ya serikali
 
Tuliosoma engineering hapa tunaona nyota tu, ngoja niende lunch nikirudi nitasoma tena
 
Kwahiyo CAG Assad ni mbumbumbu kiasi cha kushindwa kutambua uwepo wa hati fungani zilizoiva..
 
huwa mnada unafanyika wapi? huwa wanatangaza wapi hayo mauzo? Swali kwa niaba ya Saint Kayumba wote [emoji23] [emoji23]
 
Kwa ninavyojua mimi, hati fungani ni hati inayotolewa baada ya maharusi kumaliza fungate. Ndo wanapewa hiyo hati fungani na mkemia mkuu.... Ila sijui. Nimetoa tu maoni yangu jamani, aah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…