Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Wakuu habari!!Najua humu hakiaribiki kitu...Najua nitapata mawazo na muongozo bila kejeli
Wakuu nimetamani sana kwa muda mrefu kuitembelea nchi ya Botswana na hasa mji wa Gaborone
Hii imekuwa ndoto ya muda mrefu sana,mwaka huu mwezi wa Tisa Mungu akitupa uzima,ninataka nifike nchi hiyo na kukaaa siku 14 tu.
Nimesikia sifa nyingi za nchi hii.Ningependa ktk ujana wangu nifike na kujifunza,ili nijifunze mambo mengi,nimeazimia kwenda kwa njia ya basi.Toka Dsm mpaka Botswana.
Ninaomba kujua:
a)Nauli makadilio ni bei gani mpaka Botswana?
b)Niandae bei gani kwa nyumba za kulala za kawaida ktk mji huo?
c)Je kwa Mtanzania ninaweza kwenda Botswana na kuamua pia kutembelea S.Africa na kuamua kurudi tena Botswana.
*Mana kuna mtu kaniambia kuna mji mdogo unaitwa Kanye naweza kukaa hapo na kwenda South
d)Nchi hii inahitaji Visa kwa Watanzania?Kuna ubalozi wa Tz huko Gaborone
e)Je usalama upo vipi kwa raia wa kigeni?
Addendum:Yoyote mwenye ufahamu zaidi ya niliyoyauliza anisaidie.