Msaada: Ninashambuliwa na wachawi

Msaada: Ninashambuliwa na wachawi

Nalifahamu hili mkuu, mimi naomba nifundishe maombi ya kusimamia ili nijue namna ya kutoka kwenye kifungo cha hayo madhambi.
Pia waweza nipa referene mtandao na youtube nivunja maagano haya.
"Toba" huu ndio msingi...anyway nitaona nawezaje kukusaidia hapo baadae kidogo,..
 
Unachopaswa ni kuhakikisha umepokea Roho mtakatifu. Hii ndio suluhisho la kudumu. Unaweza ukaombewa ukapata suluhisho ila si la kudumu.
Unaweza kwenda kwa mganga ukawashinda kakini tatizo lingine likazaliwa.
Jinsi ya kujazwa Roho mtakatifu ni kwamba mpokee Yesu na tubu dhambi kwa upya. Kisha unaweza kupokea kwa kuombewa au itatokea bila kuombewa kadri utakavyokaa kwa Mungu na kujitunza.
Injili kama hii huwa siielewi!
Ni hivi, unaweza kuwa na silaha usipojua namna ya kuitumia adui anakuvamia na kufa ukiwa nayo!
Mtu yeyote ambaye ameokoka, anayeishi maisha matakatifu ana Roho Mtakatifu haijalishi ananena kwa lugha au la. Mtu huyo asipokuwa na maarifa jinsi ya kupambana na adui shetani na mawakala wake ataishia kuwa victim tu.
Afanye nini basi?
1. Ahakikishe Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake
2. Ahakikishe anaishi maisha matakatifu
3. Avae ujasiri na imani kwamba Bwana Yesu yuko upande wake
4. Ajifunze namna ya kuomba maombi ya vita (kwa mamlaka ya Jina la Yesu Kristo na Damu yake, enyi wachawi nawapiga na uchawi wenu na kazi zenu zote. Nawapiga kwa moto na radi ya Yesu Kristo, nateketeza na kuharibu uchawi wenu na silaha zenu zote, kwa jina la Yesu!
(Waumini wa Kanisa la Gwajima wamefundishwa vizuri sana namna ya kuomba maombi ya vita, watafute watakufundisha)
5. Tengeneza network (group) ya wana maombi (siyo lazima kuomba pamoja) hata mkiwa mbali mnaweza kupanga muda wa kufanya maombi kwa wakati mmoja. Muda mzuri wa kufanya maombi ni kuanzia saa 6 - 9 usiku. Pia ukiwa na nafasi hapo nyumbani fanya maombi kabla ya swala ya jioni ya waislamu.
 
Hosea 04:06 " watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa kwa kukosa maarifa, kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi nami nimekukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako mimi nami nitawasahau watoto wako".

Pole ndugu, unasema unasema wewe ni mcha Mungu tena unasema JF ndiyo sehemu sahihi kwako wewe kwa matatizo ya ushirikina! Nashangaa sana kwamba Mungu anayeweza kukuponya na maadui wako yaani washirikina unakuja kumtafuta JF.
No wonder washirikina wanakusumbua.
 
Ukiacha tu utalia sana watakufanya watakavyo. Kama ulikuwa unasali mara 2 sali mara 4 yaani ni mwendo wa kudouble tu.
 
Huyo jamaa pamoja na kumusaidia mawazo mawazo mazuri uliyo mpa ukweli ni kwamba kinacho msumbua si wachawi.kinacho msumbua ni hisia zake na wala hana imani yoyote ni mbabaishaji tu.
Unajifanya huu tambui uchawi Afu unaishi Tanzania, Acha kuifanya punguani wewe
 
Habari zenu ndugu.
Ninaomba msaada kwani maadui zangu ni wachawi wananishambulia kwa namna mbalimbali.
Sina la kufanya ila mimi ni mcha MUNGU, ninasali sana ila kwa sasa nahisi kuchoka.
Naombeni msaada wa mawazo kutoka kwenu najua MUNGU ndie suluhisho la matatizo yangu ila sio vibaya nikafarijiwa na kuonyeshwa namna ya kuomba Zaidi.
Nimekuja JF kwa sababu ni sehemu sahihi.
Dawa ya moto ni moto, wewe unatumia maji(maombi). Elewa yana oxygen ndani, moto utaukoleza.
 
Safii ndugu kurogwa ni habari za kufikirika tu ni ujinga mkubwa kutangaza unarogwa huo ni udhaifu wa imani na akili sisi tunao jiamini haturogwi.ndio maana mnao rogwa njooni mjifunze kwetu tutawafundishwa msirogwe namna dunia inavo kimbia we unahubiri kurogwa leo?kwa nini hambadiliki jamni kurogwa ilikua enzi hizo mbaka leo jamani nyie mnao rogwa mmeganda akili au inakuaje?
 
Habari zenu ndugu.
Ninaomba msaada kwani maadui zangu ni wachawi wananishambulia kwa namna mbalimbali.
Sina la kufanya ila mimi ni mcha MUNGU, ninasali sana ila kwa sasa nahisi kuchoka.
Naombeni msaada wa mawazo kutoka kwenu najua MUNGU ndie suluhisho la matatizo yangu ila sio vibaya nikafarijiwa na kuonyeshwa namna ya kuomba Zaidi.
Nimekuja JF kwa sababu ni sehemu sahihi.
Acha kufikiri kwa habari za wachawi anza kufikiri kwa habari za Mungu wako kwa maana yeye ni Mkuu kuliko wao.Na yeye akiwa upande wako ni nani aliye juu yako change your language anza kuamini utashinda.
 
Habari zenu ndugu.
Ninaomba msaada kwani maadui zangu ni wachawi wananishambulia kwa namna mbalimbali.
Sina la kufanya ila mimi ni mcha MUNGU, ninasali sana ila kwa sasa nahisi kuchoka.
Naombeni msaada wa mawazo kutoka kwenu najua MUNGU ndie suluhisho la matatizo yangu ila sio vibaya nikafarijiwa na kuonyeshwa namna ya kuomba Zaidi.
Nimekuja JF kwa sababu ni sehemu sahihi.
Eti jf ni sehemu sahihi una masihara wewe..!

Kwanza nikupe pole sana kwa yanayokusibu pili nikuulize swali, Labda Mungu yupi unayemuomba ambaye anazidiwa nguvu na waturutumbi/wachawi..??

Nikuonye kwa kukushauri kwanza acha kutenda dhambi, tubu na ujinyenyekeze mbele za Mungu akibaki kuwa msaada wako kwa yale usiyaweza mwenyewe weka tumaini lako kwake. Makosa ya kusali kwako ni haya kwanza utakuwa unasali huku ukiwa unadhambi na kwa imani ndogo labda sababu ya matatizo yako. Kumbuka maandiko yanasema sala/maombi ya mwenye dhambi ni kelele kwa Mungu.

Ila mkitubu kwa kuwa Baba yenu ni mwenye rehema na huruma atawasamehe dhambi zenu. Hao wachawi wanajua udhaifu wako. They know you well..
 
Habari zenu ndugu.
Ninaomba msaada kwani maadui zangu ni wachawi wananishambulia kwa namna mbalimbali.
Sina la kufanya ila mimi ni mcha MUNGU, ninasali sana ila kwa sasa nahisi kuchoka.
Naombeni msaada wa mawazo kutoka kwenu najua MUNGU ndie suluhisho la matatizo yangu ila sio vibaya nikafarijiwa na kuonyeshwa namna ya kuomba Zaidi.
Nimekuja JF kwa sababu ni sehemu sahihi.
Ongeza maombi tu,Mungu huwa hamtupi mjawake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom