Msaada: Nina tatizo la kutokwa mafuta sehemu ya uke

Sep 4, 2016
57
125
Habari za humu ndani,

Naomba ushauri huu ugonjwa siuelewi yaani wakati wa haja ndogo kutoka huchanganyika na mafuta yenye rangi ya mawese na yakidondoka kwenye sink la choo huganda haraka sana nikigusa naona ni mafuta kabisa tena yanaharufu mbaya.

Anayejua anisaidiee plz.
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
29,012
2,000
Habari za humu ndani, naomba ushauri huu ugonjwa siuelewi yaani wakati wa haja ndogo kutoka huchanganyika na mafuta yenye rangi ya mawese na yakidondoka kwenye sink la choo huganda haraka sana nikigusa naona ni mafuta kabisa tena yanaharufu mbaya. Anayejua anisaidiee plz.
Kutokwa na uchafu mweupe au wa kijivu ulio kama maziwa ya mgando ukeni ni tatizo la kiafya, ni dalili mojawapo ya ugonjwa wa fangasi za ukeni kitabibu hujulikana kama Vaginal Candidiasis. Tatizo hili halipo katika makundi ya maradhi yatokanayo na kujamiana (STI), ingawa kugusana kwa kujamiana kunaweza kusambaza. Hata wanawake ambao hawashiriki tendo la kujamiana wanapata tatizo hili.

Kwa kawaida uke wenye afya njema huwa na bakteria rafiki na kiasi cha seli za fangasi (yeast cells), inapotokea mabadiliko ya usawa wa vimelea hawa wa fangasi huanza kujistawisha na kuzaliana. Hali hii huweza kuleta viashiria na dalili za mwasho na kuvimba sehemu za siri. Kutoka uchafu mweupe kama maziwa ya mgando na mwasho huwa ni ndani au nje ya uke, uchafu huo huweza kuwa na harafu mbaya.

Mashavu ya sehemu za siri kuvimba, kuwaka moto wakati wa kutoa haja ndogo au kujamiana, maumivu wakati wa kujamiana, tishu za ukeni kuwa nyekundu, kutoka vidonda na vipele, hizo zote ni dalili. Tatizo hili linawapata wanawake mara kwa mara kutokana na maumbile ya uke yalivyo, huwa ni ya unyevunyevu hivyo mfumo wa ulinzi wa uke huweza kuharibiwa na kuwapa nafasi fangasi kustawi.
 
Handle

JF-Expert Member
May 12, 2020
227
250
Habari za humu ndani, naomba ushauri huu ugonjwa siuelewi yaani wakati wa haja ndogo kutoka huchanganyika na mafuta yenye rangi ya mawese na yakidondoka kwenye sink la choo huganda haraka sana nikigusa naona ni mafuta kabisa tena yanaharufu mbaya. Anayejua anisaidiee plz.

IMG_9054.jpg
 
Utakua na candida nenda hospital watakupatia vidonge na cream ya kupaka pia km hutaenda tumia gynozol cream ujipake uingze ndani kabisa kwenye uke utapata nafuu ni 24 hours
IMG_9055.jpg

Hiyo cream ni kiboko kwa muwasho wowote au hata candida
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
13,131
2,000
Utakua na candida nenda hospital watakupatia vidonge na cream ya kupaka pia km hutaenda tumia gynozol cream ujipake uingze ndani kabisa kwenye uke utapata nafuu ni 24 hours View attachment 1758515
Hiyo cream ni kiboko kwa muwasho wowote au hata candida
Kutumia dawa bila kujua tatizo ni nini exactly hii ni irrational drug use ambayo pia ina madhara.

Aende kwa madaktari wenye experience nzuri watamfanyia examination na ataandikiwa dawa vizuri..Mwili wa mwanamke uko complex kidogo(physiologically).

Tulichomsaidia hapa Jf ni kumwambia kuwa hiyo sio hali ya kawaida ni ugonjwa na inaweza kuwa ni fungal infection(candidiasis).
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom