Msaada: Nimepoteza simu na pochi maeneo ya Tanga Mjini

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
7,724
12,381
Wakuu heshima kwenu,

Nimepoteza simu na pochi maeneo ya Tanga mjini hadi Pongwe, sina hakika ni wapi ila nilipanda daladala alasiri hii. Naomba kujua namna ya kubock simu yangu isiendelee na matumizi tena.IMEI namba ninazo.

NB. Kwenye pochi kulikuwa na vitambulisho,kadi ya ATM na simu (Lenovo)

Kwa atakayeviona, tafadhali tuwasiliane PM.

Asante.
 
Uombe Mungu aliyeviokota awe msamaria mwema.
Nilikuwa kwenye sherehe fulani miezi michache iliyopita. Basi machale yakanicheza niangalie mkwanja nilipouweka sioni. Duh! Akili iliniruka na kijasho chembamba kikaanza kunitoka. Nikaamua kutangaza pale akatoka kijana mmoja na kusema ameokota ule mkwanja na kunirudishia. Nilimshukuru sana na kumpa ahsante yake. Pole sana.
 
Asante mkuu,shida ni hivyo vitambulisho mkuu,simu haina shida sana,maana zipo hata za 25k
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom