Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,333
- 7,885
Habarini wana jamvi. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, jana usiku majira ya saa mbili nilipita mgahawani kwa ajili ya kupata meal. Nilipata chakula freshi tu kama ambavyo imekuwa ikielelekezwa kitaalamu kwamba baada ya kula chakula ndio ushushie matunda.
Sasa baada ya kupiga zangu ugali kisamvu na maharage na dagaa za kukaanga nilisogeza vipande vya tikitiki na kuanza kuvishambulia, wakati nikiwa tayari nimeshamaliza kipande cha kwanza kabla naelekea kula cha pili ndipo niliposhtuka kuskia kma mdudu ananitembelea kwenye vidole. ile kuangalia kwa makini nikaona funza wengi sana wakiwa kwenye mashimo zinapokaa mbegu...
Kwa kuona hivyo tu ni dhahiri tayari nilikuwa nimeshawabugia hata kwenye kile kipande cha kwanza.
Wasiwasi ni kuwa tukio hili halijawahi kunitokea na ndio mara ya kwanza naombeni msaada kama kuna madhara yoyote nifanyeje hili kuyaepuka??
Asanteni.