Msaada; Nilisubmit cheti feki, sasa ninacho original

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
Wakuu,

Baada ya tumbua tumbua ya wenye vyeti fake, kipindi wanahakiki watumishi kwa upande wangu nilijikuta natumia cheti bandia ila kikiwa na matokeo, namba na kila kitu changu ambacho kipo katika matokeo na cheti halisi.

Sasa orodha imetoka na nimejumuishwa, hivyo nimepigania kukifuata cheti changu OG na nimefanikiwa kukipata.

Hivyo nakuombeni JF mnaoelewa suala hili, nimefikiria kukata rufaa ili niweze toa cheti changu halisi na kazi yangu na hali irejee katika hali ya kawaida.

Naombeni mawazo yenu please
 
Wamesema hakitakunusuru, maana mmefutafuta na pia mmetumia vyeti feki kujiendeleza kielimu.
 
wakuu
Baada ya tumbua tumbua ya wenye vyeti fake, kipindi wanahakiki watumishi kwa upande wangu nilijikuta natumia cheti bandia ila kikiwa na matokeo, namba na kila kitu changu ambacho kipo katika matokeo na cheti halisi!

sasa orodha imetoka na nimejumuishwa, hivyo nimepigania kukifuata cheti changu OG na nimefanikiwa kukipata

hivyo nakuimbeni Jf mnaoelewa suala hili,nimefikiria kukata rufaa ili niweze toa cheti changu halisi na kazi yangu na hali irejee katika hali ya kawaida

naombeni mawazo yenu please
Elewe. hapa kosa ni kughushi,na si kutokuwa na Cheti
 
Waziri Kairuki kasema wasilisha cheti kama kile kile kilichoko kwenye file kile kilichokaguliwa
 
ulikua unatikisa kiberitii eeeh.... vp si umeziona njiti mzee babaa sasa tulia ivoivoo... nguvu ulizotumia now kupata original mwanzo ulikua haunazo??? um sorry
 
Kalime bwana ww usaidie viwanda kitendo cha kutumia cheti feki mwanzo kinafanya upoteze sifa za iyo kaz uliyokuwa ukiifanya unastahiri kunyea debe sema tu ndo ivyo jamaa kawastili mm sitetei yoyote mwenye cheti feki isipokuwa yule aliyeonewe
 
Waziri Kairuki kasema wasilisha cheti kamvyetuvle kilichoko kwenye file kile kilichokaguliwa
kwani walikagua vyeti vya kwenye mafaili?? Si walikuja vituoni kuchukua nakala za vyeti vyetu
 
Pole Na hongera....lakini nafikiri kutakuwa na matatizo fulani ya kufikiri na kuamua. Duniani kote,haijawahi tokea mlevi akachinja mbwa(akiwa amelewa) akifikiri ni mbuzi.Lakini bado siamini kama stori yako ni halisia...... Ulipata wapi feki Na huku una Original??
Tulia hiyo imetoka kaka...
Baada ya watumishi wa umma,zoezi linaenda sasa sekta binafsi,usiende huko maana ukidakwa Mara ya 2,adhabu mara 2...
 
Yule katibu utumishi ameeleza vzr sana, kama ulitumia cheti feki katika kupata kazi hicho cheti ulichotumia kupata kazi ndicho kinapaswa kuhakikiwa na siyo kingine, kwa muktaza huo mleta uzi imekula kwako..Pole.
 
Back
Top Bottom