Msaada: Nilimnunulia tecno C8, nimeenda na kumkuta anamiliki Iphone 6

Msaada: Nilimnunulia tecno C8, nimeenda na kumkuta anamiliki Iphone 6

Vanestrooy

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2016
Posts
259
Reaction score
128
Habari za wakati huu ndugu zangu, natumai mko na wakati mzuri kabisa, na Jumapili imeenda vizuri kabisaa.

Niende kwenye mada ndugu zangu nna mpenzi wangu tumekuwa kwa muda mrefu kidogo Anasoma chuo fulani hapa tulipo, sasa mpenzi wangu kuna kipindi alnganganiaa simu saaana alkuwa na ka nokia kake fulani ka tochi nikajitahd kwelii ndugu zangu nikanunua TECNO C8.

Sasa cha kushangazaa hivi majuzi nilimtokea gafla nkamkuta mpenzi ana Iphon6 mpyaaa, mimi mwenyewe sijawai miliki hiyo simu jamani hapa nina ka samsungs3 tena niliachiwaa na jamaa yanguu nikampooza kidogo kidogo mpaka nikamaliza deni...Leo hii mpenzi Anamiliki Iphone kwelii.

Nishaurin jamani km kuna mdau ako na Nguvu kuliko mimi jamanii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemuuliza au unamuogopa. Kama humuogopi muulize kaipata wapi kapata wapi pesa,,,atakuelewesha ukiona majibu yanamashaka ndo uulize,,,sawa mdogo wangu?
 
sasa si alianza na mtaji mdogo mpongeze biashara inakuwa kuliko kumkuta na kitochi mkuu.
 
Kosa kubwa kwanini haujamuuliza je kama ni bumu lake la mwenzu mzima??
 
nadhani kakudhihirishia kuwa ni mhangaikaji...si ndo anafaa huyo lol.
 
Wala usipate shida, tafuta ndugu yako asiye na simu mpatie hiyo C8..

Mambo madogo hayo!
 
Back
Top Bottom