Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Ni zaidi ya mwaka sasa sijapata nafuu

Discussion in 'JF Doctor' started by tindikalikali, Oct 18, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,887
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 135
  Wakuu nimekuwa nikijisikia hovyo mara kwa mara<mate machungu kujaa mdomon, kuumwa kichwa na uchovu>. Kuna kipindi niliugua malaria na ilijirudia rudia sana, nimejaribu kupima magonjwa mengine yote na sina. Nahisi huenda madawa niliyokuwa nayatumia yametengeneza sumu mwilini. Je kuna dawa ya kutoa sumu mwilini? Je suluhisho la haya ni nini? Naomben msaada kwani naelekea kuanza kibarua, kwa hali hii naweza kushindwa kufanya kazi inavyotakikana.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,369
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  pole sana mkuu,subiri matabibu watakuja kukupa majibu
   
 3. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,887
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 135
  asante mkuu, ngoja niendelee kuvuta subira.
   
 4. T

  THE PRINCE Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaamini uponyaji kupitia DAMU YA YESU?
   
 5. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,887
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 135
  naamini mkuu.
   
 6. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  &#8216;Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa &#8211; dr. Batmanghelidj'.

  Kosa kubwa ambalo binadamu tumelifanya dhidi ya miili yetu mpaka sasa, ni kusubiri mdomo ukauke au kiu ndipo tunywe maji. Ni kama vile kusubiri katikati ya mchana jua likiwa limewaka, ndipo unamwagilia maji bustani au kutembea umbali mrefu na gari na kusubiri mpaka maji yaishe kabisa ndipo uongeze maji kwenye injini papo hapo!.

  Madhara makubwa ya kiafya yatokanayo na upungufu wa maji (dehydration) ambayo siyo lazima yaoneshe kukauka kwa mdomo au kiu, yanajitokeza kabla ya mdomo au kiu kutokea.

  Kimsingi kiu na mdomo kukauka, ni ishara za mwisho kabisa za mwili kupungukiwa maji, na ikiwa mtu anategemea ishara hizi ili kunywa maji, basi mtu huyo atakuwa anajikaribishia mauti yasiyo ya lazima, kwani anaulazimisha mwili kusambaziwa maji kwa mgawo kutokana na amri zinazotolewa na ubongo ili kusambazia maji mifumo mhimu zaidi ukiwemo ubongo wenyewe.


  kwa siku huwa unakunywa maji kiasi gani?, je ni chunvi ipi unatumia, ile ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) au ile ya dukani ya unga?, maji ni suluhisho kwa kila ugonjwa, jisomee mwenyewe katika: http://maajabuyamaji2.artisteer.net/jitibu-kwa-kutumia-maji/
   
 7. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,887
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 135
  nashukuru mkuu, nitasoma kwani maji nakunywa lakini inawezekana si kwa mpangilio unaotakikana
   
Loading...