Samahani,
Ni mgeni sijawahi kufika Songea na natarajia kwenda huko wiki ijayo,naomba kufahamishwa ni basi gani zuri kwenda huko kwa ndugu zangu wangoni?
Natanguliza shukurani.
Kama unatokea Dar, Panda Superfeo au Selou...
Na inategemea unataka kupitia Lindi au Iringa. Ukipitia Iringa, toka Njombe kwenda Songea kuna kona kalikali nyingi na bahati mbaya kona hizo mnapita usiku wa kuanzia saa Moja. Ruti ni Dar-Morogoro-Iringa-Makambako-Njombe Wino- Songea
Ukipitia Lini... Dar Nangurukulu- Lindi-Mnazi mmoja (Mingoyo)-Mtama-Ndanda-Masasi-Tunduru-Namtumbo-Songea
Tofauti ya umbali kwenye ruti hizo mbili ni kama 50 to 80kM, huku uelekeo wa Lindi ndiyo mbali kuliko wa Iringa. Nauli zinafanana na ni Tshs 46,000/- kwa sasa.
Kwa wingi wa askari wa barabarani kwa sasa, Songea utafika kati ya Saa 3 na saa 6 Usiku bila kujali ruti. Kama hutajali mambo ya adventure, nashauri upitie Lindi. Ruti zote zina lami hadi Songea, ila uelekeo wa Lindi hauna kona kona na milima mingi ukilinganisha na uelekeo wa Iringa.
Kwa uelekeo wa Iringa, chakula mnapata Ruaha Mbuyuni wakati huku kwingine Masasi
Safari inaanzia Ubungo.... Hivyo kama unakaa uelekeo wa Kimara, unaweza ukapandia njiani ILA UNATAKIWA USEME KWAMBA UTAPANDIA NJIANI (TAJA ENEO) WAKATI UNAKATA TIKETI. Na vile vile kama unakaa uelekeo wa Mbagala, Rangi 3 ndo kituo kikubwa baada ya kuwa lishaondoka Sudani
Tiketi unaweza ukakatia kariakoo, Ubungo, Temeke Sudani au Mbagala rangi tatu. Unaweza ukabuku na kulipa siku moja kabla ya safari, saa 6 mchana MWISHO
Vile vile unaweza ukabuku kwa simu na kulipa kwa simu na ukatafuta namna ya kuipata tiketi yako. Ukihitaji namba njoo inbobo nikupe
Msafiri Mwenzio wa kunyumba
Ngali K