Msaada ndugu zangu dawa ya kunguni

RASHIDI OMARY

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
524
496
Miezi kadhaa iliyopita nilipata wageni toka kijijini walikaa kwangu kama mwezi hivi kumbe waliniachia balaa la kunguni.

Nimetumia dawa mbali mbali kupambana nao bado wananisumbua naomba msaada kwa anayejua dawa kali niwamalize maana ndani hakulaliki.
 
Tumia mafuta ya ndege kupakaa maeneo yote ila angalizo weka mbali na moto utanipa mrejessho.
 
Miezi kadhaa iliyopita nilipata wageni toka kijijini walikaa kwangu kama mwezi hivi kumbe waliniachia balaa la kunguni.

Nimetumia dawa mbali mbali kupambana nao bado wananisumbua naomba msaada kwa anayejua dawa kali niwamalize maana ndani hakulaliki.
Tumia dawa inaitwa NUVAN utakuja kunishukuru
 
Kuna dawa inaitwa lava na nyingine dudu changanya na maji kila chumba lita mbili za maji

mChanganyo hakikisha dawa ni kali,tafuta kopo la maji ya kunywa weka hyo dawa toboa vitobo viwili kwenye mfumiko nyunyiza kwenye vitanda na kwenye magodoro

Fanya hilo zoezi mara mbili kwa mwezi,hautawaona hao wadudu
 
Wana kashikashi si mchezo. Hizo jamaa zinahitaji intergrated approach. Iko ivi, tumia njia zote maana ni sahihi. Kwanza hakikisha unawawekea mkakati kama wa miezi sita. Na kila baada ya wiki unafanya hizi njia. Kila week hakikisha unatoa vitu nje, hasa vyenye mavamizi.

Kama wamevamia kwenye makochi ama masofa, we jipange tu kununua mengne mzee baba maana ni shida. Vyumbani sasa, toa vitu nje iwe ni nguo ama stuli na meza kama zipo. Godoro, nguo, out.....loweka kwenye maji ya moto.

Fungua kitanda, peleka mbao nje. Mwagia maji ya moto yaliyowekwa ariel na mafuta ya taa. Maji yawe ya moto hasa. Hizo nguo kwa mwezi toa mara moja. Lakini hii usafi fanya kila wiki kwa miezi sita. Inshort kumaliza kunguni ni ajira isiyo na mkataba wala allowance..na pia kwa wiki zingne tumia maji ya moto na hzo dawa ulizotajiwa na wakuu hata kama kwangu hazikufanya kazi. Pole aisee.
 
Nakupa hii ni uhakika!

Jaribu kutumia mafuta ya taa spray ndani kote Kila baada ya wiki moja! Hakikisha unaspray vzr wakiendelea kuwepo bas hama nyumba
 
Kuna dawa ya kuua mbu iliitwa ngao, ngao ya kidonge iliyoyeyushwa ilikuwa kiboko pia kwa kuua kunguni wate mpaka wale waliojificha. Hakuna kunguni aliyepita eneo lililopakwa dawa hiyo akasalimika
 
Kuna dawa ya kuua mbu iliitwa ngao, ngao ya kidonge iliyoyeyushwa ilikuwa kiboko pia kwa kuua kunguni wate mpaka wale waliojificha. Hakuna kunguni aliyepita eneo lililopakwa dawa hiyo akasalimika
Hivi ile sumu bado inapatikana kweli siku hizi, nakumbukuka ilipigwa marufuku lakini ilikua kiboko ya wadudu wote wa nyumbani.
 
Back
Top Bottom