Msaada ndugu zangu dawa ya kunguni

Msaada ndugu zangu dawa ya kunguni

Hivi ile sumu bado inapatikana kweli siku hizi, nakumbukuka ilipigwa marufuku lakini ilikua kiboko ya wadudu wote wa nyumbani.
Nawashukuru sana kwa ushauri wenu ule wa maana nitaufanyia kazi haraka kwa kweli kunguni ni wasumbufu sanaa
 
Hao wahuni hawaondokagi mpaka ukiwashe,lasivyo wakikuzoea Ndio imetoka.Na kukiwasha namaanisha uchome hayo matandiko kabla hawajakichafua.
 
Dah! Jiandae kupokea harufu mpya ndani ya nyumba yako, maana hizo dawa za kunguni sio poa.
 
Tafuta dawa ya wadudu inaitwa Akheri Powder utawakomesha. Lakini ujue hayo ni maroho ya mizimu ya kwenu yanakushambulia kwa kukiuka masharti ya ibada za kiukoo. Kumbuka kule misri yalitumika na Musa kama mapigo kwa Farao ili atii amri ya kuwaachia wana Waisraeli kutoka utumwani.
 
Wana kashikashi si mchezo. Hizo jamaa zinahitaji intergrated approach. Iko ivi, tumia njia zote maana ni sahihi. Kwanza hakikisha unawawekea mkakati kama wa miezi sita. Na kila baada ya wiki unafanya hizi njia. Kila week hakikisha unatoa vitu nje, hasa vyenye mavamizi.

Kama wamevamia kwenye makochi ama masofa, we jipange tu kununua mengne mzee baba maana ni shida. Vyumbani sasa, toa vitu nje iwe ni nguo ama stuli na meza kama zipo. Godoro, nguo, out.....loweka kwenye maji ya moto.

Fungua kitanda, peleka mbao nje. Mwagia maji ya moto yaliyowekwa ariel na mafuta ya taa. Maji yawe ya moto hasa. Hizo nguo kwa mwezi toa mara moja. Lakini hii usafi fanya kila wiki kwa miezi sita. Inshort kumaliza kunguni ni ajira isiyo na mkataba wala allowance..na pia kwa wiki zingne tumia maji ya moto na hzo dawa ulizotajiwa na wakuu hata kama kwangu hazikufanya kazi. Pole aisee.
wana nyanyasa..
 
Kuna dawa flani hivi unga unga wa rangi ya pinki unapakwa kwa kutumia unyoya wa kuku kwny kitanda na godoro aisee hutakuja kuona tena kunguni maisha yako yotee!
 
Kuna dawa flani hivi unga unga wa rangi ya pinki unapakwa kwa kutumia unyoya wa kuku kwny kitanda na godoro aisee hutakuja kuona tena kunguni maisha yako yotee!
Nikisumbuliwa na kunguni Kwa miaka miwili yaani Kila njia na dawa nilitumia lakini walikua waipoa Kisha wanakiwasha. Sasa nilipewa dawa ikiwa kwenye kichupa Kama vile vya dawa za sindano maarufu PPF. Ile dawa ilikua na rangi Kama mafuta ya kupikia na nililipa shilingi elf 15 na matumizi yake ni kupaka Kwa kutumia unyoya Kama hiyo dawa Yako. Nilipaka sehemu Kama sita kidogo kidogo na ilibaki nyingi tu. Tangu hiyo siku mpaka Leo ni miezi sita Sasa sijaona hata kifaranga Cha kunguni.

Sijui dawa inaitwaje maana aliniuzia ikiwa Haina maandishi yoyote.
 
Back
Top Bottom