Msaada: Naweza kupata magari binafsi yatakayoniwezesha kufika Mwanza ikiwa nitapanda saa tisa alasiri?

Nenda Wazo hill kiwandani kule au tafuta tanker mpaka saa tano asubuhi achana na hiyo saa tisa yako. Ukipata tanker kesho Mwanza mapema tu.
 
To Mwanza & Mbeya nenda ubungo maji mbele ya jengo la Tanesco Kuna gari zinakuja zinasimama na kupakia saa zingine Hadi kwa zamu hizi nyingi n xile zinasafirishwa kwenda nchi jirani Kama Zambia, Congo DRC, Rwanda & Burundi hata pale oilcom ubungo mchana gari zinaingia nakuuliza abiria.

Kwenda Moshi & Arusha ukikosa saibaba, harambee au Lim safari nenda ubungo oil com kuanzia jua linapotoka Hadi usiku saa tano gar la mwisho n la gazeti saa sita kasoro usiku

Ukiwa Arusha au Moshi kwenda dar & tanga ukikosa saibaba, Lim safari au harambee basi nenda himo njia panda Kuna gari ndogo zinakuja pale pia Kuna Costa za kupakia kwazamu Hadi saa nne pia Kuna basi la kutoka Nairobi Hilo linaitwa zoa zoa juz nimewapa 10k likanileta DSM na kurudi nategemea saibaba niwape 7k wanishushe Ars
jamani
 
Kwa imani natumaini kuwa wote tu wazima! Wakuu niko DSM na nimepata dharura ya kwenda Mwanza hivyo kulingana na dharura yenyewe sitaweza kupanda mabasi ya asubuhi ili angalau niweke mambo sawa kidogo kisha niondoke na zaidi ni kwamba natakiwa kuwa Mwanza kabla ya saa tatu asubuhi siku ya kesho.

Sasa nauliza naweza kupata magari binafsi yatakayoniwezesha kufika Mwanza ikiwa nitapanda magari hayo saa tisa au kumi alasiri? Na ni wapi naweza pata magari hayo kwa urahisi? Naombeni kusaidiwa wakuu kwa wale wenye uzoefu wa kusafiri na magari binafsi.
wahi maeneo ya mbezi mwisho panda IT hadi tinde, hapo utasubiria usafiri wa kufika mwanza chap
 
Kwa imani natumaini kuwa wote tu wazima! Wakuu niko DSM na nimepata dharura ya kwenda Mwanza hivyo kulingana na dharura yenyewe sitaweza kupanda mabasi ya asubuhi ili angalau niweke mambo sawa kidogo kisha niondoke na zaidi ni kwamba natakiwa kuwa Mwanza kabla ya saa tatu asubuhi siku ya kesho.

Sasa nauliza naweza kupata magari binafsi yatakayoniwezesha kufika Mwanza ikiwa nitapanda magari hayo saa tisa au kumi alasiri? Na ni wapi naweza pata magari hayo kwa urahisi? Naombeni kusaidiwa wakuu kwa wale wenye uzoefu wa kusafiri na magari binafsi.
Ushaanza safari?
 
Back
Top Bottom