Kwa imani natumaini kuwa wote tu wazima! Wakuu niko DSM na nimepata dharura ya kwenda Mwanza hivyo kulingana na dharura yenyewe sitaweza kupanda mabasi ya asubuhi ili angalau niweke mambo sawa kidogo kisha niondoke na zaidi ni kwamba natakiwa kuwa Mwanza kabla ya saa tatu asubuhi siku ya kesho.
Sasa nauliza naweza kupata magari binafsi yatakayoniwezesha kufika Mwanza ikiwa nitapanda magari hayo saa tisa au kumi alasiri? Na ni wapi naweza pata magari hayo kwa urahisi? Naombeni kusaidiwa wakuu kwa wale wenye uzoefu wa kusafiri na magari binafsi.