Msaada: Naweza hamisha mkopo toka Baypot kuja CRDB?

kilanio

JF-Expert Member
May 30, 2015
221
69
Habarini wakuu,

Mimi ni mtumishi wa umma, mnamo mwezi March mwaka huu nilichukua mkopo Bayport.

Kipindi hicho nilikua sijatimiza vigezo vya kwenda kopa bank na nilikua na uhitaji sana wa pesa hivyo nikakopa Baypot, na ilipofika mwezi Octoba mwaka huu nikafanya top up kama ya kukopa tena kama laki Tisa tu, ila kwa sasa nimeshatimiza vigezo vya kwenda kukopa CRDB, nataka nihamishie mkopo huko maana naimani nitakua secured nikiwa na mkataba na CRDB.

Hivyo naomba kujua je katika mazingira haya naweza enda hamishia mkopo wangu CRDB,? Kule Baypot nilikopa mil.7 na CRDB kwa rate ya mshahara wangu naweza kopa hadi mil 11.5, nataka nifanye top up Bayport sasa wamenikata huu mwezi wa pili sasa.

Naomba kwa mwenye uzoefu na hiki anijuze.

Natanguliza shukrani.
 
CRDB hawanunui madeni. Halafu kwann mnajichanganya kwenda kukopa kwenye hivi visaccos?
Bayport wanasumbua sana kwenye makato. Usipoangalia wanaweza kukukata mpaka unastaafu..

Hapo mpaka deni liishe au utafute hela ukalipe den slip salary iwe plain ndio utaweza kukopa
 
Hakuna kitu ninachokiogopa kama mikopo ya benk na saccos,riba kubwa mno,niliwahi kukopa makato yaliniumiza sana,kwa kijana anaenza kazi plz kuna njia nyingi zakufikia malengo yako,hii shortcut inaumiza sana
 
Hivi crdb kwa wafanyakazi wa kampuni binafsi wanatoa mkopo na vigezo vyao vipoje mimi nimeajiriwa na kampuni ya wahindi mshahara wangu unapitia crdb kwa muda wa miaka sasa vp naweza kuomba mkopo hapo bank?samahani kwa kuingilia uzi mkuu
 
Bayport ni hatari kweli. Kuna mdada alikopa 4 mil baada ya kushtuka alienda postal bank akaresha ule wa bayport hata hivyo waliendelea kumkata mpaka 3 month
 
Bayport, blue finance, tunakopesha ltd,finca,kwetu finance,efc,sijui nini usije kukopa hata kama una shida kubwa kiasi gani.
 
Hakuna kitu ninachokiogopa kama mikopo ya benk na saccos,riba kubwa mno,niliwahi kukopa makato yaliniumiza sana,kwa kijana anaenza kazi plz kuna njia nyingi zakufikia malengo yako,hii shortcut inaumiza sana

Mkuu samahani unaweza kutuambia baadhi ya hizo njia ni zipi kwa walioingia ajira mpya mbali na kukopa. Bank....
 
Ulikuwa na haraka sana MWAKA mmoja wa probation uliona 90 siyo ngoja waendelee kukukomba kama VP uza kiwanja ulipe mkopo Bayport ukakope CRDB
 
I don't recommend any one anaeanza maisha kuchkua mikopo..labda Kama unabiashara inayojiendesha
 
Hizi taasis kama bayport platinum ni majibu haya,,,,ila yanamilikiwa na kina mkapa warioba riba zao ni kubwa sana!!
 
Kaka kuna ugumu sana hapo,kuna njia 2.
1.ni kutafuta hela ulipe huo mkopo wa bayport ili ukope pengine na sehemu nzuri nenda kwenye chama cha wafanyakazi wa serikali kama ni za mitaa au kuu huko riba ni 12% na kwa mshahara wako ulio kopea bayport unaweza kukopa zaidi ya 7M Kwa miaka 3 tu.
2.siku hzi Crdb hawanunui madeni unachoweza kufanya ni kuwasiliana na uongozi wa backlays makao makuu na kuwaomba kuwa unataka uchukue mkopo mkubwa ili ulipe deni lao hivyo wao watawasiliana na afisa utumishi wako kumuamba asitishe makato yako kwenye mfumo.badaye utakwenda Crdb na vielelezo hivyo ku process huo mkopo.
 
baclays hapo sijakupata mkuu
 
Back
Top Bottom