Msaada: Nataka kuwashitaki Voda kwa kuwaficha matapeli

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,213
2,000
Siku tatu zilizopita niliwasiliana na agent wa basi fulani ili anikatie tiketi niweze kusafiri. Nilimwambia kwamba nitamtumia nauli kupitia M-pesa. Baada ya muda mfupi ikaingia zile msgs za kitapeli "nitumie zile pesa kwa namba hii". Baada ya kuwa nimeweka pesa ya nauli kwenye simu, sikujiuliza mara mbili nikatuma nauli kwa tapeli.

Nilipompigia yule agent kumuuliza kama amepokea muamala akakana, ndipo nilipogundua kuwa nimeibiwa. Nikawapigia kampuni husika, kama mjuavyo jinsi ambavyo inachukua muda mrefu kuwapata watu wa customer care, nilipowapata na kuwaarifu pesa ikawa imeshachukuliwa! Nilipojaribu kucheki ile namba iliyotumiwa na tapeli nikagundua kuwa haijasajiliwa!

Kwa kuwa sheria inayataka makampuni ya simu kuwasajili wateja wake ili kupambana na wizi wa mitandaoni; na Vodacom hawakuwa wamemsajili mwizi wangu (kama wangekuwa wamemsajili ningemripoti polisi na angefuatiliwa), nafikiria kuwashitaki Vodacom kwa kumsaidia tapeli kuniibia.

Wanasheria naomba msaada wenu; kisheria imekaaaje hili suala maana kwa makusudi kabisa wameshindwa kutimiza wajibu wao na kwa maana hiyo wanaendekeza vitendo vya wizi dhidi ya wateja wao.

Vv
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,191
2,000
Hizo namba ambazo hazijasajiliwa ni za wafanyakazi wa hayo makampuni huwezi kuwapata. Namba zote ambazo hazijasajiliwa zilifungiwa ila hao voda ndo wezi wenyewe.
Yeahh, hii inaweza kua kweli mkuu

Maana namba zote kwa sasa zinazotumika zmesajiliwa

kweli Mkuu

Wezi nihao hao Voda

Jamaa angewadili haohao.
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
14,368
2,000
Hizo namba ambazo hazijasajiliwa ni za wafanyakazi wa hayo makampuni huwezi kuwapata. Namba zote ambazo hazijasajiliwa zilifungiwa ila hao voda ndo wezi wenyewe.
Uko sahihi, waliona msg za kutimiana hela ndiyo maana wakaona fursa, juzi kuna mtu nilitakiwa nimtumie hela nikachat naye kwa njia ya msg,baada ya dk 3 hivi msg ikaja tuma kwa namba hii, nusura niingie mkenge, ikabidi nimpigie tena dogo kuuliza kama ananamba nyingine siijui akakataa, nikagundua wezi ni wafanyakazi wa makampuni
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,803
2,000
Huu mtandao ni wa kinyonyaji zaidi hata ya hao matapeli wanaowalinda. Masikini kutoa pesa 10,000 garama zaidi ya 14% 1450tzs... bado huduma za za kitapeli songesha.... ada ya maombi....riba ....kwa siku....
 

Kiraka

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
2,857
2,000
Uko sawa kabisa. Ukiangalia hapo ni kuwa kuna mtu aliona mawasiliano yako ndio maana akaingilia kati. Uwezekano mkubwa ni watu wa ndani wa vodacom.
Hii pia iko Airtel, utashangaa ukipokea muamala mkubwa kwenye simu yako zinaanza kuja hizi message na zile za kupigiwa na wanaojidai wafanyakazi wa huo mtandao.
Haya makamouni yana wafanya kazi wezi au yana fanya kazi na kampuni zenye wafanyakazi wasioaminika.

Baada ya kufuatilia, nimepata maelekezo yanayoleta maana kidogo.
Tuwe makini na mawakala tunaowatumia kufanya trasaction zetu za simu, inaonekana hawa ndio hutoa taarifa kwa wezi mara wakisha kuhamishia muamala.
 

Nzuguni one

JF-Expert Member
Dec 23, 2019
1,037
1,500
Siku tatu zilizopita niliwasiliana na agent wa basi fulani ili anikatie tiketi niweze kusafiri. Nilimwambia kwamba nitamtumia nauli kupitia M-pesa. Baada ya muda mfupi ikaingia zile msgs za kitapeli "nitumie zile pesa kwa namba hii". Baada ya kuwa nimeweka pesa ya nauli kwenye simu, sikujiuliza mara mbili nikatuma nauli kwa tapeli...
Shitaki kampuni maana inafuga wezi
 

Nzuguni one

JF-Expert Member
Dec 23, 2019
1,037
1,500
Uko sawa kabisa. Ukiangalia hapo ni kuwa kuna mtu aliona mawasiliano yako ndio maana akaingilia kati. Uwezekano mkubwa ni watu wa ndani wa vodacom.
Hii pia iko Airtel, utashangaa ukipokea muamala mkubwa kwenye simu yako zinaanza kuja hizi message na zile za kupigiwa na wanaojidai wafanyakazi wa huo mtandao.
Haya makamouni yana wafanya kazi wezi au yana fanya kazi na kampuni zenye wafanyakazi wasioaminika.
Kabisa
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
9,369
2,000
Ukiweza kupata wakili utashinda kesi bila shida ila usichukue mawakili njaa kama yule aliyekuja kwa mbwembwe akitishia kushitaki makampuni ya simu mwisho akapotea.

Sheria zipo ila wanaotakiwa kusimamia sheria ni wazembe au wala rushwa ukishafungua kesi voda watakufata na kuomba mmalizane nje ya mahakama kwani utakuwa umewafumbua macho watu wengi
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,191
2,000
Kama namba zote zimesajiliwa mbona kuna gharama tofauti kwa namba iliyosajiliwa na isiyosajiliwa
Kumbe kuna namba zinazotumika na hazijasaliwa bado?

Mbon mimi walivyonifungia za awali, nikasajili HaloT, nilikaa nayo miezi miwili ,pia ikafungiwa

Mpaka niliposajili Ninazo tumia sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom