Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,745
- 5,446
Siku tatu zilizopita niliwasiliana na agent wa basi fulani ili anikatie tiketi niweze kusafiri. Nilimwambia kwamba nitamtumia nauli kupitia M-pesa. Baada ya muda mfupi ikaingia zile msgs za kitapeli "nitumie zile pesa kwa namba hii". Baada ya kuwa nimeweka pesa ya nauli kwenye simu, sikujiuliza mara mbili nikatuma nauli kwa tapeli.
Nilipompigia yule agent kumuuliza kama amepokea muamala akakana, ndipo nilipogundua kuwa nimeibiwa. Nikawapigia kampuni husika, kama mjuavyo jinsi ambavyo inachukua muda mrefu kuwapata watu wa customer care, nilipowapata na kuwaarifu pesa ikawa imeshachukuliwa! Nilipojaribu kucheki ile namba iliyotumiwa na tapeli nikagundua kuwa haijasajiliwa!
Kwa kuwa sheria inayataka makampuni ya simu kuwasajili wateja wake ili kupambana na wizi wa mitandaoni; na Vodacom hawakuwa wamemsajili mwizi wangu (kama wangekuwa wamemsajili ningemripoti polisi na angefuatiliwa), nafikiria kuwashitaki Vodacom kwa kumsaidia tapeli kuniibia.
Wanasheria naomba msaada wenu; kisheria imekaaaje hili suala maana kwa makusudi kabisa wameshindwa kutimiza wajibu wao na kwa maana hiyo wanaendekeza vitendo vya wizi dhidi ya wateja wao.
Vv