Msaada: Nataka kuwashitaki Voda kwa kuwaficha matapeli

Kumbe kuna namba zinazotumika na hazijasaliwa bado ?

Mbon mimi walivyonifungia za awali, nikasajili HaloT, nilikaa nayo miezi miwili ,pia ikafungiwa

Mpaka niliposajili Ninazo tumia sasa.
Nenda kwenye wakala wa mpesa utaona wameandika kabisa gharama za kutolea pesa kwa laini ambazo hazijasajiliwa
 
Watanzania wengi ni wajuaji sana lakini hamna kitu kichwani.

Namba ya wakala wa Bus unayo na umewasiliana naye

Namba nyingine imekutumia sms ya kuomba utume pesa then wewe na uboya wako ukatuma pesa bila kuangalia namba ya awali na hiyo nyingine kama ni namba moja.

Kwa akili yako nzuri hukutaka hata kumwuliza huyo wakala wa Bus kama namba ya pili ni ya kwake kabla hujamtumia pesa au la.

Hiyo akili ya kuishitaki kampuni ya Voda unaipata wapi wakati hukuwa nayo kabla hujatuma pesa kwa tapeli???

Kumbuka:- Ujinga wako ni faida kwa mwenzako
 
Watanzania wengi ni wajuaji sana lakini hamna kitu kichwani.

Namba ya wakala wa Bus unayo na umewasiliana naye....
Mwenzio ni boya kwa kutuma fedha kizembe wakati wewe ni boya kwa kusahihisha kiboya na bila kutumia lugha ya staha...hapo ngoma froo!!
 
Watanzania wengi ni wajuaji sana lakini hamna kitu kichwani.

Namba ya wakala wa Bus unayo na umewasiliana naye....
Na mimi nakubaliana na wewe ila bado haihalalishi yaliyotokea. Na pia mtu ukiwa kwenye harakati za maisha zilizojaa msongo wa mawazo ni rahisi sana kufanya kosa alilofanya jamaa. Haya malalamiko ya kutumiwa msg na matapeli mara unapotumiwa fedha au unapokuwa umewasiliana na mtu akutumie fedha yamezidi sana. Serikali inatakiwa kuchukuwa hatua.
 
Wewe umeibiwa kizembe sana, akili hizi za kutaka kufungua kesi zilitakiwa zikupe Alert kwamba unatapeliwa siku nyingine jitahidi ku play smart.
 
Ukiweza kupata wakili utashinda kesi bila shida ila usichukue mawakili njaa kama yule aliyekuja kwa mbwembwe akitishia kushitaki makampuni ya simu mwisho akapotea.

Sheria zipo ila wanaotakiwa kusimamia sheria ni wazembe au wala rushwa ukishafungua kesi voda watakufata na kuomba mmalizane nje ya mahakama kwani utakuwa umewafumbua macho watu wengi
hawezi shinda ina maana alikuwa hamjui jina huyo agent? sababu ukituma pesa lazima litoke jina la unayemtumia na uhakiki kwanza kabla ya kuruhusu pesa kuondoka kwenda .Mleta mada kama kaibiwa ni kizembe.Swali jina la aliyemtumia ndilo jina hilo hilo la agent? kama siyo ubavu wa kutuma aliutoa wapi
 
Hizo namba ambazo hazijasajiliwa ni za wafanyakazi wa hayo makampuni huwezi kuwapata. Namba zote ambazo hazijasajiliwa zilifungiwa ila hao voda ndo wezi wenyewe.
Nadhani natakiwa niwachukulie hatua, haya makampuni ya simu, badala ya kutukinga na kuibiwa wao wanatu-expose wateja wao kwa matapeli.

Vv
 
Wakati unatuma hela halikutokea jina la mpokeaji?

Ni uzembe uliopitiliza kutuma hela kipindi hiki bila kuona jina la mpokeaji...

Ni uzembe sana.

Pole sana mlipa kodi mwenzangu
Mkuu, msg ilisema hivi, 'hiyo hela usinitumie kwa ile namba, tuma kwa namba hii (ikawekwa namba na jina la mookeaji)'. Kwa kuwa muda huo ndio nilikuwa nimemaliza kuongea na ajenti, nilijua ni atakuwa ni yeye. Haijawahi kutokea nikatapeliwa na hizo msg, ni coincidence na haraka niliyokuwa nayo kufaniksha safari yangu.

Vv
 
Siku tatu zilizopita niliwasiliana na agent wa basi fulani ili anikatie tiketi niweze kusafiri. Nilimwambia kwamba nitamtumia nauli kupitia M-pesa. Baada ya muda mfupi ikaingia zile msgs za kitapeli "nitumie zile pesa kwa namba hii". Baada ya kuwa nimeweka pesa ya nauli kwenye simu, sikujiuliza mara mbili nikatuma nauli kwa tapeli.

Nilipompigia yule agent kumuuliza kama amepokea muamala akakana, ndipo nilipogundua kuwa nimeibiwa. Nikawapigia kampuni husika, kama mjuavyo jinsi ambavyo inachukua muda mrefu kuwapata watu wa customer care, nilipowapata na kuwaarifu pesa ikawa imeshachukuliwa! Nilipojaribu kucheki ile namba iliyotumiwa na tapeli nikagundua kuwa haijasajiliwa!

Kwa kuwa sheria inayataka makampuni ya simu kuwasajili wateja wake ili kupambana na wizi wa mitandaoni; na Vodacom hawakuwa wamemsajili mwizi wangu (kama wangekuwa wamemsajili ningemripoti polisi na angefuatiliwa), nafikiria kuwashitaki Vodacom kwa kumsaidia tapeli kuniibia.

Wanasheria naomba msaada wenu; kisheria imekaaaje hili suala maana kwa makusudi kabisa wameshindwa kutimiza wajibu wao na kwa maana hiyo wanaendekeza vitendo vya wizi dhidi ya wateja wao.

Vv
Kampuni za simu zina wakubwa ndani yake huwezi kufanikiwa
 
Watanzania wengi ni wajuaji sana lakini hamna kitu kichwani.

Namba ya wakala wa Bus unayo na umewasiliana naye

Namba nyingine imekutumia sms ya kuomba utume pesa then wewe na uboya wako ukatuma pesa bila kuangalia namba ya awali na hiyo nyingine kama ni namba moja.

Kwa akili yako nzuri hukutaka hata kumwuliza huyo wakala wa Bus kama namba ya pili ni ya kwake kabla hujamtumia pesa au la.

Hiyo akili ya kuishitaki kampuni ya Voda unaipata wapi wakati hukuwa nayo kabla hujatuma pesa kwa tapeli???

Kumbuka:- Ujinga wako ni faida kwa mwenzako
Asante mkuu kwa kuniona mimi bwege, na huo ubwege wangu nataka niwaondolee unyonge Watanzania wengine na kukomesha hayo makampuni yanayoshirikiana na matapeli kutuibia.

Vv
 
Kwa kuwa muda huo ndio nilikuwa nimemaliza kuongea na ajenti, nilijua ni atakuwa ni yeye.
jina la huyo agent wako na huyo uiyemtumia yanalingana? kama hayalingani kwa nini hukuuliza huyo agent wako kuwa mbona jina tofauti? Akupe jibu kwanza kabla kutuma? Kwa nini hilukumuuliza? kiherehere cha kutuma chap chap ulikitoa wapi?
 
hawezi shinda ina maana alikuwa hamjui jina huyo agent? sababu ukituma pesa lazima litoke jina la unayemtumia na uhakiki kwanza kabla ya kuruhusu pesa kuondoka kwenda .Mleta mada kama kaibiwa ni kizembe.Swali jina la aliyemtumia ndilo jina hilo hilo la agent? kama siyo ubavu wa kutuma aliutoa wapi
Hilo jina halikuwa la agent, ni la mtu binafsi; niliwasiliana na kampuni husika, wakaniambia hiyo namba siyo ya agent. Namba ya agent huwa ni tofauti na namba za wateja, agent namba hazifiki 9, huwa I tarakimu 4 hadi 6, hazianzi na 07.....

Na wewe mbona mabasi kibao unakata online kwa nini utumie pesa mtu?
 
Hilo jina halikuwa la agent, ni la mtu binafsi; niliwasiliana na kampuni husika, wakaniambia hiyo namba siyo ya agent. Namba ya agent huwa ni tofauti na namba za wateja, agent namba hazifiki 9, huwa I tarakimu 4 hadi 6, hazianzi na 07.....

Vv
Kabla ya kutuma jina linatokea wewe ulitumaje no ambayo hajasajiliwa? hii story yako ni ya kupika mkuu
 
Back
Top Bottom