Msaada: Nataka kuishitaki nyumba ya ibada iliyo jirani na nyumba yangu

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,119
Sina tafsiri sahihi ya hili neno "uhuru wa kuabudu" ila naona kama watu wanaitafsiri tofauti wanapitiliza.

K7na nyumba ya ibada hapa jirani huwa wanaamsha watu kwa ajili ya kuswali lakini maneno anayotumia ni ya kuogopesha mpaka kuleta tahruki katika familia yangu.

Naweza kumnukuu "Amkeni mkaswali hizo nyumba zenu hapa naona kama ni makaburi na hicho kitanda ulicholalia ni kama jeneza hilo shuka ulilojifunika ndo sanda amkaaaaa amkaaa".

Haya maneno yakikuamsha usingizini huwezi kulala tena, hii inapelekea familia nzima kushindwa kulala.

Nafikiria kupata msaada wa kisheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli inafikirisha.... Ila mimi sidhani imani inatengenezwa na vitisho hivyo, bali hutoka ndani ya mtu. Ukishitaki ukafanikiwa utakuwa umesaidia wengi... hayo maneno si mema kabisa. Watumie ,mbadala ya kuleta matumaini na sio hofu.

Pole sana, nawazza tu hao watoto wako
 
Duuh!. Huwezi kuishtaki nyumba ya Ibada, kwa sababu nyumba haina mdomo wa kunena hayo.

Badala yake, fatilia mzungumzaji wa maneno hayo. Kisha peleka mahakamani.

Anakutia hofu na kukukosesha Uhuru wa kufanya mambo yako.

Pole sana.
 
Kweli wewe ni ILLEGAL MIGRANT ndo maana huwa hamna ADABU,

Nyumba ya IBADA huwa ni tofauti na nyumba za MAIGIZO YA IBADA.

Halafu unachukia kuamshwa,USINGIZI wa alfajiri hauna FAIDA yoyote ni Uzembe tu,

Na pia unachukia kukumbushwa KIFO, utake usitake WOTE TUTAKUFA TU,

Hela na Nguvu ya kufungulia KESI ziweke kwenye IBADA NA SADAKA na sio kwenye UPUMBAVU.

karibu sana jitahidi pia utii na mamlaka zilizokuwa juu yako ili uwe LEGAL MIGRANT.
 
Sina tafsiri sahihi ya hili neno "uhuru wa kuabudu" ila naona kama watu wanaitafsiri tofauti wanapitiliza kuna nyumba ya ibada hapa jirani huwa wanaamsha watu kwa ajili ya kuswali lakini maneno anayotumia ni ya kuogopesha mpaka kuleta tahruki katika familia yangu naweza kumnukuu "amkeni mkaswali hizo nyumba zenu hapa naona kama ni makaburi na hicho kitanda ulicholalia ni kama jeneza hilo shuka ulilojifunika ndo sanda amkaaaaa amkaaa" haya maneno yakikuamsha usingizini huwezi kulala tena hii inapelekea familia nzima kushindwa kulala nafikiria kupata msaada wa kisheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo inatakiwa ufanye kazi ya ziada ya tupicha picha na tu video usikurupuke Nenda kwa mjumbe hadi Mwenyekiti wa Mtaa
 
Back
Top Bottom