Msaada: Nataka kuingia Jijini Nairobi kutokea Tanzania

ngutu

Senior Member
Jul 21, 2016
101
67
Habari wakuu.

Poleni na hongereni kwa majukumu, sijawahi kutoka nje ya Tanzania ndio nataka nianze sasa kwa kuanza na Jiji la Nairobi, Sina ndugu, rafiki wala mtu ninayefahamiana nae Nairobi, ila nimekuwa na msukumo wa ndani ukinitaka nifike Nairobi ,Sina passport ya kusafia, nahitaji kujua taratibu na kama kuna wadau hapa nipate wenyeji wangu.

Asante.
 
NGUTU KUTOKA MUSOMA VIJIJINI AU?ELEZA UNATOKEA WAPI NA UTAINGILIA BORDER IPI.
ILA KWA UZOEFU PALE BORDER KUNA KIASI CHA PESA UNATOA UNAPEWA KIBALI MAALUMU CHA KUINGIA KENYA,NO PASSPORT HAPO.
 
Nenda ofisi za uhamiaji ukapewe pass ya mwaka, gharama haizidi 50k.
Jumla.
Hakuna mlolongo kikubwa uwe na namba ya nida.

Katika hizo gharama ni pamoja na affidavit ya mzazi wako mmoja
Shukrani ,nitafanya hivyo...nifafanulie kwenye halfdavit ya mzazi
 
Shukrani ,nitafanya hivyo...nifafanulie kwenye halfdavit ya mzazi
Affidavit ni kiapo.
Ikiwa una cheti cha kuzaliwa cha mzazi wako huhitaji kufanya affidavit, kama huna cheti ndio utaapishwa kwa mwanasheria na utafanyia huko huko uhamiaji mara nyingi wapo jirani tu na ofisi za uhamiaji.
 
Asante nashukuru
 
Chukua passport ya muda panda basi Sirari usiku utafika Nairobi asubuhi zunguka mpaka jioni, usiku panda basi la kurudi Sirari ila ndio hapo sasa kama hauna mwenyeji utazunguka zunguka wapi labda ongea na konda akutafutie boda wa kukuzungusha siku nzima.... usisaha kupita Garrisa kwa wasomali kula mapochopocho (jamaa kwenye mapishi wapo vema) Lakini hio naongelea miaka hio huenda hata sehemu haipo tena....
 
Nimetabasamu...
 
Ngutu unaenda kwa ishu gani sorry lakini natamani kujua kama ni kutalii tu ama una lingine
 
Back
Top Bottom