Msaada juu ya manunuzi ya gari ndogo ya kutembelea

sakwano

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
304
827
Wakuu, hongereni na poleni na majukumu ya kimaisha.

Mimi katika harakati zangu za kimaisha sijawahi kumiliki gari hata siku moja, ila nimejichanga nina kiwango cha kiasi kama milioni 11 ya uhakika ambayo ninayo hapa.

Nilikuwa nahitaji gari ndogo ya kuanzia maisha sana sana nilitamani ist sababu kuna rafiki yangu anayo na nzuri sana ila simuamini.

Je, hatua ya kwanza ni ipi, ni wapi pazuri nitanunua nahitaji mpya.

Kuhusu kuendesha sina tatizo kabisa naweza kununua mahali popote nikafika nayo mkoani.

Nawatakia sikukuu njema nataraji muongozo sahihi kabla ya kufanya maamuzi.
 
Mkuu kwanza IST sio nzuri. Tusidanganyane sema tu kipato kinaishia hapo.

Pili, nenda na Toyota haujakosea. Kutokana na hili tatizo la wese nashauri usiende juu ya cc1500.

Kwahiyo bei unaweza kutana na madalali wakasema wakuletee Mark X, Crown, Brevis, Mark II ila wakatalie.

Nenda na IST, Runx, Allex, and alike.

Tukutane Puma au Total Tsh 3200/=
 
Mkuu kwann ist sio nzuri mbona ziko nyingi na wengi wanasema hazir mafuta pia nataka niwe nafanya hata tax bubu sometimes
Sio nzuri kwa muonekano ila inafaa sana kwa matumizi uliyosema na budget.

Hapo kwenye Taxi bubu naomba ujifikirie mara mbili.

Najua unamaanisha ile unarudi home unapitia kituoni hafu unapakia abiria wanne buku 2 kila mmoja unapata buku 8 si ndio?

Mkuu unachakaza gari knm.

Bora upambane utafute gari ya Mil 10 halafu hiyo Mil 1 ununue bodaboda iwe inakupa buku 10 kila siku ya kuhudumia gari siku ukiwa haupo vizuri.
 
Sio nzuri kwa muonekano ila inafaa sana kwa matumizi uliyosema na budget.

Hapo kwenye Taxi bubu naomba ujifikirie mara mbili.

Najua unamaanisha ile unarudi home unapitia kituoni hafu unapakia abiria wanne buku 2 kila mmoja unaoata buku 8 si nsio?

Mkuu unachakaza gari knm.

Bora upambane utafute gari ya Mil 10 hafu hiyo Mil 1 ununue bodaboda iwe inakupa buku 10 kila siku ya kuhudumia gari siku ukiwa haupo vizuri.
Asante mkuu ndio lilikuwa wazo langu nimekupata vyema
 
Wakuu, hongereni na poleni na majukum ya kimaisha.

Mimi katika harakti zangu za kimaisha sijawahi kumiliki gari hata siku moja,ila nimejichanga ninakiwango cha kiasi kama milioni 11 ya uhakika amabyo ninayo hapa.

Nilikuwa nahitaji gari ndogo ya kuanzia maisha snasana nilitamani ist..sababu kuna rafiki yangu anayo na nzuri sana..ila simuamini.

Je, hatua ya kwanza ni ipi,ni wapi pazuri nitanunua nahitaji mpya

kuhusu kuendesha sina tatizo kabisa naweza kununua mahari popote nikafikanayo mkoani.

Nawatakia sikukuu njema nataraji muongozo sahihi kabla ya kufanya maamuzi
Karibu sana mkuu nikuhudumie kwa gari used mpaka mpya budget kuanzia 5m mpaka 400m karibu sana kwa ushauri na uchaguzi.

0623953036 whatsapp/calls pia unaweza tembelea thread yangu ya@magari used tanzania
 
IMG-20220625-WA0008.jpg
 
Binafsi huwa napenda gari za juu juu, hizi za chini naona kama sipo kwenye gari; nunua kile kitu moyo wako unataka, iwe mpya, used n.k kuhusu matumizi ya mafuta, itategemea na chaguo lako; ila chakula cha gari ni mafuta.
 
Back
Top Bottom