Msaada: Nataka kuezeka nyumba hii

Karibu naleta mrejesho...
 
Habari Zenu Wadau,
Nimesoma post na ushauri wa watu ni mzuri sana. Mimi pia nipo katika mchakato wa kuezeka, naoma ushauri wapi naweza kupata mbao kwa bei nzuri ili niweze kukamilisha kuweka roof. Na vipi kuhusu mbao treated naona watu wengi hawazikubali kabisa. Mbao za minazi zinapatikana wapi?

Nawakilisha
 

Kwa huko jeshini bata za migongo midogo 120 uliuziwa kwa Tzs ngapi?
 
Mkuu naomba unieleze kwa kina jinsi ya kuchana mbao za mnazi hatua kwa hatua.bado sijakupata
 
ni mtaalamu wa ujenzi nitakucholea paa zuri la nyumba yako na nitakuonyesha hadi 3D yake pamoja na finishing yake kwa 150,000/= nitafute kama upo tayari 0712006246
 
hiyo mbao ya mnazi sasa, kuipata ni ishu, huo mnazi una umri gani!?
 
Hongera mkuu ni hatua.
Ushauri wangu hii nyumba jinsi inavyoonekana mpauo wake hautakua complicated utakua wa kawaida kabisa maana haina kona nyingi upauaji unategemea pia ramani ya nyumba chini ikoje idadi ya kona kuta zilivyochomoka. Kwa muonekano huo nyumba hii inakona nne za kawaida na baraza moja nayo haijavutwa njee sana so it is simple, nafuu pia hakuna kukatakata bati sana.
Nenda jeshini au pale tazara nunua bati za kawaida za rangi sh.elfu 22 kwa bati moja nyumba hyo itachukua bati 105 au pungufu kidogo. Maana bati zile n ndogo kidogo kwa bati hiz za kawaida.
Mbao kama walivyoshauri wadau nenda buguruni na tape measure yako kanunue zile za kupima zenye urefu wa kutosheleza kuepuka kuunga unga mbao.
Upande wa hela hyo hela haitatosha lkn usikate tamaa nunua bati weka ndani jikusanye kanunue mbao za kupaua na blandering(draft ya gypsum boad/silling boad) umalize kazi ya mbao inatesa sana katika ujenzi kuliko kitu kingine chochote kwa upande wangu.
Mkuu kila laheri. Hongera kila kitu kidogokidogo ukimtanguliza Mungu unaweza.
 
Asante sana mkuu King Kong III kwa hakika nimejifunza kitu cha maana sana kuhusu mbao ya mnazi, sikujua kuwa inafaa kwa namna hiyo! Zanzibar Spices mchango wako ni madini.

Mmh jamani mbao za mnazi ni nzuri kweli kama mdau alivyosema.
Hofu yangu iko utakapopata minazi maana ili mnazi ufae kutengeneza kitu lazima upate mnaz uliokomaa vzr sasa jmn dar unaupata wapi? Hyo ya idadi hiyo? Labda uende pwani ukatafute uchane usafirishe mwisho wa siku gharama inakuwa ile ile.
Kama ipo na iliyokomaa vizuri tumia, otherwise sikushauri kabisa usije ukakata tamaa au utachukia nyumba yako.
Na upate fundi mzuri mbao ya mnazi uliokomaa vzr ni ngumu mno kupigilia msumari ni shughuli ukipata fundi mvivu nayo itasumbua.
 
Last edited by a moderator:
jiongeze swahiba upige migongo mipana msouth nyumba itapendeza sana hiyo kwa jinsi ilivyo. Nunua mbao piga hesabu ya bati anza kulipa kidogo kidogo kwa agent wa bati za msouth ikitimia unapaua nyumba haitaki haraka utakuja juichukia baadae bure nimeipenda nyumba yako ikipata msouth pale kati ukaipa PVC windows na kuimalizia vizuri utajikuta baadae unahamu ya kurudi home mapema automatically
 

mkuu njaa unaweza kutusaidia bei ya bati migongo midogo ni shilingi ngapi?
 
Uptodate bei ya mabati ya rangi migongo midogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…