Msaada: Nataka kuezeka nyumba hii


Tathimini hiyo naipiga fresh na roof plan unaipata cheki nikichukua vipimo site alafu njoo PM tulonge
 

Attachments

  • 1411298055627.jpg
    95.8 KB · Views: 420
  • 1411298078488.jpg
    121.8 KB · Views: 540
Asante mleta mada, nimejifunza kitu hapa, hasa kuhusu treated timber na mti wa mnazi, hata mimi niko hatua kama yako na nimesimamia hapo nikizichanga, shukrani za pekee zimfikie wa 'mti wa mnazi' jf ni kila kitu.
 

King Kong III, Umenipa elimu kubwa sana, sikuwahi kufukiria mbao ya mnazi, je unaweza walau kunisaidia walau wapi miti ya minazi inapatikana kwa urahisi?

Ubarikiwe.
 
Last edited by a moderator:
King Kong III, Umenipa elimu kubwa sana, sikuwahi kufukiria mbao ya mnazi, je unaweza walau kunisaidia walau wapi miti ya minazi inapatikana kwa urahisi?

Ubarikiwe.

Miti ya Minazi kwa Wingi inapatikana Bagamoyo,Mkuranga,Pugu kwahiyo utaangalia Site yako ipo wapi zaidi kama ipo wilaya ya temeke unaweza ukachukua kutoka mkuranga/kongowe/mwandege/vikindu,kama upo wilaya ya kinoclan unaweza ukachukua maeneo ya mapinga/bunju mabwepande/zinga/kerege au kama ipo ilala unaweza ukachukua maeneo ya ukonga/kipunguni/gombs/pugu watu wa kukata mbao za minazi wapo wengi tu wenye mashine zao wanapasua mnazi mmoja kwa sh 4000 halafu mbao za mnazi hazihitaji dawa maana haziliwi na mchwa au na mdudu yeyote kuna project kama 5 hivi nimeziona zimepigwa kitu cha mnazi nikipata wasaa nitapiga snaps ni-attach uone.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu natamani nizinunue tu hizo mbao nikae nazo, hata kama sijengi sasa hivi. Unajua kwa mwendo huu zitakua hazishikiki muda sio mrefu. Ubarikiwe sana kwa kunifumbua macho kuhusu mbao za Mnazi na kwa upande mwingine huenda ikawa fursa ya biashara mkuu.
 
Aisee,Kama kazi ya Meya wa Jiji,basi mkuu Kingkong ningekupa.
Maana unajua chochoro zote hizo.
 

Asante sana upembuzi yakinifu King Kong. Uongezewe baraka, hapo tunaona faida ya jf, bila shaka wengi watanufaika na presentation yako.
 

Lakini mnazi u atakiwa upauliwe ukiwa mbichi kama sikosei wanasema ukikauka msumari haungii. Ni wazo zuri sana hongera kwa mchango wako.
 

Mjomba ubarikiwe sana
 
ndo maana ukawepo mkuu, hongera! kwa bahati mbaya hata kiwanja sina ningekutafuta ndugu
 
Kama una mtu jeshini unapata hizo bati kwa nusu bei ya mtaani,hapo nadhani ukiongeza milioni 2 utapiga bati na kulipa mafundi,lakini kwa hiyo 4 bado haitoshi,usisahau pia kuna kuongeza matofali kabla hujapaua .
 
Wazo lako ni zuri sana, ila nadhani ingependeza zaidi kama ungemuunganisha na huyo fundi mwenye gharama nafuu....

Fundi wangu alitaka tsh laki saba hela ya ufundi (kupaua). Ila ni wa Morogoro
 
Fundi wangu alitaka tsh laki saba hela ya ufundi (kupaua). Ila ni wa Morogoro

huyo wa Morogoro wanini ilihali mafundi tumejaa humu JF?. na kunafundi mwenzangu humu anaitwa mavuno nyamanoro alisha wezekea wana JF.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni nini tofauti ya hawa mafundi wanaochaji m2.5 mpaka 3 na hawa wa Laki Saba? Au wanaangalia na sura? Anaeweza kunijibu kitaalamu nitafurahi maana utofauti ni mkubwa sana.
 
Nadhani mtoa hoja atakua amepata suluhisho la ufundi...

Wakuu...., asanteni sana kwa ushauri. Nimefanikiwa kupata design kadhaa za paa na ushauri mwingi sana. Ukweli ni kwamba hizo hela ni ndogo, nimefanikiwa kupata bati za migongo midogo 120 kutoka jeshini (rangi ya blue). Fundi ameniambia niongeze walau million 3 ili nyumba imaliziwe na kuezekwa. Kwa bahati nzuri million 3 zimepatikana na sasa mambo yanaendelea. Nitawaletea mrejesho wa nyumba baada ya kuezekwa ndani ya wiki 2. Siwezi kutaja majina ya wote walio toa ushauri na wale walio ni-PM. JF daima...Thanks....
 
Hongera sana mkuu kwa hatua hiyo kubwa mno, ninakutakia yale yote yaliyomema. Hata mimi nimefanikiwa mengi kupitia ushauri wa marafiki wa kweli kutoka JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…