Msaada: Nataka kuezeka nyumba hii


Wazo zuri hilo hasa kwenye suala la mbao, thanks
 
kwa mwonekano wa nyumba kwa makadirio ina upana wa kama 30ft na urefu kama 50ft. Bati ya 28 gauge na mbao treated 4m inaisha, atafute pesa ya fundi.

Hivi inaweza kula bati kiasi hapo mkuu? naona una aidea kidogo.....
 

Asante King, kweli jamii forums ni jumba la maarifa...., ila ishu ya kuanza kutafuta minazi iliyoanguka ni ishu kubwa. Ngoja niulize wazoefu hapa kitaaa......., Asante kwa ushauri mzuri sana
 
Nakushari kwanza Badilisha Avatar,unaitwa NJAA?
Kuna majina mengine mungu hupenda kuyapa yanachokiamini.
Sasa kama upepo utapitia kwako,basi umaskini hadi unaingia kaburini.
Ni mtizamo wangu tu huo,ndio maana maandiko yanasema,wapeni watoto wenu majina mazuri.
Humu kuna ujumbe wa mungu ndani yake.

Tukija kwenye issue ya kuezeka.
Kwanza nakupongeza kwa kuzichanga,maana nikiiangalia nyumba itakuwa ilisimama si chini ya miaka miwili.
Nimependa sana ulivyokuwa makini katika ujenzi wa madirisha makubwa,nime Appreciate sana hilo.
Halafu kuwa makini sana na hao wanajeshi,naungana na jamaa hapo juu,wengi siku hizi nao wasanii maana wanajua watu wanawakimbilia wao,labda ukifanikiwa kupata jeshi wa kike.Ungekuwa huku Znz ningekuunganishia mdada mmoja.
Pili,kuna watu humu wameanza Pms nyingi,pia kuwa makini,Maana wewe umeomba tu ushauri na sio mambo ya Pm,huko watakuletea usanii pia,maana humu namo matapeli wamo kibaoo.

Ushauri wa Kingkong:-
Mnazi watu wanaudharau sana,lakini ni mbao zinadumu kwa muda mrefu sana.
Kwa watu wa mikoa ya pwani ikiwemo Zanzibar wanaijua Minazi ilivyo.Thamani nyingi sana za majumba zimetengenezwa kwa minazi.Na hata mahoteli ya Coast hapa ukitembelea bado mnazi umesanifiwa kwa hali ya juu sana huwezi kuamini kama ni mnazi.
Fanya uwezavyo ili uweke gharama chini,then ukitaka anasa utafanya wakati mwingine.Jiji hilo kupanga ni kama jela.Ikikaribia muda wa kulipa kodi mtu unakonda.
Huku Zanzibar kuna watu wengi sana kwa kukataa adha hiyo wamejenga nyumba nusu,kisha mtu anahamia na anaimalizia yumohumohumo ndani,na mtu akikuambia alihamia ikiwa nusu huwezi kuamini kwa jinsi ilivyo bomba.
Mbao treated ni uzushi tu,mie hapa ninapoishi fundi alisema ni treated,ila yale madudu baada ya miezi sita tu yalianza kula mbao kama wazim,kuna jamaa ndio akanipa dawa ya kupata,ila ni msiri wala hakuniambia ni nini,mie alinipa tu,maana ni mtu wa mitishamba,ila ilikuwa kama mti fulani aliusaga na kuuloweka kama wiki kisha akaniambia paka,basi hata sisimizi hasogelei.



Mie pia ni miongoni mwa wanaoamini kwamba zinatosha,cha msingi tumia basic roof set up itakusaidia,ila kama unataka anasa kwa kuweka paa na bati za kisasa hiyo utaishia njiani.Fuata ushauri wa fundi na sio wewe kufanya kujua kuliko yeye.
Ushauri kwa wana Jf:Kila mwenye familia ajaribu kujitolea kumsomesha ndugu yake yoyote VETA au sehem yoyote ya ufundi wa aina yoyote.Au hata kumsomesha Kijana unaemuona mtaani anakipaji cha ufundi hata kama sio ndugu yako nahana uwezo..
Mie wakati na jenga chanika sikupata shida,maana Fundi wa Nyumba ni Mjomba wangu,so hapa nilisave sana,na kuezeka ni mwanae,hapa pia nilisave sana gharama.Umeme alinifanyia Collegemate mwenzangu.
Yaani kuna vitu vingi sana Familia lazima iwe navyo katika miomboni kwa members.
Mfano wa Pili ni Upande wa Biashara yangu ya Carry,nikwamba Drivers wawili ni ndugu zangu yaani upande Mama yangu Mdogo,na pia kwanza walianzia kupitia Gerage miaka kibao,kwahiyo hapo sina gharama ya Fundi na gari zinatuzwa vizuri sana.Na ndio maana inanipa hamasa pia nihamishe mmoja kwenye Daladala nikiipata.


Wife pia taalum yake ni kushona,na pia nilimpeleka kozi za kutengeneza Udi,Sabuni,Ice Cream,mwezi ujao nampeleka Sido kujifundisha Kusingika asali ambapo ndio up comming project yetu.
Mtu kujifunza sio lazima ufanye kazi hiyo,ila ujuzi kuwa nao ni muhim sana.Maana huwezi amini mie Wife ni Standard Seven tu lakini she kwows much kuliko mie.Na baadhi ya vitu inabidi nipigwe shule.Please wenzangu naomba tusidharau hivi vikozi vidogo na kuona kama ni vya watu wa elim za chini,nyingi ni muhim sana na huko ipo njia ya mafanikio katika famila zetu.

Ni mtizamo wangu tu,kuna vitu vingi tunaingia gharama kubwa sana bila sababu ya msingi.
 

nice talks
 
Sijuhi unaweka mbao za aina gani, namaanisha za kenchi, kama ni zile treated, hiyo pesa ni ndogo
Na ni vizuri zaidi akatumia mbao hizo kwa afya ya kudumu ya paa lake. Vinginevyo kwa M. 4 ukijumlisha na gharama za ufundi bado iko chini kidogo....
 
Wazo lako ni zuri sana, ila nadhani ingependeza zaidi kama ungemuunganisha na huyo fundi mwenye gharama nafuu....
 
Wazo zuri sana.ila nadhani ungemuunganisha na huyo fundi mwenye gharama nafuu kidogo ungemsaidia sana mwenzetu mleta uzi.
 

probably the best message of day
 

Mkuu nakukubali..mbao za treated nyingi ni fake..jirani yangu saivi anaalamika...paa la nyumba yake linazidi kwisha..mbao alinunua baguruni jamaa wamempa fake..mbaya zaidi ameweka bati kama vigae..ni issue kubwa
 

Asante mwanajamvi, umeeleweka sana, thanks
 
Mkuu design ya paa ni kuona plan au picha zote 4 eevation.ukubwa hapa hauonekani.hata hivyo bati pekee zinaweza kula hela hiyo.
 
Hivi inaweza kula bati kiasi hapo mkuu? naona una aidea kidogo.....

makadirio ya bati yanategemea mchoro na hesabu yake ngumu kwa sisi mafundi mchundo, ngoja nijaribu kukumbuka Veta; kama ina upana wa kuishia bati ni ft 28 king post itakuwa kama 14ft ulalo wa bati utakuwa kama ft 19.8, na urefu wa futi 48; eneo iltakuwa 20x48x2 , idadi ya bati 2x48x2/3 10%=70 hii kwa mgongo wa Tembo.
Nani anajenga mgongo wa Tembo miaka hii!
Kulingana na pendekezo la mchoro bati 110 zinaweza kukupa paa zuri la kupendeza.
 
Nimevutiwa na utaratibu uliotumia kuja hapa JF ili angalau uwe na tahadhari. Aliyekushauri kwenda na kipimio chako unaponunua mbao ni sahihi,kile kipimo chao wanakata katikati.
Kuna jambo lingine nikushauri,utakapopata fundi ni muhimu uone kazi yake kwanza aliyomaliza upime ubora,mafundi wengine ni wasanii anaweza kukuharibia na hutakuwa na jinsi ya kumshtaki na kulipwa. Mimi nimelazimika kupaua upya nyumba niliyoezeka mwaka jana August,mvua za mwaka huu ziliishia ndani kwa kuvuja.
 

Daah hiyo noma, pole sana mkuu..., naomba isinitokee...
 
nitumie upana wa nyumba na urefu.tuma kwenye 0787803577
niidesign ktk archcard then nikupe hesabu kamili mkuu.
 
Mkuu unavyoomba ushauri wa design ya hilo paa ina maana hukujenga kwa kutumia ramani? Ramani uliyotumia kujenga si ina roof plan tayari? Pili, hiyo hela kwa uhalisia ni ndogo, ungepata fundi akupigie mahesabu ya bati ngapi zinahitajika ununue kwa hiyo hela then ujichange zaidi hela ya mbao na labour charge
 
Ombi lako halijajitosheleza. hauwezi kukadiria kwa kutazama picha weka vipimo vya urefu na upana. nikupe makadirio. kwa pesa hiyo nunua bati za Simba dumu 30g ni nzuri. bando ni bati 16 sh.235,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…