Inakuwaje mkuu. Inategemea unahitaji ngapi. Ila kama unataka nyingi tengeneza mwenyewe za zege ni gharama nafuu na rahisi kutengeneza. Chukua ndoo kubwa na ndoo ndogo. Weka udongo nusu kwenye ndoo kubwa.
Kisha weka gazeti au karatasi kati kati.paka oili chafu kwenye mzunguko wa ndoo kubwa kwa ndani. Ile ndoo ndogo paka nayo oili chafu kwa nje. Then koroga zege vipimo cement kipimo kimoja mchanga vipimo vitatu.
Mimi natumia beleshi moja iliyojaa cement na tatu za mchanga. Inatosha kwa kazi hiyo. Koroga vikiwa vikavu vichanganyike vizuri. Then weka maji kidogo then anza kwa kuweka zege ndani ya ndoo kubwa halafu weka ndoo ndogo juu yake then weka zege kwenye mzunguko kati ya ndoo ndogo na kubwa huku unatikisa tikisa mpaka ienee kote. Iache ikauke.
Baada ya masaa kumi, toa ndoo ndogo na toboa shimo la kutolea maji kwa bisibisi . kutokana na hali ya hewa acha ikauke kabisa then geuza ndoo juu chine utoe pot lako