Msaada natafuta mganga mashuhuri wa jadi

Deepro

Member
Nov 3, 2016
63
54
Husika na kichwa cha habari.,
Mimi ndugu yenu nina matatizo ambayo hayahusiani na hospital (siumwi) ila ni masuala binafsi ya biashara zangu hivyo naomba anayejua mganga anayeweza kuninyooshea mambo fasta anipe maelekezo kwa Pm ntashukuru sana.!
Kama mjuavyo kumekuwa na matangazo mengi kwenye nguzo za umeme kuhusu waganga lakini kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua hao wengi huwa matapeli tu ila mganga original huwa hajitangazi.
Natumaini haya ni mambo ya kiimani zaidi na humu jukwaani lazima kuna wadau tupeane "mchongo"
Pia niwaombe radhi wale ambao wataingiza habari za dini humu kwani kama dini kila mtu ana dini yake na imani yake na ana uhuru wa kuabudu anachokiamini.!
Hivyo ukiona mada iko tofauti na imani yako pita kimya.!
Ntashukuru kwa mtakaojitahidi kunisaidia walau "direction"
 
Mtoto ukililia wembe ngoja tukupe
Ni kweli baadhi waganga wa kukuza biashara ni matapeli

Ushauli unaokufaa
Nikushauli ukitaka waganga watakao kufaa wa kukuza biashara zako nenda pale posta,
hao ni wauhakika wanaofisi kubwa sana wamesajiriwa na serikari na shughuri zao ni kukuza biashara na kutajilisha watu
Ukifika pale posta uliza ilipo ofisi ya Freemasonihy uliza kwa madereva wa tax au mtu yeyote atakuonyesha

Hao ni wa uhakika na wana Leseni ya kazi yao hiyo

Nenda hapo ndugu utafanikiwa.
 
Siwezi kupita kimya kwa sababu ninakupenda na sitaki uendelee kuamini katika GIZA. Kwanini umwamini shetani ambaye hatima yake ni moto wa milele yeye pamoja na wafuasi wake? Mungu anakupenda ndugu yangu ña anataka umfuate Yeye ili uwe na uhakika wa maisha haya na yale yaliyo ya baada ya haya yaani UZIMA WA MILELE. Njoo kwa Yesu akuweke huru! uondokane na utumwa wa ki- ibilisi.
 
Uushirikina hautakunufaisha hata siku moja, hali ya uchumi kudorora unadhani mganga ataitatua?. huyo mganga mwenywe sasa hivi anatafuta wateja maana wale wa kwenda kutafuta wapenzi hawana pesa siku hizi. ukienda atashukuru kweli walau nae atapata hela ya chakula. imani potofu za kishirikina ndio mwanzo ya matatizo yote, watakwambia hadi uwaroge na ndugu zako huko. maana ndio gia yao hiyo kwamba ndugu zako ndio wanafanya biashara yako idorore. elimika
 
Husika na kichwa cha habari.,
Mimi ndugu yenu nina matatizo ambayo hayahusiani na hospital (siumwi) ila ni masuala binafsi ya biashara zangu hivyo naomba anayejua mganga anayeweza kuninyooshea mambo fasta anipe maelekezo kwa Pm ntashukuru sana.!
Kama mjuavyo kumekuwa na matangazo mengi kwenye nguzo za umeme kuhusu waganga lakini kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua hao wengi huwa matapeli tu ila mganga original huwa hajitangazi.
Natumaini haya ni mambo ya kiimani zaidi na humu jukwaani lazima kuna wadau tupeane "mchongo"
Pia niwaombe radhi wale ambao wataingiza habari za dini humu kwani kama dini kila mtu ana dini yake na imani yake na ana uhuru wa kuabudu anachokiamini.!
Hivyo ukiona mada iko tofauti na imani yako pita kimya.!
Ntashukuru kwa mtakaojitahidi kunisaidia walau "direction"
Kaka mganga kiboko wakukunyoshea mambo yako Kwa mda mfupi ni Yesu basi uyo ndie kiboko ukitaka kujua njoo in box utajuta kumfahamu
 
Back
Top Bottom