Msaada: Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo

Msaada: Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo

huyo mtaalamu wako labda alijichanganya...ukipima H.Pyroli test lazima irudi kuwa positive sababu mwili una antibdoy tayari vs huyo mdudu.
Hivo haishauriwi kupima H.Pyroli test i.e kwa njia ya damu baada ya kumaliza doze yake....inabidi kupima Fecal stool antigen au vpimo vingine zaidi vizuri ambavyo viko very specific kudetermine kama mdudu ametoweka kwenye damu.

Vipimo vingi vya ku check antibody huwa sio vizuri wakati mwingine,ni sawa na ku check HIV antibody test kwa mtoto mchanga alozaliwa kwa mama mwenye HIV/AIDS ukitegemea itakua Negative.(wakati mama anampsia mwanae antibody).Antibody test inaweza kuwa positive na vipimo kama PCR kigawa negative ambacho ndo kipimo sahihi kama unaelewa sayansi nyuma yake.

Na kuwa na H.Pyroli test positive haikuondolei wewe kuwa na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na chanzo kingine.
Hivo ni vema kuwa cautious kwamba kama chanzo kimoja akijapona na dawa umetumia kwa usahihi basi maana yake kuna chanzo kingine na ni rahisi kukitafuta ukionwa na daktari ambaye anafanya kazi kwenye hospitali zenye nyenzo.

Na point ya tatu ya msingi ni kwamba hao wadudu wengi wao nao sio malofa wengi wao wana mutate na kutengeneza resistance dhidi ya dawa...Hivo kuna First,Second and third line ya matibabu...IKigoma ya kwanza maana yake usiendelee kumeza first line inabidi daktari akuhamishie second line na hili ni swala la maarifa ya wataalamu utakaokutana nao kuchanganua hizi hoja tatu na kuendelea kukutibu wao kukupatia rufaa kwenda kwa Gastro-Enterologist maana madaktari wengi wamesoma ile general medicine na kuna maarifa wanakua Shallow na hapo linapokuja swala la kumpatia mtu rufaa aonwe na watu walobobea


Ushauri: Nenda hospitali ya MKoa omba rufaa kwenda kwa Gastro-enterologist hao ndo wamesoma miaka zaidi ya mita wakisomea matumbo tu nje na miaka mitano ya udaktari wa kawaida na nje na miaka mitatyu ya u specialist wa kawaida.

Jumla wamesoma miaka 11 kwenye fani ya udaktari na lazima tukubali kuwa hiyo miaka ya ziada wana kitu cha ziada wanakijua.
Nakushukuru kwa ushauri huu mujarabu mkuu. Nitaufanyia kazi kwa 100%.
 
Nimeshuhudia wagonjwa wenye tatizo kama lako wakipona kupitia hospital, inategemea na aina ya dawa unazopewa.

Dose, unapewa heligo kit 2 kwa siku 14 then kuna dawa ya liquid ipo kama maziwa unapewa vichupa viwili then ukimaliza hizo kit kuna dawa ya siku 30 na unameza kidonge kimoja kwa siku kabla ya kulala chochote.

Rudi hospital utapewa kama hizo, zimewasaidia watu wengi, Allah akufanyie wepesi upate kupona.
Hizo dawa hua hazitibu bali zinatuliza kwa muda...
 
Tafuteni majani na mbegu za mlonge, saga pamoja kwenye lishe unakua unakoroga uji unakunywa asubuhi na jioni.... utaharisha usiogope itakata weww endelea hadi kwa siku 30 kisha jaribu kula kitu cha kutibua vidonda kama bado endelea na dozi kwa mwezi mwingine.

NB: Hii ni tiba lishe haina madhara.
 
Poleni sana jamani yupo mama mmoja ni bingwa wa kutibu hivyo vidonda vya tumbo anapatikana chalinze,unashuka kituo kinaitwa PINGO STEND hii ni kabla haujafika chalinze mwisho,pingo zipo nyingi so muhimu kumwambia konda hivyo hivyo nishushe PINGO STEND,Ukishuka vuka barabara kama utakua unatokea dar,mchukue bodaboda mwambie nipeleke kwa MAMA DINA mama wa kimasai anavaa miwani.Gharama ya dawa yake ni 150,000 yan LAKI NA NUSU.Kwa atakae enda akitumia hiyo dawa uje uwahadithie na wenzako humu humu.Na akikuuliza nani aliekuelekeza huku mwambie mwanao anaekaa kariakoo.Namba zake hizo 0657 82 14 56 akiwauliza mmemjuaje mwambieni hivyo hivyo mwanao wa kariakoo ndio amenipa namba.
Samahani mkuu naomba utoe direction vizuri zaidi. Hiyo kabla hujafika Chalinze Mwisho ni kama unatokea Dar au Moro? Na hiyo Chalinze Mwisho ni ipi? Au ni pale njiapanda ya kwenda Tanga? Fafanua zaidi kiongozi wangu.
 
Back
Top Bottom