Msaada: Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo

hunter2018

Member
Aug 12, 2018
9
7
Nasumbuliwa navidonda vyatumbo takribani km miaka miwili sasa'kwahyo naomba km kunamwenye kuweza kunisaidia kwakunifahamisha dawa yakunisaidia ili hili tatizo langu liweze kupona nakuisha kabisa.

MziziMkavu
 
Nasumbuliwa navidonda vyatumbo takribani km miaka miwili sasa'kwahyo naomba km kunamwenye kuweza kunisaidia kwakunifahamisha dawa yakunisaidia ili hili tatizo langu liweze kupona nakuisha kabisa...Mzizi Mkavu.

angalia usijenyweshwa juice ya kabichi!
Nenda hospitali upime ujue vidonda vyako vimeletwa na nini ili uweze kutibu chanzo...usipotibu chanzo vitakuja ku kugeuka sikumoja!

complications zake!
1.Kutoboka
2.Kuvujia damu na kukufanya uishiwe damu kila mara
2.Unaweza pata cancer ya tumbo.
 
Nimeshaenda hospital'huwa wananipaga dawa nakunywa vnatulia km 1wk au 2wk hivi"arafu vinaanza kusumbua tena
 
Mkuu, ugonjwa wa vidonda vya tumbo hauponi hospitali hata kama ikigungulika chanzo cha tatizo. Mimi nina tatizo la vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na bacteria wa H. pylori lakini nimetibiwa hospitalini imeshindikana. Naomba mwenye kufahamu tiba asilia inayoweza kuniponyesha anisaidie. Hili tatizo la vidonda ni kubwa sana miongoni mwa wanajamii.
 
Kuna dawa nimetumia hivi karibuni ni ya miti shamba kwa imenisaidia kwa asilimia kubwa sana naweza kusema nimepona kama vp nikuelekeze
 
Mkuu, ugonjwa wa vidonda vya tumbo hauponi hospitali hata kama ikigungulika chanzo cha tatizo. Mimi nina tatizo la vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na bacteria wa H. pylori lakini nimetibiwa hospitalini imeshindikana. Nomba mwenye kufahamu tiba asilia inayoweza kuniponyesha anisaidie. Hili tatizo la vidonda ni kubwa sana miongoni mwa wanajamii.

Nimeshuhudia wagonjwa wenye tatizo kama lako wakipona kupitia hospital, inategemea na aina ya dawa unazopewa.

Dose, unapewa heligo kit 2 kwa siku 14 then kuna dawa ya liquid ipo kama maziwa unapewa vichupa viwili then ukimaliza hizo kit kuna dawa ya siku 30 na unameza kidonge kimoja kwa siku kabla ya kulala chochote.

Rudi hospital utapewa kama hizo, zimewasaidia watu wengi, Allah akufanyie wepesi upate kupona.
 
Nenda hospital upimwe ili chanzo cha vidonda ifahamike,mfano huenda n asidi nyingi kuzalishwa kutokana na magonjwa mbalimbali kama uvimbe(gastrinoma),bacteria aina ya H.pyoli n.k....so nenda upate Tiba ...kuna combination therapy utapewa ya dawa tatu hadi NNE zikiwemo metronidazole,tetracycline,bismuth cpds,n.k....
NB: usimeze bila ushaur wa daktari
 
Mkuu, ugonjwa wa vidonda vya tumbo hauponi hospitali hata kama ikigungulika chanzo cha tatizo. Mimi nina tatizo la vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na bacteria wa H. pylori lakini nimetibiwa hospitalini imeshindikana. Nomba mwenye kufahamu tiba asilia inayoweza kuniponyesha anisaidie. Hili tatizo la vidonda ni kubwa sana miongoni mwa wanajamii.
N kweli inawezekana usipone kwa sababu hawa bacteria wanaresistance ...but ukimpata mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa chakula aliyebobea unaweza kupona kabisa....
 
Nimeshuhudia wagonjwa wenye tatizo kama lako wakipona kupitia hospital, inategemea na aina ya dawa unazopewa.

Dose, unapewa heligo kit 2 kwa siku 14 then kuna dawa ya liquid ipo kama maziwa unapewa vichupa viwili then ukimaliza hizo kit kuna dawa ya siku 30 na unameza kidonge kimoja kwa siku kabla ya kulala chochote.

Rudi hospital utapewa kama hizo, zimewasaidia watu wengi, Allah akufanyie wepesi upate kupona.
Asante kwa taarifa hii mujarabu mkuu. Basi yawezekana mimi nilipata tiba nusu au robo. Nilimezeshwa dawa ya heligokit ambayo nilikuwa nameza vidonge vitatu asubuhi na vitatu jionii kwa muda wa mwezi mmoja; ikifuatiwa na umezaji wa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Kisha nikaenda kupima nikakuta bacteria bado wapo wa kutosha. Nilipomuuliza daktari imekuwaje sijapona akanambia huenda nimepata new infection. Again nikapewa dozi ya pili kwa mtiririko huo huo. Baada ya kumaliza dozi hii ya pili, nikaenda kupima na kukuta bacteria wapo. Nikakata tamaa na kuamua kubaki na bacteria wangu hadi nitakapopata tiba asilia.

Mkuu, naomba kama kuna hospitali inayotibu ugonjwa huu unielekeze niende nikatibiwe maana hivi vidonda vimenitesa kwa muda miaka 16 sasa (tangu mwaka 2002). Hata mtu akiniambia mavi yanatibu nipo tayari kula ilimradi nipone. Natanguliza shukrani.
 
Nenda tu hospital hizi za government utatibiwa tu kama nilivyokwambia.

Tumia heligokit kwa siku saba pamoja na ile ya maji then 7 tena pamoja na ile ya maji. Ukimaliza unganisha na ile ya mwezi mmoja kabla hujaweka kitu chochote then acha ifanye kazi kwa muda wa masaa matatu.

Bacteria hawaishi haraka hivyo, wanachukua muda kupotea lakini tumbo linaacha kusumbua.

NOTE: ikishindikana kabisa, anatibu magonjwa mengi ila anagharama kweli. Naomba hii iwe option ya mwisho
 
Nimeshaenda hospital'huwa wananipaga dawa nakunywa vnatulia km 1wk au 2wk hivi"arafu vinaanza kusumbua tena
Kunywa juisi yenye mchaganyiko wa kabeji, bamia na karoti. Glass 1 asubuhi na jioni kwa miezi 3. (usisahau kuleta mrejesho hapa)
 
Nenda tu hospital hizi za government utatibiwa tu kama nilivyokwambia.

Tumia heligokit kwa siku saba pamoja na ile ya maji then 7 tena pamoja na ile ya maji. Ukimaliza unganisha na ile ya mwezi mmoja kabla hujaweka kitu chochote then acha ifanye kazi kwa muda wa masaa matatu.

Bacteria hawaishi haraka hivyo, wanachukua muda kupotea lakini tumbo linaacha kusumbua.

NOTE: ikishindikana kabisa, anatibu magonjwa mengi ila anagharama kweli. Naomba hii iwe option ya mwisho
Nakushukuru sana kwa taarifa hii muhimu mkuu. Ushauri wako nitaufanyia kazi 101%.
 
Asante kwa taarifa hii mujarabu mkuu. Basi yawezekana mimi nilipata tiba nusu au robo. Nilimezeshwa dawa ya heligokit ambayo nilikuwa nameza vidonge vitatu asubuhi na vitatu jionii kwa muda wa mwezi mmoja; ikifuatiwa na umezaji wa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Kisha nikaenda kupima nikakuta bacteria bado wapo wa kutosha. Nilipomuuliza daktari imekuwaje sijapona akanambia huenda nimepata new infection. Again nikapewa dozi ya pili kwa mtiririko huo huo. Baada ya kumaliza dozi hii ya pili, nikaenda kupima na kukuta bacteria wapo. Nikakata tamaa na kuamua kubaki na bacteria wangu hadi nitakapopata tiba asilia.

Mkuu, naomba kama kuna hospitali inayotibu ugonjwa huu unielekeze niende nikatibiwe maana hivi vidonda vimenitesa kwa muda miaka 16 sasa (tangu mwaka 2002). Hata mtu akiniambia mavi yanatibu nipo tayari kula ilimradi nipone. Natanguliza shukrani.

huyo mtaalamu wako labda alijichanganya...ukipima H.Pyroli test lazima irudi kuwa positive sababu mwili una antibdoy tayari vs huyo mdudu.
Hivo haishauriwi kupima H.Pyroli test i.e kwa njia ya damu baada ya kumaliza doze yake....inabidi kupima Fecal stool antigen au vpimo vingine zaidi vizuri ambavyo viko very specific kudetermine kama mdudu ametoweka kwenye damu.

Vipimo vingi vya ku check antibody huwa sio vizuri wakati mwingine,ni sawa na ku check HIV antibody test kwa mtoto mchanga alozaliwa kwa mama mwenye HIV/AIDS ukitegemea itakua Negative.(wakati mama anampsia mwanae antibody).Antibody test inaweza kuwa positive na vipimo kama PCR kigawa negative ambacho ndo kipimo sahihi kama unaelewa sayansi nyuma yake.

Na kuwa na H.Pyroli test positive haikuondolei wewe kuwa na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na chanzo kingine.
Hivo ni vema kuwa cautious kwamba kama chanzo kimoja akijapona na dawa umetumia kwa usahihi basi maana yake kuna chanzo kingine na ni rahisi kukitafuta ukionwa na daktari ambaye anafanya kazi kwenye hospitali zenye nyenzo.

Na point ya tatu ya msingi ni kwamba hao wadudu wengi wao nao sio malofa wengi wao wana mutate na kutengeneza resistance dhidi ya dawa...Hivo kuna First,Second and third line ya matibabu...IKigoma ya kwanza maana yake usiendelee kumeza first line inabidi daktari akuhamishie second line na hili ni swala la maarifa ya wataalamu utakaokutana nao kuchanganua hizi hoja tatu na kuendelea kukutibu wao kukupatia rufaa kwenda kwa Gastro-Enterologist maana madaktari wengi wamesoma ile general medicine na kuna maarifa wanakua Shallow na hapo linapokuja swala la kumpatia mtu rufaa aonwe na watu walobobea

Ushauri: Nenda hospitali ya MKoa omba rufaa kwenda kwa Gastro-enterologist hao ndo wamesoma miaka zaidi ya mita wakisomea matumbo tu nje na miaka mitano ya udaktari wa kawaida na nje na miaka mitatyu ya u specialist wa kawaida.

Jumla wamesoma miaka 11 kwenye fani ya udaktari na lazima tukubali kuwa hiyo miaka ya ziada wana kitu cha ziada wanakijua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom