Msaada: Napendwa na wasichana mpaka kero

bishororo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
254
Reaction score
358
Habari wapendwa,

Poleni na majukumu ya kazi na kujenga mimi ni kijana wa miaka 27 kimaumbile nipo kawaida mrefu wa wastani, maji ya kunde kifupi najiona mtu wa kawaida lakini nashanga jinsi watoto wa kike wanavyonisumbua na kujirahisisha kwangu wengine mpaka wanadiriki kunitongozaa na kunihonga bila kuomba.

Tatizo hili nimeanza nalo toka mdogo nilipoanza kujitambua ikafika kipindi mpaka wakinamama wananitaka kimapenzi kinguvu hata ikafikia kipindi mpaka mahouse girls wanataka niwape utamu nikawa sina raha wasichana wanapigana kisa mimi wengine kunywa mpaka sumu.

Mpaka sasa hivi sielewi imekuwa kero sasa wake za watu wananisumbua wasanii wakubwa wazazi wa marafiki zangu naumia sana sitoki nje sasa hivi naogopa wasichana wakiniona wanachanganyikiwa.

Kwa tatzo hilo nikaamua kwenda kwa ustaadhi kumwelezea alichoniambia sitaki kuamini eti na jini linalonifanya nipendwe na nisipoangalia nitapata maradhi mpaka nilitoe, jamani mpaka sasa sijui nifanyeje.

Nini msaada wenu tafadhali?
 
Weka na picha yako mkuu, tukuthaminishe[emoji23] [emoji23]
 
Weka picha kwanza, maana nimeona unakuja kujitangaza hapa jukwaani! Sijui ndio ninyi mnaotafutwa na Mh. Kigwangala
 
Itakuwa Radhi ya kuwaona wazazi wakiduu
 
Haya maneno tutaaminije sasa, weka ushahidi wa picha jinsi wanavyokufatafata au kukusumbua ili tukushauri.
 
naona namba inasomeka vizuri..
Darasa la 7 mtahitimu mnajua kusoma na kuandika sasa...

Mh.ongeza!!
 
Mkuu usiwe unakuja na post za namna hii, kama ni mwanaume kweli unajidhalilisha sana, wanawake wenyewe wanaotongozwa mara kibao hawaji kulia lia jukwaani, iweje kwako mwanaume??
Mimi mwanaume sa ka mm naliona ttzo nkae kimya tuuu
 
Man wala ucogope.. just kuwa na msimamo... wakukataaa... wale ambao unaona hawana nia njema. And wala ucogope kutoka nje..
Ww endelea na shughuli zako... lakin kuwa na msimamo na uwe makini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…