Msaada: Naomba ushauri kuhusu kuwekeza kwenye mazao

ibra017

Member
Dec 7, 2023
5
6
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa kwanza, nilikua nawazo la kuanza kuwekeza kwenye kilimo kupitia boom langu.

Sasa ni kwamba kwasasa sijui ni aina gani ya mazao ambayo nitaweza wekeza na yakanipa faida kutokana na hali yenyewe jinsi ilivyo ya kiuchumi, na ni vema nianze na kiwango gani cha mtaji.

Naombeni msaada tafadhari
 
mi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa kwanza, nilikua nawazo la kuanza kuwekeza kwenye kilimo kupitia boom langu Sasa ni kwamba kwasasa sijui ni aina Gani ya mazao ambayo nitaweza wekeza na yakanipa faida kutokana na hali yenyewe jinsi ilivyo ya kiuchumi, na ni vema nianze na kiwango Gani Cha mtaji.
Naombeni msaada tafadhari
Mkuu, Mimi ushauri wangu ni huu, sikushauri uwekeze kwenye kilimo wakati ukiwa chuo. Maana yangu ni kwamba kilimo kizuri ni kile upo site unasimamia mwenyewe, ogopa sana kilimo Cha kuweka mtu alafu wewe unakuwa ni mtu wa kupiga simu tu. Sijajua upo eneo ulilopo ni karibu na ilo shamba au ni mbali.

Ushauri wangu kwa mara nyingine ni huu, ni Bora ungetafuta shughuli ambayo wewe ungekuwa karibu na usimamizi asilimia mia. Hata kama ni hapo Chuo najua Kuna furusa za kufanya, Kwa mfano unaweza kuwa unaagiza dagaa wa mwanza walio kaangwa then unafunga kwenye mifuko unauza around chuo na maeneo ya jirani.
Utapata pesa Yako ambayo Haina stress.
 
Ili ufanikiwe kwenye kilimo kunahitaji vitu 3

1.Usimamizi.
Unao muda wa kutosha wa kuweza kusimamia shughuli zako? Ukikosa muda bora usilime kwa sababu utaibiwa.Wafanyakazi/Vibarua wanaiba sana kuanzia mbegu,mbolea,madawa na mazao yenyewe.

2.Uzoefu.
Hilo zao unalotaka kulima unalifahamu,unajua utunzaji,masoko nk.

3.Mtaji
Fedha za kugharamia shughuli zote kuanzia uandaaji wa shamba,uvunaji na utunzaji baada ya mavuno zipo?Fedha zinatakiwa ziwepo zote,maana unaweza kusema mwezi machi Mjomba atanikopesha fedha za mbolea halafu inafika machi Mjomba hana fedha na huna sehemu nyingine ya kupata fedha hapo mazao yatakosa mbolea na utapata hasara.


Haya hivyo haya ni mawazo yangu tu yanaweza yakawa siyo sahihi na pia ushauri huu umetokana na eneo nilipo.
 
Hoja haiigwi rungu, na ushauri wako umenikumbusha kitu muhimu sana kwenye kilimo, Asante kiongozi napokea ushauri kwa mikono miwili.
 
Subiri msimu wa mavuno.

Ingia vijijini kusanya mahindi, alizeti n.k.

Then weka store kusubiri bei isimame upige bei.
 
Msimu wa mavuno ukifika nunua mazao yawekee dawa then hifadhi.Ukisubiri Bei iongezeke. Tahadhari Usiamini mtu ingia mzigoni mwenyewe Mambo ya kutumia hela wamepigwa wengi, usije ukarudi kutulilia hapa. Ila hakikisha kabla haujaingiza hela watafute wazoefu wa izo kazi, Hakuna biashara nyepesi Piga kazi.
 
Back
Top Bottom