Msaada: Naomba kujuzwa Hospital nzuri ya macho Kigamboni

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
Habari ya usiku huu wapendwa.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,nimekuwa nikisumbuliwa na kichwa mara nyingi sana.

Juzi kilinizidi mpaka nikahisi ni corona Wallah😂😂😂 (maisha kweli matamu) ikabidi niende kufanya vipimo nikakutwa na nilichokutwa na dawa nikapatiwa lakini bado kichwa kinaniuma sana.

Kuna kipindi mtu alinigonga na kiwiko kwenye jicho bahati mbaya siku iliyofuata nikashindwa kufungua macho kabisa. Nikaendea hospital nikapatiwa dawa likakaa sawa. Baadae tena likaanza kunisumbua nikaenda hospital nikapatiwa dawa nikatumia likakaa sawa.imepita mda kidogo.

Wiki kama mbili tena limenianza kuuma nikilifungua kunakuwa na vitu kama vinachomachoma.na upande jicho linalouma,ndipo na kichwa kinauma mno upande huo huo.

Asanten
 

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
396
500
Mimi nafanya kazi medewell health center ipo Kibaha tunayo huduma hiyo, unaweza ukaja kutembelea tuna kitengo cha macho kizuri ambapo tuna fanya operation ya mtoto wa jicho bure bila garama yoyote endapo utagundulika na tatizo hilo.

Pia gharama ya kumwona Daktari wa macho elfu 5. Pia gharama hizi haziambatani na za dawa. Pia tu kwanini tunafanya cataract bure. Ni bure kwakuwa ni charitable center hivo kama na ndugu jamaa rafiki mlete asaidiwe na hawa wahusika wa macho wenye shida ya mtoto wa jicho.

Medewell ipo Kibaha Mpakani Mezani ya zamani. Ukishuka hapo utaona bodaboda wengi tu watakufiksha mpka kituo cha hudumua bodaboda ni shiling elfu moja tu. Hivyo siku za huduma za macho kuanzia j3 hadi alhamisi. Unashauriwa kuwah alfajiri sana ya saa kumi na mbili na nusu hadi saa moja kamili uwe umefika. Pia unaanza mapokezi utawaeleza umekuja kwenye huduma ya macho utapewa namba.na utaelekezwa wapi pa kwenda kulipia hiyo elfu 5 yako.

Unashauriwa kuwahi kuchukua namba ili kuwa miongoni mwanaotakiwa kumwona daktari kutokana na idadi iliopangwa ndan ya siku hiyo.

Hivyo bas kama utagundulika na shida ya ya mtoto wa jicho utaandikwa kwenye kitabu maalumu kukuweka kwenye orodha ya watu wa kufanyia upasuaj huo mdgo. Kisha utaambiwa ukae karibu na simu yako watakupigia simu ndan ya week mbili.
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,584
2,000
RAKI BIG ahsante kwa maelezo mazuri na yanaweza kuwasaidia wengi.

Lakini kwa maelezo ya Chakorii tatizo lake sio mtoto wa jicho anasema shida imeanza baada ya kugongwa, sio mtaalam ila huenda hicho ikawa chanzo cha mtoto wa jicho?

Nashauri atafute hospitali ya macho lakini pia iangaliwe hiyo kugongwa kama imeathiri sehem za ndani za kichwa zinazosababisha hayo maumivu.

Likija suala la afya, upatikanaji wa huduma hauzingatii ipo sehem gani. Ningeshauri uwatembelee International Eye Hospital wako mbele ya Moroco, Victoria nafikiri upande wa kushoto ukielekea Makumbusho.
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
RAKI BIG ahsante kwa maelezo mazuri na yanaweza kuwasaidia wengi.

Lakini kwa maelezo ya Chakorii tatizo lake sio mtoto wa jicho anasema shida imeanza baada ya kugongwa, sio mtaalam ila huenda hicho ikawa chanzo cha mtoto wa jicho?...
Asante sana mkuu Mungu akubariki .nitakwenda huko.ubarikiwe👏
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
Ubarikiwe pia, kikubwa zaidi nakutakia uponyaji kwa shida inayokukabili. Pole sana.
Mkuu asante sana uzidi kubarikiwa.nilienda INTERNATIONAL EYE HOSPITAL nikapata huduma nzuri sana..lkini nikagundulika ninatatizo kubwa zaidi ya nilivyodhan..

Nimepatiwa dawa bado naendelea kutumia baada ya mwezi nitarudi tena.shukrana sana mkuu
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,584
2,000
Mkuu asante sana uzidi kubarikiwa.nilienda INTERNATIONAL EYE HOSPITAL nikapata huduma nzuri sana..lkini nikagundulika ninatatizo kubwa zaidi ya nilivyodhan..

Nimepatiwa dawa bado naendelea kutumia baada ya mwezi nitarudi tena.shukrana sana mkuu

Amen, nakuombea uponyaji upesi. Barikiwa pia
 

dimple

Member
Dec 6, 2016
33
125
Ni hosp ya macho only au mnatoa na huduma gani zingine?je kwa maswala ya uzazi je?na gharama zipoje?
Mimi nafanya kazi medewell health center ipo kibaha tunayo huduma hiyo, unaweza ukaja kutembelea tuna kitengo cha macho kizuri ambapo tuna fanya operation ya mtoto wa jicho bure bila garama yoyote endapo utagundulika na tatizo hilo.

Pia gharama ya kumwona Daktari wa macho elfu 5. Pia gharama hizi haziambatani na za dawa. Pia tu kwanini tunafanya cataract bure. Ni bure kwakuwa ni charitable center hivo kama na ndugu jamaa rafiki mlete asaidiwe na hawa wahusika wa macho wenye shida ya mtoto wa jicho...
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,890
2,000
bure garama, kwa dar es salaam hospitali nzuri za macho zipo Msasani, Morocco na Victoria wasikudanganye hao wa bure, bure gharama
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
bure garama, kwa dar es salaam hospitali nzuri za macho zipo Msasani, Morocco na Victoria wasikudanganye hao wa bure, bure gharama
54423986-DB80-4372-8968-BBC1750F19C7.jpeg
nenda hapo mkuu hutojutia
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
Nilikuwa ninatatizo la macho nikaenda hospital mbili tofauti lakni hakuna cha maana.

Wanaishia kunipa dawa za maji tu shenzi zao kumbe nilikuwa ninatatizo kubwa ambapo ningechelewa kulitibu basi ingeniletea kutokuona.

Kama uko vizuri nenda hiyo hospital hutojuta
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
Inapatikana victoria ukishavuka jengo la Vodacom mbele kidogo utaiona kama unatokea moroco ni upande wa kushoto

Namba zao 0787888130.kila la heri na ugua pole.Afya nikitu cha muhimu mno
 

Minah 92

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
714
1,000
Inapatikana victoria ukishavuka jengo la Vodacom mbele kidogo utaiona kama unatokea moroco ni upande wa kushoto

Namba zao 0787888130.kila la heri na ugua pole.Afya nikitu cha muhimu mno
Kumuona Daktari kiasi gn? Na je ina include Vipimo au?
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
40,061
2,000
Kumuona Doctor ni 60,000 kama sijakosea...
Vipimo inategemea watataka upimwe nini.kuna kipimo mpaka 300,000 ingawa nilitumia bima..

Gharama za hosptal kwa sie wakoga vumbi ni kubwa sana.....Yaani kuona dokta tu ni elfu 60 tu hatari.....Bora serikali ipambanie kuanzisha Bima ya afya kwa wote.
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
11,071
2,000
Gharama za hosptal kwa sie wakoga vumbi ni kubwa sana.....Yaani kuona dokta tu ni elfu 60 tu hatari.....Bora serikali ipambanie kuanzisha Bima ya afya kwa wote.
Hiyo ni kumuona dactar pamoja na vipimo vidogo vidogo vya awali ila kutaka kujua ni tatizo gani au ni vipimo gani hasa vya kupima ili kugundua tatizo.

Ni hospital nzuri sana,wanahuduma nzuri sana na pia wafanyakazi wake wako friendly sana I recommend....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom