Kuna watu wanachekesha na ushauri wao,mtu amekaa na mama yake zaidi ya miaka 20 ameshindwa kumpa hizo details then mnamshauri ambembeleze mama!
Yeye ndio anamjua mama yake na ndio maana amekuja humu baada ya kushindwa kumshawishi na kuna wale wanamwambia achana naye,jambo kama halijakukuta ni rahisi kuhukumu,sidhani kama anamtafuta ili amuombe msaada ila anataka kumjua ili amfahamu na aondoe hilo doa la kutomjua baba.
Kuna rafiki yangu baba yao alikua na mtoto nje na hakuwaambia ila jamaa alikuja akiwa mtu mzima baada ya kutafuta details za baba na akakaa kama masaa 5 tu baada ya kumuona mzee na family yake akaondoka na hakuacha details zozote alizuga atakuja tena.
Mpaka leo ni zaidi ya miaka 8 hawajui alipo na mzee wao alishafariki