Msaada: Namtafuta Baba yangu

Msaada: Namtafuta Baba yangu

kuna muda nahisi kuna kitu nafichwa kitu sasa ni mtu mzima nahitaji kufahamu ukweli ambao najua siwezi upata kwa mama zangu maana ni kipindi kirefu nimekuwa nikiungoja na kuutafuta
Ukiona kuna kitu unafichwa,jua kuna swala la msingi nyuma yake.Huenda mama amezalishwa na ndugu,anayefahamika vyema na wamama wadogo.Hivyo wameamua kukupoteza maboya.Kuwa na tahadhari kubwa na kuwa tayari kusikia chochote na kuikabili.(ndoa zina siri nyingi
 
Hayupo tayari kuniweka wazi kuhusu hili swala sasa sielewi ni kwann ndo nimefikia maamuzi haya ya kuomba msaada wa taarifa kuhusu yeye

Pole sana, nadhani huenda walitengana katka mazingira yasiyo ridhisha, nakutakia kila la kheri umpate mzazi wako.
 
Naamini utampata tu mzee wako mana damu ni nzito kuliko maji. Huenda mzee wako alimkwaza sana mama'ko ambapo akikumbuka machungu hayo anashindwa kukupa ukweli. Ila wamama siku zote wameumbwa kwa moyo wa huruma, mwambie mama kwa upole huku ukionesha hisia za uchungu mpaka mwenyewe akuonee huruma na usimkaripie. Naamini ukifanya hivyo atakwambia ukweli wote na baba'ko utampata kirahisi.
 
Ngoja nishughulike na namba ulizotoa kwanza!!!
 
kuna muda nahisi kuna kitu nafichwa kitu sasa ni mtu mzima nahitaji kufahamu ukweli ambao najua siwezi upata kwa mama zangu maana ni kipindi kirefu nimekuwa nikiungoja na kuutafuta
Be carefull, ukweli mwingine unauma ukiujua, labda ndio maana unafichwa
 
Mtu aliyeishiwa hoja hukimbilia kwenye kuangalia makosa ya sarufi,cha umuhimu kujua context ilikuwa nini.
Maudhui nitayapataje kama umekosea kuandika?

Huwezi kuwa na hoja halafu ukashindwa kuipresent vizuri,umelewa?
 
Maudhui nitayapataje kama umekosea kuandika?

Huwezi kuwa na hoja halafu ukashindwa kuipresent vizuri,umelewa?
Kwani nilikuwa nazungumzia furniture za zamani kwenye huu uzi? Acha Ujuaji na UBASHITE.
 
Baba yako alikuwa anafanya kazi gani maana mi kuna mtu alikuwa mwalimu na alikuwa anatumia hilo jina A sendeu.. yy alikuwa mtwara huko..
 
Habari wanajamii forum? Kwa jina naitwa Shamsa,namtafuta baba yangu mzazi ambaye tulipotezana miaka 23 iliyopita sikuwahi bahatika kumfahamu wala kuikariri sure yake sababu aliondoka ningali bado mdogo sana.

Kwa taarifa nilizozipata juu juu baba huyo alikuwa akifahamika kwa jina la "Abbas Sendeu" ingawa bado sina uhakika sana kuhusiana na hilo jina la Sendeu ila kiasili alikuwa ni mtu kutoka Tanga japokuwa sikubahatika kujua kabila lake kabisa,, walikutana na mama yangu ambaye anaitwa Salama ambaye pia aliwahi kusoma chuo cha biashara cha Shinyanga na katika historia yao fupi waliwahi kuishi Mwanza na Arusha kabla ya kutengana na mama yangu kuhamia Dodoma ambapo ndio makazi yetu mpaka sasa.

Tafadhali! popote upatapo ujumbe huu naomba usiache kunitafuta baba yangu maana natamani kuijua true identity yangu....pia ombi langu kwa wanajamii forum, yoyote mwenye taarifa inayoweza kunisaidia kupatikana kwake na inayoshabiihana ama kurandana na majina au historia tajwa hapo naomba asisite kunifahamisha kwa namba zifuatazo...0754638458 na 0756289602.

Mwisho naomba kutoa angalizo au tahadhali naomba namba zilizo wekwa hapo juu zitumike kwa ajili ya matumizi yaliyotajwa hapo juu.
nakushauri jambo..
nenda ofisi za NIDA... kajieleze... labda utapata msaada maana kule wataweka taarifa zako katika system alaf wakusaidie kutafuta adress yake.. vizuri..

sina uhakika kama watakubali kutoa taarifa husika... ila wakikubali hiyo kazi ni ndogo sanaa
 
Back
Top Bottom