Msaada: Namna ya kufungua SACCOS

jaykiwele

JF-Expert Member
May 22, 2013
552
414
Habari Wakuu,
Kifupi mimi wafanyakazi wenzangu tuna umoja ambao tuliuanzisha haswa kwa lengo la kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kimaisha kama harusi, msiba na kujifungua mtoto.

Sasa tumekaa mda wa zaidi ya miezi sita tumekubaliana tupanue zaidi wigo wetu kwa kufungua miradi na kuweza kuwekeza katika shughuli nyingine sasa tunakwama kipato hivyo tunataka kufungua SACCOS ambayo itatuwezesha kupata mikopo ambayo itatwezesha kufungua miradi ili umoja wetu uweze kukua zaidi.

Hivyo nakaribisha maoni yenu wadau haswa kwa wale wenye uzoefu na weledi ya hatua gani tuzifuate na taratibu gani zinahusika na pia Kama kuna mawazo mazuri zaidi ya kuweza kuendesha kikundi chetu katika namna bora zaidi!
 
chakwanza naomba kujua misingi thabiti na idadi ya wana chama hai katika umoja wenu...nitajua namna ya kukuelekeza.pili kila kikundi cha umoja chena dhana ya kusaidia kutatua matatizo mbalimbali huwa kinakuwa na viongozi na kamati mbalimbali ya kutekeleza maazimio ya chama..wajumbe hawa huongozwa na taratibu maalum.. kama katiba.je katiba hii tayari mnayo?
kama katiba ipo ambayo ni msingi mkubwa wa utekelezaji shughuri zote za kikundi...ni yawazi kwawajumbe wote?(nikimaanisha nikatiba yenye maridhiano)hii husaidi kulinda umoja wenu ili isitokee mjumbe mwingine akahisi mnaongoza kienyeji.
unapo ona maoni haya machache yana reflect na mpango kazi wa umoja wenu. waweza kunitafuta kwa number 0755229028.kwataratibu zingine kwaajiri ya usajiri
mpaka kwa mrajisi vyama vya ushirika nk.
 
Mnatakiwa kwanza muuandae RASIMU ya Katiba ya SACCOS yenu,pamoja na vipengele vinavyoainishwa ktk Katiba za SACCOS ni pamoja na Jina LA SACCOS na Majina 9 ya Bodi ya Waanzilishi wa SACCOS,.Wakati JF tunaendelea kuvuta kumbukumbu nenda Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata yoyote ,muulizie Afisa Ushirika au Afisa Maendeleo ya Jamii ,azima Nakala ya any SACCOS au Fika Ofisi ya Halmashauri ,onana na Afisa Ushirika
 
Tupo wanachama 11 na katiba inayotuongoza ipo
 
Mnatakiwa kwanza muuandae RASIMU ya Katiba ya SACCOS yenu,pamoja na vipengele vinavyoainishwa ktk Katiba za SACCOS ni pamoja na Jina LA SACCOS na Majina 9 ya Bodi ya Waanzilishi wa SACCOS,.Wakati JF tunaendelea kuvuta kumbukumbu nenda Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata yoyote ,muulizie Afisa Ushirika au Afisa Maendeleo ya Jamii ,azima Nakala ya any SACCOS au Fika Ofisi ya Halmashauri ,onana na Afisa Ushirika
Asante kaka kwa ushauri wako naomba nijue vizuri kuhusu hayo majina 9 ya wanabodi yanatokana na wanachama au?
 
Aidha nimeangalia sasa hivi kwenye Mtandao hasa wa Internet, hii issue imefafanuliwa kwa kina, andika hivi KATIBA YA SACCOS TANZANIA, after that, lete mrejesho
 
Angalia mtandaoni kama vile Firefox,Chrome - Andika VICOBA / USAJILI WA SACCOS/USAJILI WA KAMPUNI
 
Asante kaka kwa ushauri wako naomba nijue vizuri kuhusu hayo majina 9 ya wanabodi yanatokana na wanachama au?

Mkiwa wanachama 11 au idadi yeyote chini ya 20 hamtakuwa na haki ya kuanzisha SACCOS bali mtaanzisha Pre-Cooperative group,mtapewa muda wa kuikuza kufikia sifa ya kuwa na SACCOS.

Kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya 2013 lazima muwe wanachama msiopungua 20,kuwe na uwezekano kukua kiuchumi.

Maelekezo sahihi mtafute Afisa Ushirika wa Wilaya/Manispaa au Jiji kulingana na mahali ulipo.Kikao cha kwanza cha kuanzisha rasmi SACCOS ni lazima Afisa Ushirika awepo.Maelezo ya hatua za kupita,kuchagua Bodi anzilishi,kuandaa masharti ya chama( katiba),na taratibu nyingine utaelekezwa na Afisa huyo.Yeyote aliyekuomba uwasiliane naye nje ya taratibu za kiofisi ninazokuelekeza anakudanganya.Hata mimi ninayekupa ushauri huu nikikuita nje ya taratibu nilizokueleza nitakuwa nakudanganya.Ni matakwa ya kisheria.

Hakuna gharama yeyote ya kukutana na Afisa Ushirika wa Wilaya uliyopo.Nawatakia mafanikio makubwa.
 
Asante sana
 
Back
Top Bottom