Msaada: Namna ya kuendesha duka vizuri

Msaada: Namna ya kuendesha duka vizuri

Baba Kapompo

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
1,344
Reaction score
468
HABARI ZENU WAKUU,

mimi ni kijana nnaye miliki hardware mtaan kwetu,ni miaka mitatu tangu nifungue biashara yangu .na niliwah kuisimamia biashara hii (yani kukaa mwenyewe golini kuuza na kufunga mahesabu)kwa muda wa miezi 8 tu kutokana ninasoma ilinibidi niajiri kijana kwa ajili ya kuuza na tangia mwishon wa mwaka 2011 hadi sasa nimeajiri sio chini ya vijana watatu yani kila mmoja nnamtimua kulingana na kosa/tabia zake ikafika wakati hadi mama yangu mzazi akawa anasimamia na biashara ilienda vizuri sana hadi nikatamani bimkubwa aendelee kutokana nae alinishikia tu kwa muda nhadi nipate kijana na yeye aendelee na shughuli zake ..ila sasa kijana nilie nae anakaribia miez 8 ila nimemuona kama kashaanza kuwa mjanjamjanja hivi.

Kiukweli japo nipo busy sana ila najitahidi kuwabana sana lakini mambo yanakuwa tofaut kama nikuza mwenyewe au bimkubwa inakuwa vizuri ile miezi ya kwanza kiasi kwamba nnasema hapa nimepata kijana nnamuamini mwishowe viswahili vinazid na kila nikikuta shot dukan kuna mawili eiza kukata kwenye mshahara au kuanza upya mahesabu(kama unavyo jua unapo lala mwenzio anaamka)

Ila tatizo langu kubwa lililo nileta hapa ni...nimeshajigundua kuwa utaratibu wangu ktk kuchukua takwimu ya vitu vya hardware ni mbovu(duka limesheheni vikorokoro vingi) inshort natumia mfumo wakuandika vifaa vyote vya dukani na idadi yake then nikija (may be after 3weeks) kuangalia mzunguko wa vifaa km vipo sahihi...na nimejaribu kufanya investigation kwenye hardwarebaadhi ya mtaani kwetu naona wengi wao wanauza/simamia wenyewe...wachache wapo kama mimi ila kilio ndio kilekile tena wengine zaid yangu..

NAOMBENI USHAURI MLIO WENGI MNATUMIA UTARATIBU GANI AU HATA KAMA UPO WAKIELECTRONIC/CMPTER NISAIDIEN KIMAWAZO...ILI KUEPUKA HII DHAhMA YA KUFUKUZA WATU KILA LEO NA KAMA KUNA NJIA MBADALA TUJUZANE TUU..maana hali imekuwa tete
 
Pole sana, kama unawanyanyasa wafanyakazi ni lazima na wao wa kutese so kama ni hivyo badilika
 
Pole sana.kama unawanyanyasa wafanyakazi ni lazima na wao wa kutese so kama ni hivyo badilika

Niajiri mm.pia cjui kaka cjui dada unatakiwa kuchukua mtu anayejua biashara na anayeweza kuogea na mteja vizuri sio wote wanawexa biashara mpenz so kuwa mwangalifu kwa hilo kuuza kipaji
 
Unaweza kazi alafu sory km huna uhakika na jinsia ya mtu jaribu kugeneralize maana nimejiskia vibaya (RED)
Ila km unaweza karibu fanya mawasiliano PM/ zuberiamiri@hotmail.com
 
Hongera sana na pia pole sana kama uko DAR nitafute nadhani kwa 75% shida zako za kibiashara zitapungua tunafanya biashara hiyo hiyo ya HARDWARE kwa zaidi ya miaka 20 sasa na tuna vijiduka zaidi ya 5, pia hatuna haja ya kuajiri ndg wala jamaa wala kabila, nadhani utajifunza sana kutoka kwenye mfumo wetu
 
Ndugu kupigwa haikwepeki,hata bakhresa anapigwa,tena sana tu,ilimradi wasikufilisi,angalia kama ni wachapakazi,ukigundua umepigwa Kata mshahara,usifukuze watu kazi hovyo.
 
Na ili wafanyakazi wako, Wasikuibie ni lazima uwalipe mshahara unaotosha,Sio unamlipa kijana wa watu elf 50 Alafu unankomalia kooni,Lazima wakukimbie na hapo ndio kipimo cha Ubinadam kinapoangaliwa kwa jicho la Ukaribu.
 
Na hata kama anamlipa 50,basi amgharamikie angalau chakuka na malazi.
 
wakuu kwa hili hamna shida kabisa maana ninawalipa vizuri na wanaish kwangu na chakula mbaya zaid hata sikukuu 60% nahusika mimi juu yao...ndio kinachonifanya niumie sana hadi nashindwa kukuza mtaji wangu naogopa nisije kucheza sandakarawe
 
wakuu!mm mwnyewe nimeajiriwa kwnye kaduka kaka m1 anauza cd na kukodi pamoja na huduma ya pesa kwa njia ya simu(mpesa}nilikuwa naomba mbinu ili niweze kusimamia vyema bila kuchanganya mahesabu.mbinu hizi zitaweza kumsaidia ata m~tz ili ampe huyo mfanyakazi wake mybe aelewi vyma mbinu za kusimamia vyema hyo hardware ya bosi wake
 
HABARI ZENU WAKUU,

mimi ni kijana nnaye miliki hardware mtaan kwetu,ni miaka mitatu tangu nifungue biashara yangu .na niliwah kuisimamia biashara hii (yani kukaa mwenyewe golini kuuza na kufunga mahesabu)kwa muda wa miezi 8 tu kutokana ninasoma ilinibidi niajiri kijana kwa ajili ya kuuza na tangia mwishon wa mwaka 2011 hadi sasa nimeajiri sio chini ya vijana watatu yani kila mmoja nnamtimua kulingana na kosa/tabia zake ikafika wakati hadi mama yangu mzazi akawa anasimamia na biashara ilienda vizuri sana hadi nikatamani bimkubwa aendelee kutokana nae alinishikia tu kwa muda nhadi nipate kijana na yeye aendelee na shughuli zake ..ila sasa kijana nilie nae anakaribia miez 8 ila nimemuona kama kashaanza kuwa mjanjamjanja hivi.

Kiukweli japo nipo busy sana ila najitahidi kuwabana sana lakini mambo yanakuwa tofaut kama nikuza mwenyewe au bimkubwa inakuwa vizuri ile miezi ya kwanza kiasi kwamba nnasema hapa nimepata kijana nnamuamini mwishowe viswahili vinazid na kila nikikuta shot dukan kuna mawili eiza kukata kwenye mshahara au kuanza upya mahesabu(kama unavyo jua unapo lala mwenzio anaamka)

Ila tatizo langu kubwa lililo nileta hapa ni...nimeshajigundua kuwa utaratibu wangu ktk kuchukua takwimu ya vitu vya hardware ni mbovu(duka limesheheni vikorokoro vingi) inshort natumia mfumo wakuandika vifaa vyote vya dukani na idadi yake then nikija (may be after 3weeks) kuangalia mzunguko wa vifaa km vipo sahihi...na nimejaribu kufanya investigation kwenye hardwarebaadhi ya mtaani kwetu naona wengi wao wanauza/simamia wenyewe...wachache wapo kama mimi ila kilio ndio kilekile tena wengine zaid yangu..

NAOMBENI USHAURI MLIO WENGI MNATUMIA UTARATIBU GANI AU HATA KAMA UPO WAKIELECTRONIC/CMPTER NISAIDIEN KIMAWAZO...ILI KUEPUKA HII DHAhMA YA KUFUKUZA WATU KILA LEO NA KAMA KUNA NJIA MBADALA TUJUZANE TUU..maana hali imekuwa tete
Hapo unaweza ukatumia computer software itakayokua na database kwa ajili ya kurekod bidhaa zilizopo,zilizouzwa(inarekod na mapato baada ya kuuzwa bidhaa hizo) pia inaonesha bidhaa zilizobaki.Faida ya software hiyo inakua na user accounts mbili ambazo ni ya wewe mmiliki kwa ajili ya kuangalizia mapato na pia akaunt ya muuzaj ambae anakua anarekod mauzo tu bila kujua kwamba ww utakuja kuangalia kilichouzwa na mapato yaliyopatikana,na mie natumia program hii ktk biashara zangu kwa kweli siibiwi.
Ukihitji program hii nambie nikupe namba za jamaa anaetengeneza.
 
Back
Top Bottom