Msaada: Nahitaji mtu wa kunifundisha gari

Kwa nini ulitie mtaroni? VETA si ulifanya mazoezi ya kuendesha? Na ukafanya mitihani kwa vitendo wa kuendesha, sheria unazijua? Jiamini na kuwa mwangalifu, kuwa wazi kwa mwajiri wako, kama ni kuanzia, uendeshe huko Masaki tu kwa kipindi fulani halafu taratibu unajichanganya maeneo yote.
 
Jiamin mkuu, kama gari ya huyo Boss wako ni Auto nafkiri itakuwa rahisi zaidi wala usijali
Nashukuru kwa kunipa moyo bro!
Ila gari yenyewe ni Manually shida ipo hapo.
 
Kwa nini ulitie mtaroni? VETA si ulifanya mazoezi ya kuendesha? Na ukafanya mitihani kwa vitendo wa kuendesha, sheria unazijua? Jiamini na kuwa mwangalifu, kuwa wazi kwa mwajiri wako, kama ni kuanzia, uendeshe huko Masaki tu kwa kipindi fulani halafu taratibu unajichanganya maeneo yote.
VETA nilifanya mazoezi na mtihani pia nimefanya ila unapokuja suala la control barabarani kwa aliyepitia hapo VETA ataniunga mkono,
Kwa sheria na alama za barabarani nipo vizuri sana tena sana, na ndio kipaumbele chuoni.
Pia ahsante kwa ushauri wako mzuri nitaufanyiakazi mungu akubariki
 
Aisee izi shule nyoko sana yaana unaweza soma na chet ukapewa sasa njoo chukua gari na uwe unandesha peke yako kama ni manually gia pekee utakayoenda nayo sawa ni kwanzia no4 na 5 na hizi kwenye folen hazina kazi hapo ndio unajikuta gar ikizima kila ukitaka kuondoka

Mb; mkuu kama huko veta mlijifunzia manual na ukaielewa kucontrol pako ndani ya akili yako kujiamin kwako ndio control yako na sio zaidi mengine utayajulia huko barabarani.

Kama boss wako gar lake ni out kwako itakua rahisi zaidi maana ni mwendo wa kuangalia mistar ya barabarani.
 
Kwa nini ulitie mtaroni? VETA si ulifanya mazoezi ya kuendesha? Na ukafanya mitihani kwa vitendo wa kuendesha, sheria unazijua? Jiamini na kuwa mwangalifu, kuwa wazi kwa mwajiri wako, kama ni kuanzia, uendeshe huko Masaki tu kwa kipindi fulani halafu taratibu unajichanganya maeneo yote.

Ndugu kuwa muelewa.. gari usipoendesha muda mrefu unaloose control.. ndio maana kazi za madereva zinataka experience.. yaani asome veta mwezi mmoja ajue kisha akae mwaka mzima bila kugusa gari.. halafu asikosee kweli?
 
Kama una muda uwe unaenda mitaa ya Bandarini kuanzia geti namba 5 muda ya saa 10 foleni ikianza.

Jichanganye uongee na wale madogo wa kuuza karanga/sigara uwa wanaachiwa kusogeza gari za trip town zenye container empty.

Kule utapata uzoefu mzuri wa manual maana madereva wenye Mishe zao huacha gari wasogezewe, utapata kujiamini kwa kuendesha manual vigongo za Madina 2001 na Motichand.
 
Mimi: Oooooh Mungu nisaidie niweze kula njaa inauma
Mungu:Malaika hakikisheni mimi anaishi ndani ya shamba la mahindi ili asije kufa njaa
Mimi: Ooooooh Mungu nisaidie niweze kula njaa inauma
 
Stori yangu ya mimi kujua gari ilikua hivi

Mwaka 2014 natoka zangu school (boarding) nakuta Wazee wamenunua gari RAUM hawakuniambia walisema walitaka iwe saprize basi mzee nikafurahi kwakua ndo ilikua Mara ya kwanza kwa familia yetu kumiliki ndinga ila mimi nilipoiona tuu gari nikawa nawaza kuendesha tuu nikaanza hadi kuangalia video za YouTube jinsi ya kuendesha gari.

Nikimuomba mzee ananiambia subili mpk umalize SIX ndo ntakufundisha nikasema hapa nisipokua mjanja wenzangu school wataendelea kunitambia tuu. Nikawa nasubil wakiondok naenda naliwasha kidg nazima baadae video za YouTube zikanisaidia jinsi ya kuitoa gari naanza naitoa hatua kadhaa alafu nailudisha. Sasa ikaja mother amesafiri ameenda zanzibar na mzee nae yupo mkoa home nipo mimi na madogo na sister wa kazi.

Nikapania Siku hiyo lazima niitoe nyumbani kweli nikaiwasha nikazunguka nayo sana mitaani Luna mjinga akampigia simu mother mother akanipigia mimi akanichimba mkwala mpk ikabidi nikimbie home niende kwa bibi. Siku niliyopewa ndinga ilikua harusi alafu mzee wangu ndo msimamizi yeye na bwana harusi wakaja home kuvaa na kujiandaa shida ikatokea hamna dereva wakuwapeleka kanisani Mzee akaniuliza si unajua kuendesha gari nikajibu kwa ujasiri kabis NDIO basi nikapewa funguo nakumbuka nilitetemeka kidg lakin nilijiamini na tangu siku hiyo nikaamini home nikaanza kupewa ndinga.

So brother jiamini usikubali kusema siwezi
 
Yaani kamanda gari la boss wa masaki hutaki kulitia mtaroni ila langu la kukufundishia unataka kulitia mtaroni
Kufundishwa unakuwa na mtu pembeni ambaye ni dereva kamili atakayekuelekeza na kukuongoza tofauti ukikaa na boss pembeni au peke yako.

Umenielewa hapo
 
Aisee izi shule nyoko sana yaana unaweza soma na chet ukapewa sasa njoo chukua gari na uwe unandesha peke yako kama ni manually gia pekee utakayoenda nayo sawa ni kwanzia no4 na 5 na hizi kwenye folen hazina kazi hapo ndio unajikuta gar ikizima kila ukitaka kuondoka

Mb; mkuu kama huko veta mlijifunzia manual na ukaielewa kucontrol pako ndani ya akili yako kujiamin kwako ndio control yako na sio zaidi mengine utayajulia huko barabarani.

Kama boss wako gar lake ni out kwako itakua rahisi zaidi maana ni mwendo wa kuangalia mistar ya barabarani.
Asnte kwa ushauri wako mkuu
 
Hayo ndo matatizo ya vyuo vyetu. Watu wanamiliki vyeti ila ukuzi hawana. Si veta tuu Hadi vyuo vikuu.
Mazoezi ya kuendesha gari veta ni madakika tuu halafu Mambo mengine yote ni theories tu.
Ni kweli kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom