Habari Wakuu,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 elimu yangu ni form IV natokea kwenye familia ya kimaskini iliyopo Kigamboni jijini Dar.
Kutokana na changamoto na ugumu wa maisha nikaamua kujiunga na kazi ya ulinzi (nimepitia kazi nyingi za msoto).
Hivyo kutokana na changamoto nikaona nisave kipato changu ili angalau niwe na fani yoyote, nashukuru mungu nilifanikiwa kusave nikaenda VETA kusomea udereva (basic driving course) na nikafanikiwa kupata cheti na leseni.
Sasa hapa lindoni kwangu ninapolinda (nalinda nyumba ya mtu binafsi masaki) huyu boss nimejaribu kumwelezea changamoto za maisha ninayopitia alichoniambia kama naweza kuendesha gari nimpelekee cheti na leseni yangu, hivyo vyote nnavyo tatizo sina experience/control hasa vurugu za barabarani naogopa kulitia mtaroni gari la watu nikapata lawama zaidi.
Mwenye nia na uwezo wa kunisaidia niweze kupata uzoefu naomba anisaidie.
Kuhusu pesa ya mafuta nitakuwa nachangia kadri jinsi tutakavyokubaliana.
Naombeni msaada wenu please.
Ahsanteni