MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

Jf ktk ubora wake. Ktk hali aliokuwa nayo jamaa hakukuwa na ulazima wa wadau kutoa kejeli kwake. Ilikuwa ima umpe pole au laah way forward! Technology inaruhusu sana kufanya online purchases, cha msingi kuzidisha umakini.
 
Pole mkuu mwenyewe nilitaka nifanye hio biashara na jamaa mmoja wa kupatana ila nimeghairi. Anatumia namba ya kikenya +234 ... ... ... Haeleweki yupo wapi exactly mara nyingine anapost toka Arusha, mara Kigoma, Mara Mwanza, Alinishtua kuomba advance ya laki ili atume mzigo kwa Dhl then malipo mengine yakamilike akifika. Mtu hataji ofisi anadai stores zipo Kenya.

Kakomalia nijaze order form yenye details then nimtumie laki ili wakave delivery charges na gharama kadhaa za kodi. Mwishowe nimempangusa tu maana ule mchezo anaotaka ucheza una harufu mbaya in the near future!
 
Jf ktk ubora wake. Ktk hali aliokuwa nayo jamaa hakukuwa na ulazima wa wadau kutoa kejeli kwake. Ilikuwa ima umpe pole au laah way forward! Technology inaruhusu sana kufanya online purchases, cha msingi kuzidisha umakini.
Haya,
Pole mdau,
 
Kupatana wenyewe WAMERECOMMEND NEVER PAY IN ADVANCE.. wewe ukaamua kinyume
Kupatana wenyewe WAMERECOMMEND NEVER PAY IN ADVANCE.. wewe ukaamua kinyume
 
Jf ktk ubora wake. Ktk hali aliokuwa nayo jamaa hakukuwa na ulazima wa wadau kutoa kejeli kwake. Ilikuwa ima umpe pole au laah way forward! Technology inaruhusu sana kufanya online purchases, cha msingi kuzidisha umakini.
Kweli kabisa mkuu, watu wanamkejeli na kumdhihaki kama vile wamemchangia hiyo hela, siyo vizuri kila anapitia mitihani tofauti, leo yeye kesho wewe
 
Awe mpole
Gharama ya kudeal na polisi itakuwa ni sawa na kununua mpyaa.

Kuna uzi kama huu umo humu wa kesi kama hiyo
Sasa wewe umekurupuka sana.

Tv yenyewe kwenye tangazo unaona kabisa Mtu ame google picha na amekuwekea,sasa wewe mpaka hapo hujaona tu kama unaibiwa?Unanua kitu usichokijua?

Mungu ambariki Tapeli,ili mlijue Jiji vizuri.

Haalfu ulivyo mzembe,badala ya kuweka mtego kirahisi tu hapo,wewe ungekuja Zanzibar then ukajifanya kama new Customer unataka kwenda kununua na una cash,badi hapo ungemnasa kiulainiiii

Yaani Malcom umejiunga JF tangu 2008?leo hii umekuwa wa DAR unaibiwa kizembe namna hiyo,aisee kweli Jiji halina Mwenyewe.

Mshkaji wangu sikupi Pole
 
Cha msingi anzisha uzi kwamba
USINUNUE BIDHAA YOYOTE KUTOKA ZANZIBAR
Hapo utakuwa umeziba soko lote na wauzaji watatafutana wao kwa wao
Maana hii imekuwa soko lote la Zanzibar

Maana bora hata ungeniambia mie nikufuatilie huyo mtu kabla ya kutuma pesa.Ungenilipa pesa ya mafuta ya gari tu.
 
Aisee ndugu pole yako.. Offer ilikuwa tempting kiasi kwamba mtu unashindwa kufikiri vizuri..
Sasa sababu unao ushahidi wa text.. Kama kweli unawahitaji hao watu.. Fika polisi.. Ripoti.. Utapata mpelelezi.. Kupitia mitandao ya simu na huyo mpelelezi utawapata..Sema hii kitu inahitaji Pesa pia..kwahiyo inaweza hela yako ikatumika tena ila ukajenga heshima kwa hao matapeli..

Nawasilisha..!
 
Mkuu na hapo hujamsaidia maana inawezekana hata huku zanzibar yenyewe hayuko, katumia tu hiyo location ili aaminike, usikute yupo hapo hapo dar
 
Duh mkuu mpaka sisi wakweli atuzibie, hiyo hapana asifanye atatuharibia na sisi waaminifu
Maana inawezekana huyo mtu hayupo hata hapa zanzibar, sasa kumwambia afanye hivo duh itakua kutuchafua sote. Wafanyabiashara hii huku wengi tunajuana, sijawahi kusikia hilo jina kwa kweli na laiti kama ningekua namjua ningempa ushirikiano wote akamkamata
 
Pole mno,
Ila kwa ushauri nenda polisi wape ushahidi & mkasa uliokutokea,
Naamini watakusaidia,
Ila usipende kununua bidhaa bila kuwa mwenyeji ambao ataupokea mzigo / bidhaa na kuhakikisha inafika hadi kwako.

Mimi huwa nanunua bidhaa kupitia website ya KIKUU.
ni wauzaji wa bidhaa original na imara kutoka ulaya, China, uarabuni.
Wanakuletea mpaka nyumbani na bei unapunguziwa.

Siku zote kuwa na mwenyeji unapotaka kununua & kuuza bidhaa ili iwe rahisi kufanikisha.
 
Duh mkuu mpaka sisi wakweli atuzibie, hiyo hapana asifanye atatuharibia na sisi waaminifu
Itabidi mbadilike,muweke Picha za Duka kwa nje,na mseme lipo wapi,ili iwe rahisi kupatikana.
Na at least kuwa na reference ya angalau mtu mmoja humu JF alienunua bidhaa kutoka kwao ili kujenga imani.

Na pia watu wote wa Zanzibar tuna Ndugu DAR,na ikiwezekana basi pesa zilipwe DAR kwa ndugu zenu huku,tena lazima iwe sehem yenye kufahamika sio kukutana Congo kitaa,na kutupia picha hapo hapoa ya pamoja.

Maana inabidi sasa tuwe tunauziana kama vile Magaidi wa bidhaa.

Zanzibar ina sifa kubwa sana ya uaminifu,sasa mjinga mmoja huyo kaja kuvuruga kila kitu.Kuna watu wamewahi kuja Zanzibar mara mbili tu kununua Magari baada ya hapo wanatuma pesa tu hata 20m bila hofu na mtu gari zake zinamfikia Dar.

Kwanza naanza na Abdul hembu niambie Duka lako lipo wapi kwanza nije hapo live
 
Duh!! Huu ubwege mkuu unamuamin mtu vip kumtumia hela wakati humjui.. Mie kila siku naona matangazo km hayo huwa nasema moyoni "mtampata bwege gani wa kumtapeli kiboya hvyo kwa karne hii" sasa cha kushangaza ni kuona kila siku matangazo yanaibuka means wanafanikiwa, nikawa siamin kumbe kweli bhana wazembe wapo ndio nimeamin sasa

Anyway pole mkuu.. Sikukashifu, niwie radhi kama utakuwa umenielewa vibaya.
 
Mkuu mi nipo mtendeni kwa msonga halua kama upo zenji njoo mda wowote kuanzia saa 3 asubuhi ha saa 1 jioni, kuhusu kuyuma mzigo dar na kulipia huko ndivo ninavofanya kwa walio na shaka na mimi, ama refrence ya niliofanya nao biashara ni wengi sana sema wakisha pata mizigo yao wanaishia kunishukuru mimi tu hua hawaleti mrejesho humu kama nimeupata, wanasubiri watapeliwe ndo hua wepesi wa kuja kutoa mrejesho, 0718919725 $ 0777650286 njoo nipo utanikuta
 
Asante Mkuu
Mitaa hiyo naijua vizuri,na nimekuamini,maana kwa Zantel ya 0777,kwa sie wa Zanzibar basi ni mtu dhamana,hilo tu linatosha.

Na mfumo unaotomia ni mzuri sana.
Basia cha kazi iendelee,maana alietapeliwa katapeliwa kizembe saaana,maana hata picha kwenye post ya tangazo haikuwa halisi.
Rest in Pain Malcom mtapeliwa

Abdul,hembu niambie mpaka kuutoa mzigo Dar unagharimu ziada kiasi gani?yaani mtu anauchukau nje ya bandari Dar,yeye ni kuweka kwenye gari tu,hapo extra inakuwa kiasi gani?
Maana nilikuwa naifikiria hii biashara kwa kufanya kwa Jumla kupeleka Mwanza
 
Mkuu shukran kwanza kwa kunielewa, ama kuhusu kusafirisha mpaka kuutoa nje mi hua kama tv 32" nampa baharia 35000, 40" 40000 na 43" 50000 na 48" mpaka 55" hua nampa 65000 mpaka 70000, hapo anakutolea mpaka nje
 

 
Wewe wacha uduwanz usinipake matope. Pc nimekuuzia kabla ya kutoa hela umeichek zaid ya lisaa , umeridhika nayo tena nikakueleza nauza pc sababu kadha wa kadha, ukaielewa, matatzo madogo madogo nakumbuka nilikuambia kabisa haika na chaji muda mref.. Vingine vyote safi.. Umenipa mpunga wangu, nmeondoka baada ya wiki mbili ndio unaniambia pc sijui spika mbiv sijui takataka gani, ingekuwa wewe ungekubali ningetaka kukutapeli ningekwambia njoo nyumbani tufanye biashara ili likitokea lolote uje mpaka home ukagoma ukasema tukutane eneo...

Niuzie mimi kwa hyo laki moja basi, ongea maneno kuendana na umri wako sio unaropoka tuu..[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ulikuwa makini sana...lakini mimi na ubwege wangu nilikuamini kwa asilimia zote..hata uliponiambia nikague mzigo niliupitia juu juu tu nikakurushia pesa nikasepa...
Yaliyonikuta ndio hivyo tena nashindwa kujua nitairudishaje ile pesa niliyobebea zege kwa miezi nane...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…