kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,815
Habarini,ngoja niende kwenye mada moja kwa moja.
Mimi nina miaka katikati ya 25 na 30,katika pitapita nikakutana na dada wa miaka 34 na ana mtoto mmoja tukawa tu marafiki,mimi nimepitia mambo mengi ya kimaisha katika umri wangu huo mdogo so nina mambo mengi kichwani na ni mzuri sana wa kushauri na kutoa mawazo saidizi kwa watu wenye matatizo mbalimbali na nategemewa na wengi kwa hilo kwa wote vijana wa kiume na wa kike.
Baada ya kuzoeana na huyu dada alinisimulia matatizo mengi aliyopitia katika maisha yake,nilikuwa nakaa naye na kumshauri na kwa kweli ushauri wangu ulimpa nguvu na ari ya kwenda mbele,akaniona mimi ni kama kila kitu kwake kitu chochote ambacho alipanga kufanya ni lazima tu angenishirikisha na ushauri wangu ndo unatoa either afanye au asifanye.
Ikafiia wakati kuna binti ilivutiwa naye na yule dada kama mtu wangu wa karibu nikamshirikisha,daah aliumia sana, akaniambia maneno yaliyonishangaza kidogo,akaanza kusema sijui ana balaa gani kila mwanaume anayempata anamuacha,nikabaki nimeduwaa nikamuuliza kwani mimi ni mpenzi wako?? Aliniudhi kwa tabia ile ya kitoto,nikamwambia nop na umeniudhi sana,akaniomba msamaha pale na bahati mbaya kumbe yule binti niliyempenda alikuwa na mtu wake huko kwao so nikasitisha zoezi la kumfuata,yule dada alifurahi sana kusikia hivyo.
Maisha yakaendelea kuna kosa nililifanya baada ya kukaa naye kama miezi saba hivi na huyu dada kama marafiki tu nikaanza kutoka naye sehemu mbalimbali hatimaye siku moja nikajikuta nipo naye sehemu sio salama usiku nikafanya naye mapenzi.. Hili ni moja kati ya kosa kubwa sana ambalo mtu makini kama mimi nimewahi kulifanya,dada wa watu ameniganda hatari sana nikimwambia habari za kuvunja huu uhusiano usio rasmi analalamika sana,anatuma meseji ambazo kwa mwanaume yeyote lazima zikuume na ufikiri mara mbili.
Hadi sasa nimefanya jaribio la kuvunja uhusiano kama mara tatu hivi imeshindikana,kikubwa ni kuwa sitaki alie,huwa sipendi kumuona binti akilia huwa nawaonea huruma sana,pale binti anavyolia na kutuma meseji za kuhudhunika huwa nashindwa kabisa kuwa na amani,katika maisha yangu huwa mara zote nawafuta machozi mabinti walioumizwa safari hii inataka ionekane mimi ndo nawatoa machozi yaan hata sielewi nafanyeje, wapendwa nimeamua nililete hili hapa ili nipate mawazo yenu nifanyeje katika hili...