Msaada. Nachanika mwili bila sababu, nini Shida?

Msaada. Nachanika mwili bila sababu, nini Shida?

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2019
Posts
490
Reaction score
1,024
Habari: Wahenga wanasema mficha maradhi kifo humuumbua, hivyo sina budi kuweka wazi tatizo linalonisumbua kwa muda mrefu.

Nimekuwa nachanika mwili mithili ya mtu alonichana na kiwembe kwa ncha ya juu akikwaruza kwa mbaali au mithili ya mtu alokwaruzwa na miba ya miti au nyasi.
Hali hii ninayo zaidi ya miaka 10 sasa mana imeanza bado nipo school (A level )sema kuna kipindi inanitokea Mara kwa Mara na kuna kipindi inapotea.

Mara nyingi hunitokea nikiwa usingizini, huanza kama muwasho kwa mbaali kisha unaongezeka na kwa muda sehem inayowasha huleta alama ya mkwaruzo. Nimejaribu kufatilia kuna walonambia ni ugonjwa wa Ngozi, kuna wanaohisi ni mashetani na wengine husema labda niminyoo japo Mara nyingi nikipima minyoo huwa haionekani japo naskia dalili zote kama tumbo kuunguruma nk.

Nimeamua kulileta humu nikiamini kuna wataalamu wa kada tofauti ikiwemo Afya, tiba asili na Wataalamu wa Imani (dini).

Naomba kuambiwa hii hali inaitwaje na inasababishwa na nini hasa na nini suluhisho.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee Umeeleza vyema mkuu
.
Kama ni tatizo la ngozi kwann litokee ukiwa Mkubwa hivyo?
Na linatokea sehemu gani hasa za Mwili?
 
Aisee Umeeleza vyema mkuu
.
Kama ni tatizo la ngozi kwann litokee ukiwa Mkubwa hivyo ?
Na linatokea sehemu gani hasa za Mwili ?
@Next Man kwani tatizo la ngozi huwapata wadogo tu?

Sent from my SM-N9500 using Tapatalk
 
Aisee Umeeleza vyema mkuu
.
Kama ni tatizo la ngozi kwann litokee ukiwa Mkubwa hivyo ?
Na linatokea sehemu gani hasa za Mwili ?
Ni sehemu yoyote inategemeana na vipindi. Kuna kipindi inafululiza mikononi, kuna kipindi inatokea zaidi tumboni, mara mapajani na kwa wakati huu inanichana miguuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom