Buza Kwa Mpalange
JF-Expert Member
- Apr 15, 2020
- 268
- 156
Habari za muda huu wana JF.
Mimi sio mgeni humu, nilishakua guest humu kwa miaka 7 mpaka nimechukua maamuzi ya kuwa mwanachama rasmi.
Poleni na mapambano dhidi ya COVID-19. Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada.
Mimi ni kijana wa miaka 23 naishi Dar. Tangu nimalize kidato cha 4 mwaka 2014 .mpaka leo nipo tu
Sina ili wala lile niponipo tu kama msulule. Yaani hapa nilipo nakaa kwa kakaangu. Yaani ni mwendo wa kula na kulala tangu 2016 mpaka leo nipo hapa.
Yaani hata nikiwa naongea na watu nahisi kama wananiona naongea pumba. Muda mwingi natumia kukaa tu chumbani kama mhalifu wa kivita anayesubiria mashataka ya ICC. Yaani najisikia vibaya.
Hata marafiki ninao wachache. Yaani nikipata muda wa kutembea naamua kuzurura kwenye vitongoji vya mbali ili kupotea muda tu. Au naenda mpirani kuangalia watu wanavyofanya mazoezi muda ukiisha narudi home. Home ni kama lockdown vile ilifika saa 3 upo ndani.
Nimejaribu kutafuta kazi lakini nimekosa, nimetafuta connection ili nipate kazi na cheti changi cha kidato cha 4 lakini nimekosa. Kuna muda nilisoma kozi ya ICT lakini niliishia nusu semista tu. Semista ya 2 nilikosa ada nikaanza kusota home mara nideki mara nifue nguo za madogo.
Naombeni ushauri wenu.
Mimi si muamdikaji mzuri