Msaada na Ushauri: Nini hatma ya maisha yangu?

Buza Kwa Mpalange

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
268
156
Habari za muda huu wana JF.

Mimi sio mgeni humu, nilishakua guest humu kwa miaka 7 mpaka nimechukua maamuzi ya kuwa mwanachama rasmi.

Poleni na mapambano dhidi ya COVID-19. Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni kijana wa miaka 23 naishi Dar. Tangu nimalize kidato cha 4 mwaka 2014 .mpaka leo nipo tu
Sina ili wala lile niponipo tu kama msulule. Yaani hapa nilipo nakaa kwa kakaangu. Yaani ni mwendo wa kula na kulala tangu 2016 mpaka leo nipo hapa.

Yaani hata nikiwa naongea na watu nahisi kama wananiona naongea pumba. Muda mwingi natumia kukaa tu chumbani kama mhalifu wa kivita anayesubiria mashataka ya ICC. Yaani najisikia vibaya.

Hata marafiki ninao wachache. Yaani nikipata muda wa kutembea naamua kuzurura kwenye vitongoji vya mbali ili kupotea muda tu. Au naenda mpirani kuangalia watu wanavyofanya mazoezi muda ukiisha narudi home. Home ni kama lockdown vile ilifika saa 3 upo ndani.

Nimejaribu kutafuta kazi lakini nimekosa, nimetafuta connection ili nipate kazi na cheti changi cha kidato cha 4 lakini nimekosa. Kuna muda nilisoma kozi ya ICT lakini niliishia nusu semista tu. Semista ya 2 nilikosa ada nikaanza kusota home mara nideki mara nifue nguo za madogo.

Naombeni ushauri wenu.

Mimi si muamdikaji mzuri
 
Pole sana mkuu.
Ngoja wengine waje walau watakuwa na connection
 
Hatma ya maisha yako wewe unatuuliza sisi? Au nyie ndo wale mliokulia kwenye familia za mboga saba ugali kitenesi.. na baadae mambo yamebadilika kila kitu mnaona kama vile mungu anawaonea! Kwani wewe ni mlemavu? Tuanzie hapo kwanza!
 
kama unaenda kutafuta kazi ukiwa umeweka mkanda nje yaani umechomekea usitegemee kupata kibarua maana kazi nyingi ni zile za suruba na watu wanaishi tu kwa kazi hizo! Kama unaweza kulisha ng'ombe wa maziwa kwa sh. 150,000/ kwa mwezi huku unakula na kulala kwa bosi nitafute nitakuunganisha na jamaa yangu....na kama utakuwa na malengo mwaka mmoja unakuwa tayari na mtaji wako wa kuuza chai na maandazi ya kutembeza au hata kijiwe cha kahawa na kashata.
 
Pole sana usichague kazi. Usione aibu Hapohapo mtaani uliza kama kuna mtu anataka mtu wa kufua nguo ufue kazi za kibarua au mtu wa kupigiwa pasi. Hata ikibisi umenye viazi kwa wauza chipsi.usikae ndani tu utazidi kuwa mtu wa mawazo.Siku hizi na kipindi hiki kazi ngumu.
 
Jitahidi utafute hata sh 40,000 ufanye biashara ndogondogo kati ya hizi

1. Tafuta jiko la kuchomea mahindi sh 20,000. Nunua mahindi ya sh 10,000 na mkaa wa sh 3,000 tafuta sehemu ya barabara uanze kuchoma mahindi

AU

Fungua kagenge ka matunda mfano kama vile ndizi, machungwa, n.k

Tafuta mafundi ujenzi uombe uwe kibarua. usichague kazi. Usikate tamaa.
 
Hee! Jinsi nilivyoona unachagua kazi! Hapo lazima uone ugumu!
Ila mradi umetambua udhaifu wako si mbaya!...i wish vijana mjitoe kwenye mizones mlozoea kama analyse!..
Alafu una bahatu kubwa moja!HUNA FAMILIA INAYOKUTEGEMEA WOGA WA NINI?.Toka hapo ulipo mapema sana!

Laiti ningekuwa men na sina familia🤔🤔🤔!
 
Pole sana, maisha ya dar ni magumu sana, wengi wenye biashara ndogondogo wanaishia kupata pesa ya kula, huwezi kusave pesa. Kama una ndugu kwenye mikoa mikubwa ukiondoa Dar, nenda ongea nae mpe wazo lako la kufanya biashara ndogo ndogo labda, baada ya miezi 3 utakuwa kwako. Gharama za maisha huko zitakuwa ndogo na kidogo kidogo utafanikiwa kama ukiwa na nidhamu ya pesa.
 
Dar ugumu zaidi mie nauona kama ni sehemu ya kulala aisee!
 
Dar ugumu zaidi mie nauona kama ni sehemu ya kulala aisee!
Nikweli. Dar kila kitu ni pesa hadi maji ya kunywa. Pia Dar hakuna biashara mpya, so ndani ya eneo moja ujasiriamali wa hapo, utaukuta ni huohuo ukipiga hatua za mita 100 mbele. Kwamaana hiyo wanagawana kipato na kila mtu anapata pesa ya kumwezesha kufika kesho. Labda wale wanaouza kwa jumla kama wanaomwaga matunda( water melon, mihogo n.k)
 
Umesema kweli...kuna.siku nilipatwa hamu ya pilau nilotafuta hotel zote hakuna..
Kuna mikoa mambo.mengine hayajafika
 
Mimi si muamdikaji mzuri
Ha ha ha haaaa, dogo mbona una kipaji cha kuandika riwaya? Nimecheka sana jinsi unavyohadithia! Ungemtafuta Shigongo labda anaweza kukupa deal la uandishi wa riwaya! Shida yenu vijana mkimaliza shule mnakimbilia mjini kwa kaka zenu au shemeji zenu badala ya kukaa vijijini mkapiga kazi za shamba! Shamba mbona kwa mtu mwenye elimu linamtoa tu hila shida kabisa na huko pia kuna fursa za kuwa mwenyekiti wa kijiji au baadaye diwani kabisa! Toka mjini dogo urudi kijijini kwenu!
 
Hatma ya maisha sio kupata kazi lakini.....Pambana kijana hakuna aijuae kesho
 
Back
Top Bottom