Msaada: Mwenye kuijua hii mashine ya photocopy

Msaada: Mwenye kuijua hii mashine ya photocopy

PistolGang

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
392
Reaction score
44
Habari zenu wadau?
Kuna mashine ya kutolea copy inaitwa OLIVETTI COPIA 8020.
Please mwenye kujua sifa, tabia, faida na hasara ya hii mashine anijuze tafadhali.
Nataka kuuziwa hii mashine kwa kuanzia biashara locally kipindi najipanga for new mashine.
 
Mkuu kama mpya ina warranty unaweza kununua, lakini kama kuanzia tafuta canon ndio machine zenye kuzijua hapa bongo, ngumu na zina mafundi pia ikisumbua
 
Cardinal Rules za Biashara inayotumia Consumables....

  • Always nunua mashine ambayo ni common katika mazingira yako.. (hii itapelekea kupata spare na mafundi kwa urahisi na bei nzuri
  • Kabla ya kununua mashine angalia na compare bei ya vifaa na mashine nyingine (sababu utakuwa unabadilisha vitu kama OPC, Blade, Wino n.k.) mara kwa mara
Kwa Tanzania mashine common ni CANON; Kenya ni Kyocera na Ricoh/Nashuatec, UK ni Ricoh, kwahio kwa Bongo unaweza ukapata mashine kama Toshiba ukashangaa baada ya consumbles kuisha inabaki kuwa pambo au kununua vifaa mpaka uende kwenye duka moja tu Tanzania nzima au ukiita fundi anajifunzia kwenye mashine yako..

Cha maana muulize anayekuuzia spear / consumbles huwa anazinunua wapi na kwa bei gani na zinadumu muda gani alafu compare na CANON ambayo ni be it end all ya Copier Tanzania
 
Back
Top Bottom