Kwanza mkuu nikupe pole sana kwa maswahibu ya mwanao kubakwa. Japo nimechelewa kucomment lakini hope itakusaidia next time when u experience the same attack. Kwanza Dr wa zahanati yupo sahihi kwa upande wake akitaka kutokupoteza forensic evidence yaani ushahidi wa kimazingira wa tukio hilo, lakini kiafya sio nzuri.
Kwahiyo kama mtu huwezi kumhudumia ni bora umweleze aende sehemu nyingne taratibu za kimsingi kwa mtu aliyebakwa inapaswa apimwe ujauzito yaani UPT kuthibitisha kwanza hakuwa mjamzito wakati anaingiliwa ili apatiwe dawa za kuzuia kutunga ujauzito, zipo nyingi effectiveness yake ni within 72 hours mfano emergency contraceptive pills.
Pili, anatakiwa afanyiwe kipimo cha maambukizi ya UKIMWI yaani SD bioline kama akiwa negative ili apewe dawa za kumkinga na maambukizi yaan post exposure prophylaxis yaan PEP kwa maana status ya mtu aliyemuingilia haijulikani. Pia, afanyiwe vipimo vingine vya maradhi ya ngono yaani STI's kama atabainika hana apewe prophylactic antibiotics kumkinga. Hivyo, si busara kumwacha mpaka kesho kwa justification ya forensic medicine pekee japo ni muhimu when it comes to legal issues.
I stand to be corrected
Mihayo DP