Msaada: Mtoto wangu ananikimbia

Msaada: Mtoto wangu ananikimbia

WISE BOY

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2011
Posts
782
Reaction score
244
Salaaam wana jamvi!!!
Kuna siku mtoto alikua analia usiku, alilia kwa muda mpaka usiku sana, baada ya kubembelezwa bila mafanikio mm nikambeba nikamchapa kidogo miguuni (chapa ya kitoto) akanyamaza baada ya muda mfupi na akalala.
Sasa tangu sku hyo mtoto akiniona anakimbia na kuanza kulia, hata kama alikua anacheza anaacha kabisa, hii kitu inaninyima amani sana.
Naombeni msaada wenu ktk hili, ni vp naweza kabiliana na hii hali?
Mtoto ana umri wa mwaka 1 na nusu
 
Kwa kuguess wewe ni baba ya mtoto na si mama ya mtoto; La kujaribu ni kumpenda na kuonyesha hiyo unaweza mletea zawadi nzuri mfululizo ili ajenge imani ya kuwa wewe si mtu mbaya kwake vinginevyo anaweza kukua akikuogopa mpaka ukubwani.
 
Bado ni mdogo mno. Mpe muda ataondoa hofu. Ni kawaida isitoshe pale mtoto anapokuwa hakuoni mara kwa mara
 
Kama hajasahau akiwa mtoto basi sahau atakukubali akiwa mkubwa
 
Mh aisee kwamza nahisi hata kabla hujamchapa hukua karibu na mtoto kama baba, kwa hiyo ulipomchapa ndio ukampoteza kabisa. Jitahidi kuwa jirani naye mwonyeshe upendo mpe hug la mda mrefu, piga naye story kwa upendo hata kama hajui kuongea yeye anaelewa.
 
ukimzoesha zawadi utamuharibu...dont worry in time atakua normal. otherwise usijeogopa kumdescipline mwanao eti kisa unaogopa atakuchunia.
be careful, kids are too tricky.
 
Dogo ni mwerevu huyo. Keshajua wewe unamsababishia adha. Sasa kwa nini asikuepuke?

What you need to do is make it up to him. Re-assure him that you are not out to hurt him.

Perhaps you may want to change the way you discipline him.

But right now work on assuring him that you are not a bogeyman out to hurt him like you probably did when you flicked him.

Mind you, hurt doesn't necessarily have to be physical. Feelings can get hurt too and maybe his were hurt also.

Kids are very smart. They may just not know or not have the ability to verbally communicate their thoughts but they know it when you are being nice or mean to them and your mini-me is no exception.
 
anza na zawadi na uwe na muda nae tena uwe unacheka nae sana ili aitoe hiyo perception kichwani kwamba dingi gaidi.
 
Asanteni sana kwa mawazo yenu wandugu
 
Ukitaka kuwa rafiki na mtoto basi unatakiwa na wewe ufanye mambo ya kitoto kama vile kucheza nae michezo mbalimbali ambayo itamfanya arudishe imani na kukuchukulia kama rafiki yake.
Kumletea zawadi za hapa na pale pamoja na kuwa na tabasamu muda wote ukiwa karibu nae hivyo kumfanya mtoto akuone ni mtu mzuri.

Sio baba unarudi nyumbani umekunja sura kam nyama ya GOTI mpaka mtoto anaanza kukutilia mashaka.
 
Hahaaa, hilo ninazingatia sana, thanx
 
Bibie King'asti azidi kumchapa si huyo mtoto atazidi kumuogopa?kwa kitendo cha kumpiga mtoto wa mwaka Mmoja na nusu kinaonyesha huyu Mtoto sio baba wake samahani kama nitaku kwaza Mkuu.@WISE BOY wewe ni kweli huyo ni mwanao wa kumzaa?

Ni mtoto wangu wa kuzaa. Sikumchapa kihivyo kama unavyodhani mkuu, ni ile chapa ya kitoto tu kama anavyochapwa mtoto anaekataa kunywa uji
 
Ni mtoto wangu wa kuzaa. Sikumchapa kihivyo kama unavyodhani mkuu, ni ile chapa ya kitoto tu kama anavyochapwa mtoto anaekataa kunywa uji
Mkuu WISE BOY Pamoja na hivyo Sheria haikurusu umchape mtoto tena wa mwaka 1 na nusu umevunja sheria kama ni ulaya nilipo mimi huku unakwenda jela na mtoto

anachukuliwa na Serikali inaonyesha wewe huwezi kumlea mtoto una bahati upo Tanzania hakuna sheria huko. Kama ungelikuwa upo huku na mimi ni jirani yako ninawaambia Polisi wanakuja kukukamata na unakwenda jela na mtoto

anachukulia na Serikali usirudie tena kumpiga mtoto unaona sasa mtoto anakuogopa wewe?Mtoto wako mwenyewe anakuona wewe kama kwake ni aduwi mkubwa kwa sababu ulimpiga ili alale usingizi.Mtoto kwa kawaida ana michezo 40 kwa siku hiyo kutotaka

kulala ni moja ya michezo yake wewe umempiga ili alale umetumia njia ya Ku-Force ili alale usingizi? Ndio maana anakuogopa jipendekeze kwake akupende asikuone tena aduwi wake pole sana.
 
itakuwa kamati ya ufundi(wachawi) wamejgeuza na kufanana na ww na mtoto kila akikuona anakuogopa! Sali ili uweze kukabliana na hlo janga
 
Kuna kanuni moja nilijifunza kwenye kitabu cha The Art of War by Sun Tzu na ni effective balaa:
" If soldiers are punished before they have grown attached to you, they will not prove submissive; and, unless submissive, they will be practically useless. If, when soldiers have become attached to you, punishments are not enforced, they will be still useless"

Substitute neno soldiers with children.

Summary kwa case yako ni kuwa: mwonyeshe mtoto wako kuwa unampenda na yeye akajua baba ananipenda kwanza ndipo uje kum-discipline akikosea. Zingatia utaratibu huu mtoto atakupenda na bado atakuwa na adabu.
 
mtoto anahisi wewe si baba yake mzazi kwa hiyo anakuona kama stranger vile!!!! mnunulie zawadi zawadi like toys, vigari, nk. kutegemeana na jinsia ya mwanao. cheza nae na ujifanye like cartoon...akushangae..akucheke hadi hofu imtoke, naye aanze kucheza nawe!
 
Back
Top Bottom