Msaada: Mtoto wangu ana hasira sana

Msaada: Mtoto wangu ana hasira sana

Unataka kusema wamakonde na wanaojitia tatoo wanafanya abuse?
Kama ni wewe katika hiyo avatar, jaribu kuweka chale uone utakavyozidi kuwa mrembo.

.....wamakonde ni utamaduni wao, na tattoo ni hiyari kwa mtu mzima kujiweka.
Lakini iwapo utamuweka mtoto sababu ya kosa au ukorofi wake,sasa hiyo itakuwa abuse sababu mtoto hajaweka kwa hiyari yake.
 
.....wamakonde ni utamaduni wao, na tattoo ni hiyari kwa mtu mzima kujiweka.
Lakini iwapo utamuweka mtoto sababu ya kosa au ukorofi wake,sasa hiyo itakuwa abuse sababu mtoto hajaweka kwa hiyari yake.
Wewe hutaki kuweka chale usoni uongeze urembo na uzuri dada?
 
........Je wewe ni mtaalam wa kuweka watu chale? Kama wewe utaniweka kwa utaalam poa.
Nitakupatia mtaalam wa kuweka chale...Nikikuweka mimi huenda ukasema naku-abuse. :biggrin:
 
usimdekeze sana mkuu mpe adhabu kali akikosea
 
Nafikiri baada ya kujua kuongea na kusema anachotaka ataacha..... pia akifanya hivo jaribu kumfinya kdg.

Swala dogo hilo. Mpe adhabu kulingana umri wake kila anapokua ameharibu kitu kwa hasira zake na isiwe Mara kwa mara inatakiwa iwe Mara chache uwezavyo ataacha.

nitonye

Kama baba yake mtoto ni mkurya kazi ipo.Ni kopi ya mura hiyo.

Hasira ni kitu cha kawaida.Ila kama anaanza kuvunja vitu (destructive anger) hapo inabidi uanze kumdhibiti mapema kwa kumwonyesha umechukia na kumvuta aisifanye kile atakach😵f course atalia sana ukimvuta na kumzuia anachotaka kufanya lakini baadaye akivutwa vutwa mara nyingi ataacha.usimpe nafasi ya kutekeleza azima yake akiendelea hivyo atakuja haribika mno mbeleni.

Ila akikua kidogo ni vizuri kuanza kumchapa kidogo kidogo anapokosea ili ajue kila kosa lina adhabu.Ataacha hivyo vi hasira koko vyake na akikua ataogopa kulipuka hasira mno akijua kuwa atashughulikiwa kama mzazi ulivyokuwa ukimshughulia.Usipomshughulikia atakua akijiona yeye mfalme anayeweza fanya chochote na asifanywe chochote.Ndio maana adhabu muhimu hasa kwa mtoto anapokuwa mdogo anapokosea.

Kakiharibu we karushe mitama tu kataacha kenyewe.

Ulaya mtoto hapigwi!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wana-Jamvi,

Mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi nane lakini anakabiliwa na tatizo la kuwa na hasira hasa pale anapoona amecheleweshewa kupewa kitu mfano kama uji au juice.

Unaweza kumpa juice ikiisha anakitupa kikombe au chupa au anaenda kwenye kabati anatoa kikombe anakipasua basi roho yake inakuwa imetulia. Sasa jambo hili linanipa wasiwasi endapo ataendelea kuwa na hasira za namna hii.

Kama kuna tiba yoyote naombeni msaada.

Fimbo... Fimbo ndio dawa

MIT. 13:24 SUV

Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

MIT. 22:15 SUV

Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

MIT. 23:13 SUV

Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
 
Swala dogo hilo. Mpe adhabu kulingana umri wake kila anapokua ameharibu kitu kwa hasira zake na isiwe Mara kwa mara inatakiwa iwe Mara chache uwezavyo ataacha.

Mtoto hata miaka miwili hana kumpa adhabu YOYOTE ni kumuonea tu. Jaribu kuongea nao hapo Nyumbani waisome ratiba yake na wamsome na yeye pia.

Ninae wa hivyo, ye ana nwaka mmoja tu lakini home wanachezeaga sana vibao vyake wakimletea ujinga. Wanajitahidi kutokumuuzi lakini ukimsema vibaya tu ni kama vile anasikia, soon utakula vibao vyake.

Ana kajitundu kwenye sikio na nimeambiwa ndio sababu nami nimeamini hivyo.
 
......mimi huyu wangu naye ni hasira na ubishi. Mtoto yupo 4 yrs lakini anafanya vitu kama mkubwa.

Alivyokuwa na 2 yrs ukimuudhi au akitaka kitu apate muda huo huo, otherwise anajiangusha.......nikaanza kumpa viadhabu akaacha.

Sasa tokea miaka 3 hadi sasa 4 kaanzisha tabia ya kurusha vitu na kubamiza milango, yaani ukimuudhi lazima atafute kitu cha kuharibu kwa kurusha au kubamiza milango.

.....nimeanza kumstua kwa kumchapa sometimes, basi ukimchapa atakwambia stop hitting me! Namwambia nakuchapa kwa sababu umefanya hivi, ni kosa.

Wiki 2 hizi naona kama ameanza kustop kurusha vitu, ila milango anabamiza na kanasema leave me alone. Hii bado nafanyia kazi.

Usione watu tumekuwa, kumbe wazazi walifanya kazi sana kulea. Kulea mtoto ni another full-time job, unatakiwa ufanye kwa hekima kweli.

Hahahaaa haaaaaa, Wazazi wetu wana kazi sana! Nimepata hiyo picha anaposema live me alone!! Halafu anabamiza mlango nimecheka sana.
 
Wazazi huwa tunajisahau sana kwenye jambo muhimu sana la kuwaombea watoto wetu. Tunatumia nguvu na akili zetu sisi wenyewe kuwa-raise up wanetu bila kumshirikisha Mungu. Pamoja na viadhabu vidogovidogo, lazima tumshirikishe Mungu awasaidie wanetu wakue, wawe na hekima, busara, akili waweze kusamehe kuishinda hasira, wawe na upendo, watiifu, wasikivu na mengine mengi. Hii ni silaha kubwa sana sema wengi wetu huwa tunajisaha kuitumia, na ukifanikiwa kuitumia hii itakurahisishia malezi ya watoto wako.
 
Mtoto hata miaka miwili hana kumpa adhabu YOYOTE ni kumuonea tu. Jaribu kuongea nao hapo Nyumbani waisome ratiba yake na wamsome na yeye pia.

Ninae wa hivyo, ye ana nwaka mmoja tu lakini home wanachezeaga sana vibao vyake wakimletea ujinga. Wanajitahidi kutokumuuzi lakini ukimsema vibaya tu ni kama vile anasikia, soon utakula vibao vyake.

Ana kajitundu kwenye sikio na nimeambiwa ndio sababu nami nimeamini hivyo.

Kama mtoto wako anatabia kama ya mtoto wa huyu jamaa basi hana tatizo mpe muda atabadilika tu.
 
......mimi huyu wangu naye ni hasira na ubishi. Mtoto yupo 4 yrs lakini anafanya vitu kama mkubwa.

Alivyokuwa na 2 yrs ukimuudhi au akitaka kitu apate muda huo huo, otherwise anajiangusha.......nikaanza kumpa viadhabu akaacha.

Sasa tokea miaka 3 hadi sasa 4 kaanzisha tabia ya kurusha vitu na kubamiza milango, yaani ukimuudhi lazima atafute kitu cha kuharibu kwa kurusha au kubamiza milango.

.....nimeanza kumstua kwa kumchapa sometimes, basi ukimchapa atakwambia stop hitting me! Namwambia nakuchapa kwa sababu umefanya hivi, ni kosa.

Wiki 2 hizi naona kama ameanza kustop kurusha vitu, ila milango anabamiza na kanasema leave me alone. Hii bado nafanyia kazi.

Usione watu tumekuwa, kumbe wazazi walifanya kazi sana kulea. Kulea mtoto ni another full-time job, unatakiwa ufanye kwa hekima kweli.

Kweli kulea ni kibarua kigumu kweli kweli
 
Duu! Humu yamo mengi kweli mimi wa kwangu ana miaka miwili sasa lakini yeye akiudhika hasa kwa kucheleweshewa huduma mfano chakula, kufokewa (kukaripiwa) anapokosea, n.k yeye anajitupa chini haijalishi ni wapi na kuna hali gani mfano amewahi jitupa chini sehemu yenye mawe na aliumia sana. Juzi kajitupa chini kwenye matope (mvua ilikuwa imemaliza kunyesha).

Namimi nisaidieni nifanyeje!
 
pls hayo yote ni utoto tu hakuna mapepo wala nn,anashindwa kufika ujumbe hiyo ndio anaona ni njia sahihi hivyo mpatie kile kitu ambacho anataka,akikua ata acha watu wanasema tu mfano mtu anasema mkate mitama kweli huyu anaonyesha ata mtoto hana kabisa
 
Dah, malezi ni kazi kubwa sana, wakati mwingine Mzazi unachanganyikiwa na kushindwa kuelewa kipi bora kwa mwanawe. Nakumbuka kipindi mtoto wangu wa pili ana umri wa miezi kadhaa alikuwa na tabia ya kulia usiku, yaani yeye akiamka anachezaaa akiona hana kampani anaanza kulia non-stop, hata ukiamka umbembeleza hanyamazi, atalia kwa mda mrefu sana bila sababu. Nakumbuka sku moja alilia namna hiyo kwa mda mrefu, nilijaribu kumbembeleza sana lakini alionekana amejawa na hasira na hakujali kubembelezwa kwake, ghafla na mimi hasira zilinipanda nikamlaza kifudifudi na kumtandika vibao kama vinne vya makalio, then nikamwambia "nyamaza", alinyamaza haraka sana na kuanzia siku hiyo hakuwahi kulia tena usiku bila sababu, mpaka anakuwa hakuwahi tena kudeka kijingakijinga, hajawahi tena kuwa na vilio vya sauti ya juu kama mtoto wa uswahilini. Sikumbuki mara ya mwisho nimewaadhibu lini watoto wangu, lakini nikiwaadhibu ni lazima kabla ya hapo lazima nifanye nao mahojiano na walitambue kosa lao. Japo inauma sana kupiga mtoto lakini inauma zaidi kuwa na mtoto kiburi!
 
Back
Top Bottom